Hata kama utaamua kumuua bado haina maana………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata kama utaamua kumuua bado haina maana………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 1, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wengi ambao wanaamini katika jambo hili, kwamba kama mtu hana wivu, ina maana kuwa hampendi mpenzi wake. Wanaamini hivyo, kiasi kwamba wapenzi wao wanapokuwa na wivu juu yao hujisifu kwamba wanapendwa. Hali hii inatokana na kutofahamu tofauti iliyopo kati ya kupenda na kutamani au tendo la ndoa.

  Hofu za kuachwa na mwenzake humfanya mpenzi kutoruhusu mambo fulani, humfanya kuchukua juhudi za kumlinda huyo mpenzi asikutane na mtu mwingine wa jinsia tofauti. Je hujaona wapenzi wanapigana na kutoana roho kwasababu ya mwenzake kumwangalia sana mwanamke au mwanaume fulani? Halafu bado unaita kwamba mtu mwenye wivu anapenda.

  Kuongea ndiyo kabisa kwani kuna wakati mwanaume au mwanamke humkataza mwenzake asiongee na mtu yeyote wa jinsia tofauti, labda tu yule ambaye amekubaliwa kuongea naye. kila wakati mtu anahofu kwamba mwenzake atachukuliwa. Halafu mtu bado anataka tuamini kwamba huko ndiyo kupenda.

  Kumbuka kwamba upendo unakuwa wa kweli na mzuri pale unapotolewa kwa hiari, bila kutisha wala kulazimisha, bila kuhangaika, bila tafrani. Pale ambapo mpenzi au wapenzi wamefungwa kutokana na wivu. Upendo hapo hauwezi kuchipuka. Kwenye kulazimishana, kufungana, na kulindana upendo haumei.

  Unapomlinda mtu, kumbuka umemshusha sana kiasi kwamba unamchukulia kama kifaa, chombo, kama mali na sio binadamu. Yule anayeonewa wivu naye ataendelea kuwepo kwenye uhusiano na siyo kwa sababu anampenda hapana atakuwa kwenye uhusiano kwa sababu nyingine. Utampenda vipi mtu ambaye anakulinda na kukuchunga, mtu asiyeamini kwamba unaweza kulinda mwili wako mwenyewe?

  Tendo la ndoa linapopewa uzito mkubwa kwenye uhusiano wivu ni lazima utakuwa mkubwa. Mtu akiacha tendo la ndoa na wivu huondoka. Wapenzi ambao hawapendani na kufikia mahali hakuna anayetaka kusikia kuhusu tendo la ndoa, kamwe hawaoneani wivu. Unafikiri ni kwa nini? Ni kwasababu wivu unatoka kwenye tendo la ndoa na siyo mahali pengine.

  Kwa hiyo ukitaka kuacha wivu inabidi ulibadili swala la ndoa liwe upendo. Kama ukipenda mtu ile kumpenda tu ni dhamana na usalama wa kutosha kuwa hatakwenda kwa mtu mwingine. Kama kweli unampenda mtu utajua kwamba huwezi kwenda kwa mtu mwingine. Lakini kama akienda ujue hakuna upendo na huwezi kufanya lolote ameamua kwenda ni yeye. Hata kama utaamua kumuua bado haina maana kwa sababu maiti haina matumizi yeyote ya maana huwezi kuipenda.

  Kama kuna wivu ujue kabisa hakuna upendo bali hapo kuna tamaa ya mwili ambayo imefichwa nyuma ya neno kupenda. Kilichopo kati yenu ni tendo la ndoa tamaa ya mwili lakini siyo upendo. Mtu anayependa analijua jambo hili kwa sababu hana wivu. Hivyo hana shida ya kukagua simu ya mwenzake kuchakura mifuko au mikoba yake au kumtumia watu wamlinde.
   
Loading...