Hata kama mkataba na mwekezaji ungekuwa 50-50 bado tungekuwa tumeibiwa!

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,394
4,748
Nasikitika sana kuona hata wale wanaojiita wasomi na tena kwa kusomeshwa na fedha za masikini wanavyojaribu kuwalemaza watoto wa shule za kata kwa kupiga kelele za mtandaoni huku wakiwa nje ya mada.

Kilichotokea ni kwamba acacia wanadanganya kiasi na aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga (pengine kwa kushirikiana na TMAA ) na hatimaye serikali haipati kodi yake husika ....yaani ile 4% sijui inaitwa mrabaha.

Hivyo hata kama mkataba wetu ungekuwa umeundwa kwa sisi kupata 50% bado Acacia wangekuwa wametupiga.

Hoja ya msingi hapa ni kwamba hata kama ule mkataba ungeandikwa na Rafiki yangu Tundu lissu na kuwa mzuri kiasi gani bado leo hii tungeongelea hili kosa lililofanywa na TMAA(ndio maana wamepigwa chini) pengine kwa kushawishiwa au kuhongwa au kudanganywa na Acacia
.

Swali la kizushi:
Hivi waziri kivuli wa nishati na madini ana maoni gani kuhusu ripoti au anasubirua upepo unavyovuma ndio ajitose?
 
Tundu Lissu hajui hata namna ipi bora ya kushauri nchi inapokuwa vitani ....anaropoka kama vile ni ile michezo ya Chadema vs CCM ....anakuja na ngojera za kuanza kupigania issues za madini toka 99 na anatumia kigezo hicho kuponda kuwa hatuibiwi kwenye mchanga!!! ....hivi hiyo mikataba hata kama ingekuwa na ubora kiwango anachotaka yeye ....itaweza kuzuia udanganyifu kama huu ukihusisha maafisa wa serikali? Mbona anamshambulia JPM kuwa anajua alikuwa upande upi kipindi mikataba inasainiwa lakini hawataji mawaziri wakuu walioshiriki kama wakuu wa serikali ambao wapo nao huko Chadema? ....Tundu Lissu asitake kutafuta sifa kwenye issues za kitaifa ....maoni yake ni kama anatamani kuwasaidia ACACIA kuishtaki serikali .....atafute namna ya kutoa maoni yake kwa faida ya taifa na si kuropoka ovyo kama vile hii ni siasa .....Tundu Lissu amevimba kichwa inabidi aambiwe ukweli ....
 
Ni kweli mleta uzi usemacho, lakini ni aibu kujadili mrabaha wa 3%. Kujadili kipato hicho hata kama hatuibiwi huo ndio wizi mkubwa kuliko hata wa huo mchanga wenyewe. Tukubaliane tu kuwa hicho kiwango ni kidogo sana, sasa ni wakati muafaka wa kuipitia hiyo mikataba upya kwa wote tunakubaliana kuna walakini wa mikataba hiyo.
 
Tundu Lissu hajui hata namna ipi bora ya kushauri nchi inapokuwa vitani ....anaropoka kama vile ni ile michezo ya Chadema vs CCM ....anakuja na ngojera za kuanza kupigania issues za madini toka 99 na anatumia kigezo hicho kuponda kuwa hatuibiwi kwenye mchanga!!! ....hivi hiyo mikataba hata kama ingekuwa na ubora kiwango anachotaka yeye ....itaweza kuzuia udanganyifu kama huu ukihusisha maafisa wa serikali? Mbona anamshambulia JPM kuwa anajua alikuwa upande upi kipindi mikataba inasainiwa lakini hawataji mawaziri wakuu walioshiriki kama wakuu wa serikali ambao wapo nao huko Chadema? ....Tundu Lissu asitake kutafuta sifa kwenye issues za kitaifa ....maoni yake ni kama anatamani kuwasaidia ACACIA kuishtaki serikali .....atafute namna ya kutoa maoni yake kwa faida ya taifa na si kuropoka ovyo kama vile hii ni siasa .....Tundu Lissu amevimba kichwa inabidi aambiwe ukweli ....
Endeleeni kumshambulia Lissu kana kwamba yeye ndo adui mkubwa wa nchi hii. Tatizo la ukweli ni kwamba huuma mno unapoambuwa. Tatizo siyo madini yaliyopo kwenye mchanga ambapo hata hivyo mkataba unatambua mashapo ya dhahabu tu. Mchanga na na Madini mengineyo yaliyopo kwenye huo mchanga ni mali ya muwekezaji.

Sasa nyie mnaambiwa mikataba ndo tatizo mnaanza kuimba habari za akina Lowassa na Sumaye kana kwamba mmewajua leo. Hizi reactions zenu ni kwasababu tu ya stress what you are doing is just redirected aggression to relieve yourself lakini haiondoi ukweli kuhusu blunder zilizofanywa na Mkapa ambaye hamumtaji hata kidogo mnakimbilia Lowassa na Sumaye kwasababu walishaondoka huko.

Just deal with the reality.
 
Back
Top Bottom