Hata kama kimbunga hakijatokea hatupaswi kuwabeza watabiri

dogo kubwa

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2016
Posts
798
Reaction score
697
Tulipokea tahadhari kutoka idara inayohusika na utabiri wa hali ya hewa, ikitutahadharisha juu ya uwezekano wa tufani na hata mafuriko katika mikoa ya kusini.

Mpaka muda huu bado hayajatokea, binafsi sijafurahishwa na baadhi yetu kuanza kuwabeza waliotuletea tahadhari hiyo.

Kwanza pamoja na kutimiza wajibu wao, wameifanya kazi hiyo kwa upendo mkubwa. Siamini kuna yeyote kati yao alipanga kuwafanya wana Mtwara washinde njaa airport na waishi kwa taharuki.

Pili wanapata taarifa kwa njia ya picha za satellite na wanazitafasiri kadiri ya utaalamu wao. Nani asiyejua kuwa human knowledge is limited, kwa vyovyote wamefanya yote yaliyokuwa kwenye uwezo wao kutufanya tuishi kwa usalama.

Kama kimbunga hakijatokea, tumshukuru Mungu na wote wanaoendelea kuomba kisitokee, tusibeze utabiri wa hali ya hewa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mwanzo kabisa walikanusha
Baadae walivyochungulia kwenye vyombo vya wenzao
Wakajifanya kutembea kifua mbereee kua wakazi wa Pwani ya bahari ya hindi haswa katika mikoa ya Lindi na Ntwara tujiandae kumpokea mgeni.
 
Wanasayansi wa bongo uchwara kweli kweli[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna jinga moja limehojiwa na mwandishi wa habari limesema hivi: nanukuu" Mimi sijafurahishwa na hiki kimbunga kutokutokea hapa mtwara sababu nilitaka nione kinafananaje maana huwa nasimuliwa tu sijawahi kuona""
 
TMA wana vifaa duni.Wametupa taharuki tu
 
Hao watabiri hawabezwi kwa hilo suala la kimbunga tu, bali utabiri wao wote huwa hawapatii, ni kama utabiri wa waganga wa kienyeji. Kwa maneno marahisi wanakula hela za bure wakati hawana tija yoyote. Mjinga tu ndio anaweza kuamini utabiri wa TMA.
 
Tulipokea tahadhari kutoka idara inayohusika na utabiri wa hali ya hewa, ikitutahadharisha juu ya uwezekano wa tufani na hata mafuriko katika mikoa ya kusini.

Mpaka muda huu bado hayajatokea, binafsi sijafurahishwa na baadhi yetu kuanza kuwabeza waliotuletea tahadhari hiyo.

Kwanza pamoja na kutimiza wajibu wao, wameifanya kazi hiyo kwa upendo mkubwa. Siamini kuna yeyote kati yao alipanga kuwafanya wana Mtwara washinde njaa airport na waishi kwa taharuki.

Pili wanapata taarifa kwa njia ya picha za satellite na wanazitafasiri kadiri ya utaalamu wao. Nani asiyejua kuwa human knowledge is limited, kwa vyovyote wamefanya yote yaliyokuwa kwenye uwezo wao kutufanya tuishi kwa usalama.

Kama kimbunga hakijatokea, tumshukuru Mungu na wote wanaoendelea kuomba kisitokee, tusibeze utabiri wa hali ya hewa.
Kitatokea ghafla siku ambayo haijatabiriwa
 
Hao watabiri hawabezwi kwa hilo suala la kimbunga tu, bali utabiri wao wote huwa hawapatii, ni kama utabiri wa waganga wa kienyeji. Kwa maneno marahisi wanakula hela za bure wakati hawana tija yoyote. Mjinga tu ndio anaweza kuamini utabiri wa TMA.
Mimi nashukuru tu kuwa this time uta iri wao umekuwa si kweli tena maana ungeluwa kweli ingekuwa shida
 
Back
Top Bottom