Ni maoni yangu tu, kutokana na hiyo gia iliyobadilishwa angani. Hatari yake imeshaanza kuonekana, ni kudondokea baharini na kuangamia.
Nasema tu kwa kifupi kuwa CHADEMA asili, kabla haijauzwa na kutekwa na mafisadi, ingeweza kushinda uchaguzi mwaka huu 2015. Hata kama isingeshinda, kupitia mgombea yeyote, isingesambaratika, iwe ndani au nje ya kinachoitwa UKAWA.
Lakini sasa kwa kosa la tamaa: ya fedha, madaraka, na kwa kitendo cha kubadili misingi iliyoisimamia CHADEMA, (nazungumzia CHADEMA tu kwa sababu ilikuwa chama kilichokaribia kutuletea matumaini), naona upinzani, na hasa CHADEMA wanapoteza yote: Uchaguzi huu mgombea wao hatashinda, na mbaya zaidi baada ya uchaguzi, mi sio mtabiri, ila hali halisi inadhihirisha kuwa CHADEMA itasambaratika rasmi. Itasambaratika kwa sababu mafisadi waliokivamia watarudi labda waliokotoka.
CHADEMA itabaki, lakini sio imara tena kama awali, kwani ilishabomoa misingi yake iliyosimamia. Wachache waliopinga gia kubadilishiwa angani hawatakuwa na nguvu tena ya kutetea au kurudisha misingi iliisimamia. Kwa ujumla upinzani uliokuwepo awali wote utatikiswa. Vyama vikuu kama CUF na CHADEMA vitabaki vya kipinzani na upinzani dhaifu baada ya nguzo zake kutikiswa.
Siipendi CCM, ila sipendi pia ugeugeu wa CHADEMA wa kukumbatia tena ufisadi na mafisadi waliotuaminisha kuwa ndiyo wanaoitafuta Nchi.
CHAMA kilinunuliwa, ... sasa tumeambiwa tena kinapigwa tena bei kwa "matajiri wa tano", unategemea nini baada ya uchaguzi wakishinda, au na wasiposhinda?
Ni hayo tu, tukutane baada ya Oktoba 25.