Hata hili pia lahitaji kupigiwa kelele!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata hili pia lahitaji kupigiwa kelele!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mjomba wa kale, Feb 3, 2012.

 1. mjomba wa kale

  mjomba wa kale JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ninakosa imani na SPIKA na NAIBU wake kwakushindwa kulipa suala la mgomo wa madaktari kipaumbele na kuruhusu lijadiliwe na wabunge kama hoja ya dharura kutokana na sintofahamu ya tamko rasmi la serikali kuhusu suala hilo huku wagonjwa(wananchi) wakizidi kupoteza maisha, ninajiuliza hata hili la kuhitaji utashi tu ambalo liko wazi na linawaangamiza waliowaweka pale na kujiona MIUNGU watu kiasi kwamba kujifanya nao watetezi wa serikali kwa kila kitu huku wakihojiwa wanajigamba wote tuko hapa kwaajili ya kutetea wananchi ni wananchi gani wanaowatetea wao katika hili sikubaliani kabisa na kauli hiyo waliozowea kuitoa mara kwa mara inasikitisha sana kwakweli TUNAHITAJI MAGEUZI MAKUBWA SANA HAPA NCHINI la sivyo tutaangamia wote huku tuliowapa dhamana ya kutusemea serikalini wakituangalia ilimradi wao wanaingiza mkate wao wa kila siku!.
   
Loading...