Wimbi la wana CCM waliokimbilia CDM kwenye uchaguzi wa mwaka jana na sasa kuanza kurudi CCM litarajiwe kuendelea kuongezeka kutokana na karibu tanzania nzima kuvutwa na utendaji kazi wa Magufuli lakini pia tabia ya wanasiasa wengi kusaka fursa za uongozi
Kwenye mkutano wa kamati kuu ya CCM tuliwashuhudia mzee Msindai na Mpendazoe wakirejea CCM huku wakieleza mengi ni kwanini wamepata maamuzi yakuondoka CDM nakureja CCM.
"Kule kwa wenzetu sifa moja kubwa yakupata vyeo ni vurugu",Haya ni maneno ya Mpenda Zoe ambayo moja kwa moja unapata jibu kwamba baadhi yao walikimbilia fursa za uongozi lakini bado roho zao zipo CCM hasa kipindi hiki cha utendaji kazi mzuri wa Magufuli hivyo walihama CCM baada yakuona fursa za uongozi kwa wakati ule hawakuzipata.
Hata James Lembeli alichokionesha jana na maneno alioyatamka utagundua kwamba wakati wowote anarudi CCM,"Kama utakisafisha chama mimi nitarudi na mkia wangu".Hapa utagundua kwamba kwa sharti hili mpaka sasa Lembeli si mwana Chadema tena lakini hemu jiulize swali hili:
Je kama James Lembeli angeupata Ubunge mwaka jana kupitia CDM angeweza kurejea CCM?
Lakini hakika Lembeli atarudi CCM baada yakuona fursa za uongozi ziko vizuri na nawahakikishia roho ya Lembeli haipo CDM kwa sasa na 2020 atawania ubunge kupitia CCM.
Kabla yakumaliza na Bulaya tujikumbushe kisa cha John shibuda wa Maswa ambaye kilicho muondoa CCM wakati ule ni kuenguliwa kwenye kura za maoni akakimbilia CDM na kushinda ubunge lakini badae alipoona CDM fursa napo zimebana aliondoka.
Eater Bulaya naye halikadhalika ni Mbunge wa CDM aliyehama kutoka CCM dakika za mwisho kabisa baada yakukosa nafasi kwenye kura za maoni ndipo akapata maamuzi yakuhamia CDM na hatimaye kushinda ubunge na hii ndio salama ya CDM,ila ni imani yangu kama 2020 akikabwa koo nakuangukia pua tutarajie naye kutubu nakurejea CCM.
Hivyo kinacho wasumbua wanasiasa wetu hasa wa Tanzania na Africa kwa ujumla si uzalendo bali ni kusaka vyeo