gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,297
- 3,319
Wimbi la wana CCM waliokimbilia CHADEMA kwenye uchaguzi wa mwaka jana na sasa kuanza kurudi CCM litarajiwe kuendelea kuongezeka kutokana na karibu tanzania nzima kuvutwa na utendaji kazi wa Magufuli lakini pia tabia ya wanasiasa wengi kusaka fursa za uongozi
Kwenye mkutano wa kamati kuu ya CCM tuliwashuhudia mzee Msindai na Mpendazoe wakirejea CCM huku wakieleza mengi ni kwanini wamepata maamuzi yakuondoka CHADEMA nakureja CCM.
"Kule kwa wenzetu sifa moja kubwa yakupata vyeo ni vurugu",Haya ni maneno ya Mpenda Zoe ambayo moja kwa moja unapata jibu kwamba baadhi yao walikimbilia fursa za uongozi lakini bado roho zao zipo CCM hasa kipindi hiki cha utendaji kazi mzuri wa Magufuli hivyo walihama CCM baada yakuona fursa za uongozi kwa wakati ule hawakuzipata.
Na hili liko wazi kwani hata Mwapachu alizungumza kilichomuondoa CCM mwaka jana ni ahadi ya cheo kutoka kwa Lowasa na nafikiri mmeona kilichotokea baada ya kukikosa tu akarudi tena CCM.
Hata James Lembeli alichokionesha jana na maneno alioyatamka utagundua kwamba wakati wowote anarudi CCM,"Kama utakisafisha chama mimi nitarudi na mkia wangu",lakini pia aliongeza nakusema,"Kubadilisha msikiti sio kuacha uislam,nyumba ikisafishika nitarudi",Hapa utagundua kwamba kwa maneno hayo mpaka sasa Lembeli si mwana CHADEMA tena lakini hemu jiulize swali hili:
Je kama James Lembeli angeupata Ubunge mwaka jana kupitia CHADEMA angeweza kurejea CCM?...Lakini hakika Lembeli atarudi CCM baada yakuona fursa za uongozi ziko vizuri na nawahakikishia roho ya Lembeli haipo CHADEM kwa sasa na 2020 atawania ubunge kupitia CCM.
Kabla yakumaliza na Bulaya tujikumbushe kisa cha John shibuda wa Maswa ambaye kilicho muondoa CCM wakati ule ni kuenguliwa kwenye kura za maoni akakimbilia CHADEMA na kushinda ubunge lakini badae alipoona CHADEMA fursa napo zimebana aliondoka.
Esther Bulaya naye halikadhalika ni Mbunge wa CHADEMA aliyehama kutoka CCM dakika za mwisho kabisa baada yakukosa nafasi kwenye kura za maoni ndipo akapata maamuzi yakuhamia CHADEMA na hatimaye kushinda ubunge na hii ndio salama ya CHADEMA,ila ni imani yangu kama 2020 akikabwa koo nakuangukia pua tutarajie naye kutubu nakurejea CCM.
Hivyo kinacho wasumbua wanasiasa wetu hasa wa Tanzania na Africa kwa ujumla si uzalendo bali ni kusaka vyeo