PreGE2025 Hassan Doyo achukua Fomu ya Urais kupitia Chama cha NLD, ataja vipaumbele Kumi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Katibu Mkuu wa chama cha National League for Democracy (NLD), Hassan Doyo amechukua fomu ndani ya chama hicho kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania urais wa Tanzania, huku akieleza sababu ya kutaka nafasi hiyo, akibainisha vipaumbele kumi.

Doyo amesema vipaumbele hivyo atavitumia iwapo chama hicho kitampitisha kuwania urais kuvinadi kwa wananchi ambao nao wakimpa ridhaa ya kuwaongoza atavitekeleza.

Screenshot 2025-03-20 171723.png
Katibu mkuu huyo anajitosa ndani ya chama hicho kuungana na vyama vingine vinne, ambavyo navyo harakati za kuwapata wagombea zinaendelea ili kwenda kuchuana Oktoba 2025 kwenye uchaguzi huo.

Mbali na Doyo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu naye ameonesha nia ya kuwania urais, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Bara, Innocent Siriwa naye ameonesha nia ndani ya chama chake.

Soma, Pia: Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Dorothy Semu atangaza nia ya kuwania Urais mwaka 2025

Wote hao Semu na Siriwa wamebainisha vipaumbele vyao na kusubiri michakato ya ndani ya vyama vyao kumpata mgombea mmoja.

Soma, Pia
 
Ivi urais tunauchukuliaje
Vyama washirika wa ccm anapewa fungu la kuzunguka mikoani na yeye anaishi umo.

Ndio sababu ya kufutwa kwa ruzuku kwa vyama ambavyo havina vigezo.

Mwaka 1995 mzee Mwinyi alitowa ruzuku kwa wagombea wote wa ngazi zote na mawakala wa vyama vyote, watu wakaona ni mradi vyama vikaota kama uyoga ruzuku ikapigwa lock.
 
Katibu Mkuu wa chama cha NLD, Hassan Doyo amechukua fomu ndani ya chama hicho kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania urais wa Tanzania, huku akieleza sababu ya kutaka nafasi hiyo, akibainisha vipaumbele kumi.

Doyo amesema vipaumbele hivyo atavitumia iwapo chama hicho kitampitisha kuwania urais kuvinadi kwa wananchi ambao nao wakimpa ridhaa ya kuwaongoza atavitekeleza.

Katibu mkuu huyo anajitosa ndani ya chama hicho kuungana na vyama vingine vinne, ambavyo navyo harakati za kuwapata wagombea zinaendelea ili kwenda kuchuana Oktoba 2025 kwenye uchaguzi huo.

Mbali na Doyo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu naye ameonesha nia ya kuwania urais, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Bara, Innocent Siriwa naye ameonesha nia ndani ya chama chake.

Soma, Pia: Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Dorothy Semu atangaza nia ya kuwania Urais mwaka 2025

Wote hao Semu na Siriwa wamebainisha vipaumbele vyao na kusubiri michakato ya ndani ya vyama vyao kumpata mgombea mmoja.

Soma, Pia
Hapo ni utakatishaji ili Ccm ionekane ilishindana na upinzani.
 
Katibu Mkuu wa chama cha National League for Democracy (NLD), Hassan Doyo amechukua fomu ndani ya chama hicho kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania urais wa Tanzania, huku akieleza sababu ya kutaka nafasi hiyo, akibainisha vipaumbele kumi.

Doyo amesema vipaumbele hivyo atavitumia iwapo chama hicho kitampitisha kuwania urais kuvinadi kwa wananchi ambao nao wakimpa ridhaa ya kuwaongoza atavitekeleza.

Katibu mkuu huyo anajitosa ndani ya chama hicho kuungana na vyama vingine vinne, ambavyo navyo harakati za kuwapata wagombea zinaendelea ili kwenda kuchuana Oktoba 2025 kwenye uchaguzi huo.

Mbali na Doyo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu naye ameonesha nia ya kuwania urais, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Bara, Innocent Siriwa naye ameonesha nia ndani ya chama chake.

Soma, Pia: Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Dorothy Semu atangaza nia ya kuwania Urais mwaka 2025

Wote hao Semu na Siriwa wamebainisha vipaumbele vyao na kusubiri michakato ya ndani ya vyama vyao kumpata mgombea mmoja.

Soma, Pia
Ndio nani huyo huko dar ?!
Ngoja nami nije dar nitafute chama chochote nigombee alafu kwenye kampeni namtaja mama nama mamaaa... baada ya uchaguzi sikosi ukuu wa wilaya
 
Back
Top Bottom