Hasira dhidi ya Marekani hazikuanzia na video | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hasira dhidi ya Marekani hazikuanzia na video

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 27, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Nizar Visram
  WIKI iliyopita tulizungumzia maandamano dhidi ya Marekani yalivyoenea kote duniani, kufuatia video iliyoandaliwa Marekani ikishambulia Uislamu. Baada ya hapo maandamano yamezidi kuendelea licha ya Marekani kutuma majeshi na manowari zake mashariki ya kati.


  Kwa mfano, huko Yemen baada ya manowari kuwasili pamoja na majeshi 250, wabunge walilaani kitendo hicho na kusema hawatakubali majeshi ya Marekani nchini mwao.


  Jijini Cairo maelfu waliandamana, wakakwea kuta za ubalozi wa Marekani, wakateremsha bendera na kupandisha bendera nyeusi ya Kiislamu. Wakaandika ukutani “Tahadhari Marekani, kuna Osama Bin Laden bilioni 1.5 duniani.”
  Na nchini Lebanon wananchi wanaokadiriwa 500,000 waliandamana, wakati huko Afghanistan maelfu ya wananchi waliandamana huku wakiimba “Kifo kwa Marekani” na kuchoma magari ya Serikali. Wakatupia mawe kambi ya majeshi ya Marekani na kuchoma makontena yao.


  Serikali ya Pakistan ilitangaza siku ya Ijumaa ni ya mapumziko ili wananchi waweze kuandamana. Maelfu wakaitika, wakachoma bendera ya Marekani na sanamu ya Obama. Wawili waliuawa na 70 wakakamatwa wakati polisi walipofyatua risasi za moto na mabomu ya machozi. Hata hivyo, wengine walimudu kuparamia ukuta wa ubalozi wa Marekani.


  Nchini Ufaransa Serikali ilipiga marufuku maandamano. Waziri Mkuu alitangaza kuwa hakuna sababu kwa raia wa Ufaransa kuandamana kuhusu suala la “kigeni.” Hii ni siku moja baada ya wananchi kuandamana jijini Paris hadi ubalozi wa Marekani na Wizara ya Mambo ya Ndani. Polisi waliwakamata waandamanaji 100.


  Huko Bangladesh, India, Indonesia na Ufilipino pia maelfu waliandamana, wakichoma bendera za Marekani na Israeli mbele ya ubalozi wa Marekani.


  Maandamano yanayoendelea hivi sasa yalianza baada ya balozi wa Marekani nchini Libya kuuawa na ubalozi kushambuliwa kwa mabomu na maroketi.


  Huyu ni balozi aliyekuwa mwandani wa Gaddafi, akionana naye mara kwa mara. Kwa mujibu wa mtandao wa Wikileak, balozi huyo alikuwa akimsifu Gaddafi katika ripoti zake za siri alizotuma Washington. Kwa nini?


  Kwa sababu Gaddafi alikuwa akishirikiana na mataifa ya magharibi, tena kwa hali na mali. Kwa mfano, mnamo 2006 alitumia majeshi yake kuzuia maandamano dhidi ya Denmark. Askari wake walifyatua risasi na kuwaua watu kumi na moja.


  Pia alikuwa akiisaidia Marekani katika kuwatesa na kuwafunga wafuasi wa Al Qaeda, kazi ambayo pia ilifanywa na Mubarak wa Misri na Assad wa Syria. CIA ilikuwa ikiwakamata watuhumiwa wa ugaidi kote duniani na kuwakabidhi kwa Gaddafi ili “awashughulikie”


  Tony Blair naye akatembelea Libya na kuzungumza na Gaddafi jinsi ya kupambana na “ugaidi”. Baada ya hapo Shirika la Ujasusi la Uingereza (MI6) likawakamata wapinzani wa Gaddafi nchini Uingereza na kuwarejesha Libya.


  Licha ya yote haya Gaddafi akauliwa kwa msaada wa NATO na maiti yake ikavuliwa nguo na kudhalilishwa kinyama. Hillary Clinton akawasili Libya, akashangilia na kufurahia.


  Hakujali kuwa Libya ilikuwa imemeguka, wakati waasi waliopewa silaha, fedha na mafunzo na NATO, Saudia na Qatar wanatamba bila ya kujali Serikali ya Tripoli


  Ndio maana mnamo Januari mwaka huu kikundi cha wapinzani kilivamia makao makuu ya Baraza la Mpito la Taifa (NTC). Halafu mnamo Aprili msafara wa UN ulishambuliwa kwa mabomu. Na mwezi Mei ofisi za msalaba mwekundu zilipigwa roketi. Kisha msafara wa balozi wa Uingereza ulishambuliwa mnamo mwezi Juni, na Agosti bomu liliripuka mbele ya ubalozi wa Marekani.


  Hivyo hasira hazikuanzia na hii video, bali ni matokeo ya sera za kibeberu ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu. Hata kuuawa kwa balozi huko Benghazi si mara ya kwanza, kwani nchini Afghanistan balozi wa Marekani aliuawa mwaka 1979.


  Hasira hii inaongezeka. Utategemea nini wakati, kwa mfano, hivi majuzi ndege ya NATO iliwaua wanawake tisa nchini Afghanistan wakati wakiwa wanakusanya kuni za kupikia. Maelfu wamekufa kwa njia hii. Wakati huo huo askari wa Serikali ya Afghanistan anafyatua risasi na kuwaua wanajeshi wanne wa Marekani. Kwa njia hii tayari askari wa NATO zaidi ya 50 wameuawa na ‘wanafunzi’ wao.


  Si ajabu hasira inaongezeka. Obama alipoingia madarakani aliahidi kubadilisha sera ya ukandamizaji huko mashariki ya kati, lakini leo baada ya miaka minne hakuna kilichobadilika.


  Licha ya ahadi aliyotoa, Obama ameendelea kuwafunga na kuwatesa watuhumiwa katika gereza la Guantanamo bila ya kuwafikisha mahakamani. Ameendelea kutumia ndege za drone kuwaua maelfu katika nchi za Kiarabu, Asia ya kati na Afrika


  Marekani iliporomosha makombora huko Libya na sasa Syria kwa sababu ya “kuwalinda wapinzani wanaoandamana” dhidi ya Gaddafi na Assad. Sasa Obama anawaonya watawala wa Kiarabu wawadhibiti wanaoandamana dhidi ya Marekani. Mkuki kwa nguruwe.


  Lengo la ubeberu lilikuwa ni Libya iliyogawanyika, isiyoweza kujitawala yenyewe na inayotegemea majeshi na ‘misaada’ ya Marekani. Ndivyo walivyofanya Iraq, Afganistan na Libya na sasa wanafanya Syria na wanatarajia kufanya Iran.


  Matokeo yake ni kuwa waasi walewale waliojengwa na NATO huko Benghazi ndio waliomuua balozi. Inasemekana hata silaha walizotumia ni za NATO. Na huko Afghanistan askari waliofunzwa na Marekani sasa wanashirikiana na Taliban. Wachambuzi wanasema bomu lao linawaripukia mkononi.
  nizar1941@yahoo.com Hasira dhidi ya Marekani hazikuanzia na video
   
 2. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Mi nimesoma hako kauchambuzi kako lakini hata sijaona sehemu yoyote inayooanisha kifo cha huyo balozi na sababu nyingine zaidi ya filamu. Halafu hilo suala la hasira dhidi ya Marekani kutoka mataifa ya waarabu wala siyo kitu kipya hapa duniani. Kwahiyo mimi sioni kama umeleta kitu chochote kipya hapa zaidi ya kuzungukazunguka tuuuu. Lakini kama kawaida ya JF, kuna vilaza watakugongea LIKE za kumwaga tu pamoja na kuandika hewa na pumba.
   
 3. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,934
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  agggrrrrr ..... too much boasting ....
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hizi ni makala za nizar visram.
  hii amechemka kwa sababu alichoandika ni cha kawaida sana hakuna jipya kwa ujumla.
   
 5. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Sure, hakuna jipya lakini si vibaya kukumbushia historia huku nikiamini kwamba si wote wanayafahamu YOTE hayo yaliyoandikwa!! Don' Forget....:
  1. Wewe ukisema cha nini, mwenzako anasema atakipata lini...
  2. Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.....
  3.....Ongezea mwenyewe hapo!
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,734
  Trophy Points: 280
  Yan wewe dharau ni party yako ya maisha!oooh my sweety punguza kupanic.

   
 7. T

  Tukopampja Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Home » News
  [h=2]Waislamu wa Ahmadiyya wakumbusha mafundisho ya Mtume[/h]


  BY RESTUTA JAMES  26th September 2012


  [​IMG]
  Email  [​IMG]
  Print  [​IMG]
  Comments

  Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, imetahadharisha kuhusu maandamano yanayofanywa na Waislamu katika nchi mbalimbali kulaani filamu iliyomkashifu Mtume Muhammad (S.A.W) na kueleza kuwa njia hiyo kamwe haiwezi kutatua tatizo lililojitokeza.

  Badala yake, imewataka kutumia njia ya amani ikiwemo kueleza matendo mazuri ya Mtume Muhammad na uzuri wa dini ya Kiislam pamoja na kushinikiza kipengele cha kuzuia mtu yeyote kumkashifu kiongozi wa dini yoyote duniani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mohmood Chaudhry, alisema Waislamu wanayo haki ya kuonyesha hisia na kulaani filamu hiyo lakini sio kwa kuua ama fujo.

  “Pamoja na haki ya kuonyesha kukereka kwao, wale Waislamu walioamua kulipiza uovu kwa uovu kwa kuharibu mali za watu, kushambulia ofisi za kibalozi, kuua watu wasio na hatia na kufanya vurugu nao wamefanya kosa na wamekwenda kinyume na mafundisho ya Islam na ya Mtume mwenyewe wanaedai kutetea heshima yake,” alisema.

  Alisema Mtume Muhammad (S.A.W), alifundisha subira hasa katika hali ya kuudhiwa ama kutukanwa na kwamba alikuwa mfano kwa kuwa na subira pindi alipotukanwa au kudharauliwa wakati wa uhai wake.

  Alisema badala ya kufanya fujo, Waislamu wanapaswa kujibu hoja za wakorofi wanaoitukana dini hiyo na viongozi wake kwa kueleza uzuri na wema wa Mtume Muhammad na pia wafanye matendo mema kama kiongozi huyo alivyoelekeza.

  Alisema kufanya fujo kutatoa mwanya kwa wakorofi hao kuendelea kutoa dhihaka kwa Waislamu na wengine watajenga imani kwamba Uislamu ni dini ya vurugu jambo ambalo sio la kweli.

  “Viongozi wa nchi za Kiislamu na Waislamu wasomi kama wanasheria wanaoishi katika nchi za Magharibi wapaze sauti zao kushawishi dunia na hasa Umoja wa Mataifa kuweka sheria zitakazozibana nchi wanachama kutoruhusu raia wao kuwatukana waanzilishi wa dini yoyote duniani kwani jambo hilo linahatarisha amani ya dunia yote,” alisema Amir Chaudhry.

  Hivi karibuni, filamu ya “Innocence of Muslims” inayomdhalilisha Mtume Muhammad (S.A.W) iliyotayarishwa Sam Bacile nchini Marekani imeibua maandamano makubwa kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu walioipinga huku Waislamu nchini wakitaka ubalozi wa Marekani ufungwe.

  Wakati huo huo, Jumuiya ya Ahmadiyya inatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa 43 kwa siku tatu mfululizo kuanzia Septemba 28 mwaka huu, utakaofanyika Kitonga, Kata ya Msongola, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumzia mkutano huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam wa jumuiya hiyo, Waseem Ahmad, alisema utahusisha mafundisho ya Quran Tukjufu, umuhimu wa elimu kwa vijana wa Kiislamu, teknolojia ya habari na mawasiliano, ukombozi halisi wa mwanamke wa leo pamoja na mafanikio ya Jamaat kwa mwaka mmoja uliopita.

  Alisema mkutano huo utaambatana na misaada kadhaa kama vitabu, madaftari na vifaa vya tiba vitakavyotolewa kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
  SOURCE: NIPASHE


  0 Comments | Be the first to comment


   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  huyu mwandishi mwenyewe kila siku makala zake niza ki-"separationism", si ajabu ni moja kati ya wahamasishaji wanaolipwa na makudi ya magaidi.
   
 9. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  mh nafikiri inatakiwa kuwa Ganda la mua la jana chungu kaona mavuno
   
Loading...