Hashim Rungwe Sipunda: Huyu mnayemuita fisadi si mumkamate au nyie waongo?

Mimi namjibu kwa haraka na urahisi kabisa kwamba yote aliyoyataja ambayo ni mambo mazuri kabisa kufanywa na Serikali ya CCM, yamefanyika kwa kipindi cha miaka 10 pamoja na Awamu nyingine zilizopita yaani II na ya III, hivyo kutegemea kwamba ndani ya Mwaka I Awamu ya V ifanye mengi zaidi ya Awamu tatu zilizopita ni ujinga na kwanza hakuna mashindano kwani wote ni Viongozi wa CCM na wanatekeleza Ilani za CCM!

Ila nimefurahia kwamba Upinzani wamekubali kwamba CCM imefanya makubwa Tanzania kinyume na wengine ambao husema kwamba miaka 50 hakuna kilichofanyika, hivyo nimefurahi kwamba mme bow down kwamba Nchi yetu inasonga mbele tena kwa kasi ya ajabu kama Mpinzani alivyosema!

Swali ni: (chini ya CCM) nchi ilikuwa imepinda au la? Magufuli amedai au hajadai kwamba kazi kubwa na ya kwanza anayofanya ni kuinyoosha nchi iliyofika pabaya? Manazi wa Magufuli mnamsifu kwa "ujasiri" wa kupambana na ufisadi uliokithiri tawala zilizomtangulia, sio?

Kumpa Magufuli sifa ya kunyoosha nchi iliyopinda lakini hapohapo iliyoongozwa "vizuri" na viongozi wa CCM waliotangulia ndio wehu anaohoji mzee Rungwe.
 
Ni kawaida hiyo na hutokea Dunia nzima, ni hulka ya Binadamu, leo hii D.Trump amesema akiingia siku ya kwanza Januari 20. anafuta Obama care, sasa hvi tayari Chama cha Republican wameshaanza kushugulikia kufuta Obama care, pamoja na kufuta vikwazo vya Kiuchumi ambavyo Obama aliiwekea Urusi, na mambo mengine mengi ambayo Obama na Uongozi wake walifanya D.Trump amesema atabadilisha kama siyo kuyafuta kabisa, sasa unajua ni kwa nini Trump anafanya hivi?
Jiongeze ww nyumbu!Trump ni Democratic? Kweli we ni zigo
 
Bavicha mnahangaika sana masikini. Hata chizi akimkosoa rais mtakuja na thread kumuunga mkono kwasababu mnafanana tabia
Aaah Mh. Ali Hassan alipomtembelea Pombe alimalizia kwa kusema..kwa mwaka mmoja amefanya vyema kuliko awamu zote Pombe akakenua...Hivi unajua huyo Mzee alikua na maana gani?
 
Sijui waswahili tuna laana ya wapi. Hivi hii nchi maendeleo yake hupimwa kwa mifano aliyoitoa Rungwe? Kuwa Kariakoo inang'aa? Kuwa barabara zote lami? Kuwa university ziko zaidi ya 40? Kuwa viwanja vya ndege vinapanuliwa? Kuwa kuna mwendo kasi? Ndio vipimo vya maendeleo hivyo?

Hivi ukubwa wa kiwanja cha ndege unanisaidiaje mimi mwananchi wa kawaida ikiwa watalii na wafanyabiashara wa kimataifa wanatumia viwanja hivyo kutorosha nyara za serikali na kupitisha dawa za kulevya?

Hivi maghorofa ya kariakoo yaking'aa yanisaidia nini mimi mwananchi wa kawaida ikiwa wafanya biashara hao wanatoa rushwa na kukwepa kodi hivyo kuwa na faida mara dufu?

Hivi bara bara za lami zikiwa nchi nzima kwanini reli nayo isifanye kazi ya kusafirisha mizigo mizito kutoka pwani kwenda bara ili bei ziwe nafuu na barabara zidumu kuepusha gharama kubwa ya matengenezo ya barabara hizo kwa fedha ninayolipa kodi? Reli ilifia wapi? Mbona yenyewe haing'ai?

Hivi kuwa na vyuo vikuu 40 vibavyojazwa na watu wasio na sifa mpaka elimu inalazimishwa kuonekana nzuri wakati ni hovyo kwa kuweka mpaka division 5? Graduated wanaotoka katika vyuo hivyo 40 wanaenda wapi? Kuna mazingira ya ajira hata kujiajiri?

Mwendo kasi unamsaidia nini mwananchi wa Bunda?

Hivi hali ya huduma za afya mahospitalini Rungwe anaijua vizuri?? Hata sasa kaangalie huduma hata Bugando uone zilivyo mbovu (mbovu).

Majibu gani Rungwe ajibiwe? Kusoma hamjui hata picha?


Kwa kifupi Binadam hana jema.
Hivi wanyama wa porini kule Liwale wanamsaidia nini mwananchi maskini kule Lindi?
Kati ya Wale wanyama kule Liwale kwenye mbuga kubwa ulimwenguni ya shelui na ile barabara ya Dsm to Kibiti Lindi kipi kimemsaidia mwananchi maskini?
Bila shaka ni barabara.
Ongezeko la vyuo limesaidia sana kuliko hao wanyama ambao walikuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu lakini hawakumsaidia Mwafrika mpaka Elimu ilipokuja .
Leo hii kuna vyuo vya utalii na vya kujifunza mapishi mbalimbali na wanafunzi wake wameajiriwa kila mahali ndani na nje ya nchi.
Madawa ya kulevya yaliuzwa na watu binafsi kwa kujificha sana. Hata sasa bado yanauzwa tatizo ni kuwa vyombo vya habari vinaminywa kueneza taarifa kwa kuzikuza au kushusha heshma ya nchi.

Kuuzwa kwa wanyama kupitia kiwanja cha ndege ni uhalifu ma haiwezi kuwa ni kukosa maendeleo.
Hata nchi ziliziendelea zinasumbuliwa na uhalifu kama ugaidi n.k.

Kila serikali inajitahidi Kulinda wanyama na rasilimali nyingine ndio maana kuna askari wa wanyama pori na walikua wameajiriwa wengi sana awamu iliyopita.

Binadamu akishindwa kuwa na maendeleo ya majengo ya kisasa ,barabara za Lami ,viwanja vya ndege ,madaraja, umeme, maji, pesa za kununua chakula ,nguo , kujenga majengo bora ya serikali, elimu ,afya,maendeleo ya mawasiliano basi atakua hana tofauti na mnyama.
Binadam ataalendelea kuishi maisha kama wanyama wengine na hatakua na uwezo wa kulinda rasilimali alizopewa na mwenyezi Mungu kama atakua hana miundo mbinu bora.

Kifupi tu ni kwamba wanyama na rasilimali zote za asili zitafikia kikomo siku moja. Serikali zote zinajitahidi sana kurefusha muda wa hizo rasilimali za porini kuendelea kuwepo.
Ni lazima binadamu awe na maendeleo na utajiri wa kuweza kuwafuga hawa wanyama kwenye maeneo maalum yaani Zoo. Ni lazima binadamu atumie misitu ya asili kuishi maisha bora na sio kuwa mtumwa wa misitu. Akishauza miti ya asili na kujenga nyumba bora na kuishi maisha bora anatakiwa apande misitu yake mwenyewe. Na hapo atailinda kwa nguvu zake zote.

Kazi ya serikali ni kuhakikisha inakusanya kodi kwa juhudi na kwa kuweka mazingira bora ya kuwafikia walipa kodi. Awamu iliyopita ndiyo iliyoanzisha mashine za EFD kwa lengo la kukusanya kodi lakini kutokana na chuki za baadhi ya watu za kutaka kumkwamisha rais aliyekuwepo kwa makusudi walikua wakifanya maandamano ili kupinga matumizi ya EFD.

Nchi haiwezi kupinda kwenye idara . Kuna maeneo yamenyooka sana.
Ni vema yaliyopinda yakatajwa bayana ili kutofautisha.

Mfano baadhi ya Maeneo yaliyokuwa yamepinda ni pamoja na mfumo wa uchaguzi na usimamizi wake. Mfumo mbovu wa uchaguzi umekuwa ukitunyima viongozi bora wa kuwakilisha wananchi hasa wabunge.
Ukiwa na wabunge wabovu huwezi kuwategemea watunge sheria nzuri zaidi ya kupiga makofi na kutetea matumbo yao. Huku ndipo pa kunyoosha.

Sehemu nyingine iliyopinda ni demokrasia. Demokrasia yetu imepinda ndio maana chaguzi zinatawaliwa na rushwa na wizi wa kura hatimaye tunapata viongozi wezi.

Kutotii sheria na kanuni za nchi kwa watumishi na kwa raia nalo pia ni kati ya mambo yaliyopinda.

Riba kubwa kwenye mabenki nayo ni kati ya mambo yaliyoponda na yanahitaji kunyooshwa.
Migogoro ya ardhi kule Loliondo na kule Morogoro ni kati ya mambo yaliyopinda.
Wanafunzi wa chuo kukosa mikopo ni kupinda huko.
Misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini ni chanzo kikuu cha wakwepa kodi kujinufaisha kupitia humo na kuipindisha nchi.
Haya mapindo yote yanahitaji kutungwa kwa sheria na katiba inayozuia hayo na sio kutegemea kikundi cha watu wanaotumia mara nyingine jazba na chuki bila kuwepo kwa sheria. Mfano ni lazima pawe na sheria ya kusajili mali za watanzania wote ili tujue nani hastahili kuitwa maskini na nani anamiliki nini na alizipataje?

Swali la Hashim Rungwe ni " Je,nchi imepinda wapi na kuelekea upande gani?
 
Lakini hata huyu aliyeshindishwa urais hajui Saddam Hussein alikuwa Rais wa wapi wala hajui kwamba nchi zingine zinasaidia raia wake kusimama tena baada ya maafa.
Ila pamoja na kutokujua kwake mambo ya kawaida bado ulimpigia kura halafu unamhoji Rungwe?
Nyani haoni k......le.
Kila mtu ana level yake ya ignorance, lakini isizidi. Hebu angalia maelezo ya huyu jamaa halafu ujiulize alikuwa anazungumzia nini. Kama ni darasa, can you get the topic? Ni mtu tu aliyejaliwa kukosa aibu.
 
Mbona sawo tu hata wengine hawajui kuwa kuna nchi huko duniani zinawajengea nyumba wananchi wao wanapofikwa na majanga ya tabianchi
Unajua tofauti ya tabianchi na tetemeko? Unajua kwamba kuna mfuko wa dunia wa mambo ya tabianchi lakini hakuna mfuko wa tetemeko. Au unadhani tetemeko pia ni mambo ya tabianchi?
 
Mimi namjibu kwa haraka na urahisi kabisa kwamba yote aliyoyataja ambayo ni mambo mazuri kabisa kufanywa na Serikali ya CCM, yamefanyika kwa kipindi cha miaka 10 pamoja na Awamu nyingine zilizopita yaani II na ya III, hivyo kutegemea kwamba ndani ya Mwaka I Awamu ya V ifanye mengi zaidi ya Awamu tatu zilizopita ni ujinga na kwanza hakuna mashindano kwani wote ni Viongozi wa CCM na wanatekeleza Ilani za CCM!

Ila nimefurahia kwamba Upinzani wamekubali kwamba CCM imefanya makubwa Tanzania kinyume na wengine ambao husema kwamba miaka 50 hakuna kilichofanyika, hivyo nimefurahi kwamba mme bow down kwamba Nchi yetu inasonga mbele tena kwa kasi ya ajabu kama Mpinzani alivyosema!

Huwezi kumuelewa Rungwe kwa akiri ya kawaida atukatai swali la Msingi kutwambia nchi imepinda je imepinda wapi CCM ajafanya kitu sema kodi za wananchi ndo zimefanya hivo
 
"Inchi imepinda" hiyo ndio kauli ya JPM imepindia wapi hakuna anayejua, na ukumbuke anasema anainyoosha nchi kwanza na matamshi na kauli zake anamaanisha hakuna Kilichofanyika bali yeye ndio anataka kufanya sasa, Rungwe anahoji nchi imepindia wapi mbona kuna a, b, c mtangulizi wako kafanya kwa nini usiendelee hapo kwa kasi kwenda mbele??
Walichoshindwa CCM ni kuongoza toka 1961 na kushindwa kuitoa Tanzania kwenye kundi la nchi masikini sana..

Mwishoni kasema akuna kitu kibaya kuendesha nchi kwa visasi na chuki
 
"Mfano baadhi ya Maeneo yaliyokuwa yamepinda ni pamoja na mfumo wa uchaguzi na usimamizi wake. Mfumo mbovu wa uchaguzi umekuwa ukitunyima viongozi bora wa kuwakilisha wananchi hasa wabunge.
Ukiwa na wabunge wabovu huwezi kuwategemea watunge sheria nzuri zaidi ya kupiga makofi na kutetea matumbo yao. Huku ndipo pa kunyoosha.

Sehemu nyingine iliyopinda ni demokrasia. Demokrasia yetu imepinda ndio maana chaguzi zinatawaliwa na rushwa na wizi wa kura hatimaye tunapata viongozi wezi.

Kutotii sheria na kanuni za nchi kwa watumishi na kwa raia nalo pia ni kati ya mambo yaliyopinda.

Riba kubwa kwenye mabenki nayo ni kati ya mambo yaliyoponda na yanahitaji kunyooshwa.
Migogoro ya ardhi kule Loliondo na kule Morogoro ni kati ya mambo yaliyopinda.
Wanafunzi wa chuo kukosa mikopo ni kupinda huko.
Misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini ni chanzo kikuu cha wakwepa kodi kujinufaisha kupitia humo na kuipindisha nchi.
Haya mapindo yote yanahitaji kutungwa kwa sheria na katiba inayozuia hayo na sio kutegemea kikundi cha watu wanaotumia mara nyingine jazba na chuki bila kuwepo kwa sheria. Mfano ni lazima pawe na sheria ya kusajili mali za watanzania wote ili tujue nani hastahili kuitwa maskini na nani anamiliki nini na alizipataje?"

Swali la Hashim Rungwe ni " Je,nchi imepinda wapi na kuelekea upande gani?[/QUOTE]..

sijui wamekuelewa...
 
Unajua tofauti ya tabianchi na tetemeko? Unajua kwamba kuna mfuko wa dunia wa mambo ya tabianchi lakini hakuna mfuko wa tetemeko. Au unadhani tetemeko pia ni mambo ya tabianchi?
Umejitahidi kama kawaida yako KUMBE tetemeko halihusiani na tabia nchi nawewe kwa kuremba hujambo
 
CHUKI NA UBAGUZI..
laana hii.

Mpaka 2020 jambo pekee ambalo atakuwa amelifanya ni kutumbua tu kasahau mambo ya msingi ona sasa nchi haina hata akiba ya chakula hii ni aibu kwako mtukufu.
 
Back
Top Bottom