Hashim Rungwe, akosoa kauli za Rais Magufuli

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,481

Mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMA Hashim Rungwe amesema kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya Mahakama nchini iliingilia uhuru wa mahakama.

Akielezea utata uliojitokeza katika hotuba hiyo Rungwe amesema hotuba hiyo ilionekana kama kuifundisha mahakama wajibu wake jambo ambalo lina utata katika uongozi wa kisheria lakini hata hivyo Rungwe ameielezea hotuba hiyo kuwa itaongeza uwajibikaji katika mahakama na haki kupatikana kwa wakati.

Wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama Alhamisi iliyopita, Rais Magufuli aliahidi kuipatia idara ya mahakama fedha kwa ajili ya kuendesha shuhguli za mahakama na kuitaka mahakama hiyo kuharakisha kusikiliza kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kesi za watuhumiwa wa kukwepa kulipa kodi.


 
Muda mwingine gari la kuzimika zimika ina bidi lisukumwe ndio liwake,kesi nyingine mtoto amezaliwa mpaka ana karibia kumaliza shule ya msingi zipo tu,je tuna furahi kusikia mahabusu wamejipaka haja na kujilaza barabarani kudai haki zao baada ya kupigwa tarehe kila kesho? Nadhani ana stahili kupongezwa kwenye hili zaidi ya kulaumiwa.
 
Muda mwingine gari la kuzimika zimika ina bidi lisukumwe ndio liwake,kesi nyingine mtoto amezaliwa mpaka ana karibia kumaliza shule ya msingi zipo tu,je tuna furahi kusikia mahabusu wamejipaka haja na kujilaza barabarani kudai haki zao baada ya kupigwa tarehe kila kesho? Nadhani ana stahili kupongezwa kwenye hili zaidi ya kulaumiwa.

Mbona hawasemi gharama alizozisema Rais kuwatunza mahabusu 1.8bilioni kwa mwezi, kama wangepunguza kesi hata serikali ingekuwa na mzigo mdogo na kuzisaidia kutatua matatizo ya mahakama.

Kwa kifupi JPM alikuwa anajaribu kuwapa elimu kuwa kila taasisi ikitimiza wajibu wake itasaidia kukuza uchumi wa nchi. Mahakama inaomba bilioni 40 kwa shughuri mbalimbali huku inachelewesha hukumu hivyo kuongezea serikali mzigo kuwalisha wafungwa.
 
Hawa wazee sio wa kupuuzwa.... Wana akili sana Yusufuuuuuuuuuuuu puuuuuuliza kibatari....
 
"Hashim Rungwe Spunda kura 11"- Kila nikisikia jina na huyu kamanda nasikia echo ya sauti ya prominent Jaji Lubuva
 
Back
Top Bottom