Hasara za kutumika

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,976
Reaction score
828,710
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza kuchukua hatua za kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika maeneo yasiyo rasmi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, wakati wa ufunguzi wa Soko Kuu la Kariakoo.

Akizungumza katika hafla hiyo, RC alisema kuwa ingawa hatua hiyo inaweza kuonekana kuwa ngumu au chungu kwa baadhi ya wafanyabiashara, ni muhimu kulinda mpangilio wa jiji na kuhakikisha barabara zinabaki wazi. Alisisitiza kuwa utekelezaji wake utaendelea kufanywa kwa kutumia diplomasia na maelewano, badala ya nguvu.
 
Swala la mpangilio wa mji walipaswa kuanza na good urban planning ... Hizi ni athari zinazojitokeza kutokana na mpangilio mibovu ya miji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…