Jana 9-10-2017, katika kipindi cha “This Week in Perspective” – TBC – kinachoendeshwa na Adamu Simbeye, waliongelea kuhusu
Vitabu Vibovu vilivyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE).
Kati ya mambo yaliyonigusa ni gharama iliyotumika kuandaa vitabu hivyo vibovu.
Profesa Galabawa wa UDSM alisema kuwa, TIE wametumia:
ZAIDI YA BILIONI 144 😱😱😱😱😱
kuandaa vitabu hivyo ambavyo sasa havina thamani yoyote kuweza kutumika shuleni. Inabidi, ama vitupwe au kuchomwa moto.
Waziri Mkuu wetu alipoulizwa bungeni juu ya nini kinafuata, alisema:
- vitabu hivyo vinaondolewa shuleni,
- TIE wanaajiri wafanyakazi wapya wenye utaalamu,
- makosa ya vitabu yatarekebishwa.
🙁🙁🙁🙁
Kwa nini serikali inataka kurudia makosa yaleyale?
Acheni sekta binafsi ifanye kazi hiyo.
Serikali iwe SERIOUS kwenye kusimamia viwango.
Sekta binafsi ikishaandika vitabu, serikali ndiyo iwe na usemi wa mwisho kusema, “Kitabu hiki kizuri, tutakitumia. Hiki ni kibaya hatukitaki.”