Harusi yangu iliniachia chuki kwa wanawake

Harusi yangu iliniachia chuki kwa wanawake

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
^^
"..Kila nikikumbuka siku yenyewe basi namwona mwanamke si kiumbe wa kuaminika,ni mwongo,msiri wa kijinga na anaweza kukuua wakati wowote.
...
Alikuwa ni binti mzuri tu ambaye kila mwanaume angeweza kumsindikiza kwa macho,huku akikitazama kiuno chake cha mviringo na umbo la wastani rangi ya sanaa,na mengi tu ya kuvutia.
...
Nakumbuka mwaka ule ndo nilikuwa likizo ya kwanza tu tangu nilipoanza kazi yangu ya ualimu.Na nilikuwa nimerudi kwetu ili pamoja na mambo mengine nitafute mchumba ili tusaidiane ktk maisha.
...
Kweli nilimpenda mwanamke huyu na nilimweleza nia yangu kwake ya ndoa na akanikubali.Alikuwa akiishi kwa shangazi yake,,kwa kuwa kilikuwa kijiji kimoja wengi walimweka katika orodha ya wasichana watakatifu wasio na kashifa yaani mwenendo mzuri,,basi taratibu zote za uchumba na uchunguzi zilianza huku mimi nikirejea kazini mkoa mwingine.
...
Kwa wengi watakumbuka jinsi mawasiliano yalivyokuwa magumu miaka ya 1994,,tulitegemea barua.Na kwa kuwa zamani suala la kuchunguza familia lilipewa kipaumbele kazi ilikamilika na taratibu za ndoa zilianza.Tulipewa mafundisho yote kwa mujibu wa kanisa katoliki na siku ya harusi ilifika.
...
Ikumbukwe ktk maisha yangu sikuwahi kumjua mwanamke kimapenzi,,lakini siku ya harusi/ndoa bibi harusi,,alipata kichefuchefu akatapika,alisaidiwa nami nikaona jambo la kawaida,sherehe ikaendelea.
...
Ilifika usiku,nakumbuka ni usiku wa saa 5 hivi,nikiwa na hamu na bibi harusi wangu,,lakini alianza kutapika tena na tena.Nikaita watu wanisaidie na muda wa usiku huo alipelekwa hospitali na akapimwa kumbe alikuwa na mimba ya mwezi mmoja!!
...
Niliumia sana! Tena sana! Sikutaka mapenzi nae,,nilipomhoji sana alikiri kuwa mimba ni ya mume wa shangazi yake,,alipokuwa anaishi !! Sio siri nilivunja ndoa,nikamrudisha kwao! Nikarudi kazini kwangu mtupu..."
Ndio maana mpaka leo siwapendi wanawake wanafichiana siri na niliamua kutooa kwani nilikula kiapo cha ndoa,,ndoa ambayo ilinigeuka..."
...
HII NI SIMULIZI YA KWELI AMBAYO NIMESIMULIWA NA MZEE AMBAYE NI RAFIKI MKUBWA KWANGU.
CC. Kaunga
^^
 
Last edited by a moderator:
Daah!!!!! Mi nilifikiri itaendelea, nimeipenda sana hiyo story

btw, hiyo rangi ya sanaa ndio rangi gani Himidini?
 
Last edited by a moderator:
Daah!!!!! Mi nilifikiri itaendelea, nimeipenda sana hiyo story

btw, hiyo rangi ya sanaa ndio rangi gani Himidini?

^^
Ungemsikiliza mzee huyu wakati anasimulia kisa hiki,juu ya uzuri wa yule bi harusi wake,,hakika ungetumia neno hilo btw,mzima best
How is Arushaone umepata msaidizi wa kazi?
^^
 
Last edited by a moderator:
^^
Ungemsikiliza mzee huyu wakati anasimulia kisa hiki,juu ya uzuri wa yule bi harusi wake,,hakika ungetumia neno hilo btw,mzima best
How is Arushaone umepata msaidizi wa kazi?
^^

Kumbe sio story yako
 
Back
Top Bottom