Harusi yageuka Msiba Taifa,Simba yapigwa thalatha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harusi yageuka Msiba Taifa,Simba yapigwa thalatha

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Aug 8, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huu tuuite mwaka wa shetani kwa Simba ama tutumie lugha gani kuuelezea?
  Team ya soka ya Simba leo imewasononesha tena mashabiki wake baada ya kukubali kichapo cha bao 3-1 kutoka kwa team ya Nairobi City Stars katika mchezo uliokuwa wa kukamilisha sherehe za Simba Day.
  Simba ambayo ilianza kwa kuteremsha kikosi cha kwanza,wenyewe wanaita kikosi cha maangamizi (angalia list hapa chini) ilishuhudiwa ikipoteza dira kipindi cha 2 na kukubali kipigo hicho kilichotibua kabisa shamrashamra zao.

  [​IMG]

  Kwa habari zaidi soma hapa BIN ZUBEIRY
   

  Attached Files:

  • List.jpg
   List.jpg
   File size:
   111.8 KB
   Views:
   226
 2. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tuzo ya heshima waliyoitoa kwa Marehemu Mafisango katika Simba Day leo na kupokelewa na Kaburu, tunaomba itakapokwenda kukabidhiwa kwa familia ya Marehemu(kama itakabidhiwa) ikakabidhiwe na rambirambi zake.
   
 3. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Haikuhusu.


  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 4. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Inanihusu sana,nyie ni wawakilishi wetu katika mashindano ya kimataifa msipo'clear hilo tatizo mtazidi kushusha rank yetu katika Fifa,kila siku 3-1...na team iliyo vizuri 3-1 na team iliyookotezwaokotezwa tu 3-1...aah mambo gani hayo??
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Hawana timu hao.
   
 6. M

  Masuke JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Subirini mashindano ya ligi yaanze ndo mtajua tuna timu au hatuna.
   
 7. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kitu kimoja ambacho Simba wameanza kukifanya na kinanifurahisha ni kuanza kuwapa nafasi wachezaji wa akiba ambao hapo nyuma walikuwa hawapati nafasi kabisaa ya kucheza,nafikiri kupoteza wachezaji wazuri kama Makipa Dida na Barthez kumewapa funzo tosha siku hizi hata kipa wa akiba anapata nafasi ya kucheza katika mechi isiyo na umuhimu sana tofauti na hapo zamani ambapo kila mechi ilikuwa Kaseja,iwe ya ligi,iwe ya kirafiki dhidi ya team ngumu,iwe ya kirafiki dhidi ya Kombania ya shule za secondary zote Kaseja golini,Kaseja-Kaseja,kila mechi Kaseja ilikuwa ni kuua vipaji vya Vijana.
  Halafu na hao akina Hamad Waziri wanapopata nafasi ya kucheza wawe wanakaza vinginevyo wataishia kuwa wachezaji wa kudumu kwenye yale mabenchi ya Uwanjani.
   
 8. M

  Masuke JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Halafu kuna wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza hawakucheza ile mechi ambao ni Kapombe(15), Okwi(25), Twite(4) na Musa Mude(5); kwenye mabano ni namba ya jezi watakazovaa msimu ujao.
   
 9. C

  CAY JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakuna timu hapo,watu nanakua tu!
   
 10. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  kwani ulikuwa unafikiri ni simba wa porini kweli? ni kapaka tu tena kadogo sana hafu mbaya zaidi kana njaa kupitiliza!!
   
 11. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Yah ni kweli,lkn ninavyoona mimi Kocha alikuwa na sababu ya kutowachezesha,Kapombe yeye ameachwa asaidie kuwabeba ile Under 20 yenu kwenye michuano ya ABC,wakati Okwi aliachwa apumzike baada ya misafari yake,Twite bado kizungumkuti na Mussa Mudde bado yuko Uganda anatibu majeruhi yake aliyoyapata kwenye Kagame.
   
 12. M

  Masuke JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Kizungumkuti cha Twite kinatoka wapi? Au kwa sababu mtoto wa mheshimiwa analeta umaarufu wa baba yake kuwatisha viongozi wa Shirikisho la Soka la Rwanda anadhani baba yake anainfluence hadi Rwanda, mwambieni aimarishe cha kwake bila kuharibu cha mwenzake, mbona PSPF wamejenga ghorofa zuri tu pale Ohio bila kuvunja la PPF na la kwao sasa linaonekana zuri kuliko la PPF, wachezaji wako wengi tu hakuna haja ya kumfuata mchezaji ambaye anataarifa kwamba timu nyingine imemsainisha na yeye anaenda kwa kutumia umaarufu wa mzee wake, mnaweza tumia wachezaji wengine na timu yenu ikatisha kuliko yetu bila hata kuchukua mchezaji mmoja toka kwetu.
   
 13. C

  Chipolopolo JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kasimba kenye njaa eti?Chakula yake huwa Yanga fundo 5-0!
   
Loading...