Harusi/sendoff sio dharula!!

usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
500
Katika tembea zako za kutafuta mjini unakutana na mtu mnayefahamiana. Mara ghafla anakuambia 'afadhali nimekutana na wewe nikupe na kadi ya mchango". Ukiangalia mchango umewekewa na kiwango na bado wiki mbili. Sasa huwa najiuliza, hivi unavyopanga kuoa/kuolewa hukujipanga mpaka kuwashtukiza watu? Kwani lazima uonekane umefanya sherehe? Hivi nani aliwaambia watu tunakaa na hela standby kawa ajili ya michango yenu ya harusi/sendoff? Hii sio misiba au ugônjwa ambao hutokea ghafla hivyo hulazimisha watu kujipiga piga kwa chochote kile kilichopo. Kupenda maonesho kusifanye tukaanza kuwasumbua wengine, watu wana majukumu yao na malengo na hela zao.!
 
Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,152
2,000
Kiongozi kama wewe umechukua kimya kimya wacha wenzio wachukue formal...na ukiombwa mchango kama huna usione aibu ama utoe kisha uje kunung'unika,wee mwambie mwombaji hapo hapo kwamba mipango imeingiliana ama huko sawa...
 
Kuchukua formal ndio kuweka sherehe usiyokuwa na uwezo nayo! Sikujua hilo! Kwani kwenda kanisani mkiwa na ndugu wachache mkamaliza kila kitu sio harusi? Duh, huu utaratibu umetufanya tumekuwa kama hatujielewi vile. Mtu akikwambia kabanwa unaona kama anataka usioe/kuolewa. Jamani tujipange kabla ili tusisumbue wengine ambao wala hawahusiki na familia tunayoenda kuijenga! We unawachomoa watu pesa nyingi aafu baada ya wiki tatu unafumaniwa nje ya ndoa na inavunjika!
 
Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
8,876

  • Hili ni tatizo, ni kweli tunapaswa kubadilika
  • Kuna harusi hivi karibuni imefanyika hapa mtaani - bajeti ilifika milioni 42 (Kwa wengine hiki ni kiasi kidogo sana, ila kwa mtanzania wa kawaida ni palefu sana)
 
Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,152
2,000
Kuchukua formal ndio kuweka sherehe usiyokuwa na uwezo nayo! Sikujua hilo! Kwani kwenda kanisani mkiwa na ndugu wachache mkamaliza kila kitu sio harusi? Duh, huu utaratibu umetufanya tumekuwa kama hatujielewi vile. Mtu akikwambia kabanwa unaona kama anataka usioe/kuolewa. Jamani tujipange kabla ili tusisumbue wengine ambao wala hawahusiki na familia tunayoenda kuijenga! We unawachomoa watu pesa nyingi aafu baada ya wiki tatu unafumaniwa nje ya ndoa na inavunjika!

Ha ha haa...mimi nikitoa hela yangu huwa naweka angalizo kabisa,endapo ndoa itavunjika kwa kipindi cha chini ya miaka mitano kuanzia ifungwe basi maharusi watalazimika kunirudishia mchango wangu niliotoa siku ya Harusi yao...kama watajali sana wakate sahani ya biriani na hito tubia tuwili nilivyoshiriki siku hiyo ova...
 
tall gal

Senior Member
Oct 24, 2013
102
0
Ukiona kakupea kadi barabarani ujue hata hakuplan kukualika....ni bas tu mmekutana anajshaua kukupa ili usimlaum utapoyaskia kwa watu.........wadada ndo wapenz wa complications kwenye sherehe zao
 
Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,205
2,000
Kiongozi kama wewe umechukua kimya kimya wacha wenzio wachukue formal...na ukiombwa mchango kama huna usione aibu ama utoe kisha uje kunung'unika,wee mwambie mwombaji hapo hapo kwamba mipango imeingiliana ama huko sawa...

1. Kuchukua 'formal' haina uhusiano na kuchangisha watu
2. wengine ving'ang'anizi, mchango anageuza kama ni haki yake,yaani kama deni, wanakera sana, mnaooa au kuolewa, jipangeni!
 
Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
15,723
2,000
Na msipopewa kadi mnalalamika!! Ila mimi kuchangia harusi itakua ngumu kidogo,sijui kama nitakua nachangia harusi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom