Katika tembea zako za kutafuta mjini unakutana na mtu mnayefahamiana. Mara ghafla anakuambia 'afadhali nimekutana na wewe nikupe na kadi ya mchango". Ukiangalia mchango umewekewa na kiwango na bado wiki mbili. Sasa huwa najiuliza, hivi unavyopanga kuoa/kuolewa hukujipanga mpaka kuwashtukiza watu? Kwani lazima uonekane umefanya sherehe? Hivi nani aliwaambia watu tunakaa na hela standby kawa ajili ya michango yenu ya harusi/sendoff? Hii sio misiba au ugônjwa ambao hutokea ghafla hivyo hulazimisha watu kujipiga piga kwa chochote kile kilichopo. Kupenda maonesho kusifanye tukaanza kuwasumbua wengine, watu wana majukumu yao na malengo na hela zao.!