Harry Belafonte na Hamza Aziz

Tanzania tumetafuta uhuru na ukombozi wa nusu ya Afrika, kivita na kidiplomasia, singlehandedly, hakuna mwanamuziki na mcheza filamu aliyetusaidia.
Wakati tunapigania uhuru wetu, hao kina Belafonte kwao kila kona vibao "For whites only". Hata kwenye mabasi walirundikwa nyuma kama mifugo, wangetusaidia vipi wakati wao wenyewe wakipigania haki zao huko kwao!

Wafundisheni historia hawa vijana wasiojua tupo hapa tukitokea wapi.
 
Asante Mzee!
Mimi nadhani huyo mwamba anapenda kujifunza ila kupitia kukosoa. Ndiyo walikuwa wasanii,vp km ilikuwa ni namna ya kukwepa vikwazo?
 
Asante sana.
Ninaendelea kula ukoko hapa.

Mimi sipendi udini wala ukabila.
Mzee,swali la jamaa kuhusu sisi kutopiga kura mbona liko wazi kwa majibu.

Urusi anajitetea na kujilinda km ambavyo Palestine ingeweza kufanya dhidi ya Israel na washirika wake.
Sema kwakuwa Urusi ana nguvu kumzidi Ukraine ndo maana tafasiri za wengi wetu ni kwamba Urusi ni muonevu.

Km ilivyo kwa Palestine,Marekani ananufaika sana pale Israel na ndo maana anaogopa kumkemea na ndiye mshangiliaji mkuu wa Israel.
Kwa sababu za udini tulio wengi tunaamini Palestine anastahili kuonewa na Israel lkn kiuhalisia msimamo wetu dhidi ya mgogoro huu ilibidi uendelee kuwa km awali.

Mabadiliko ya msimamo huenda ikawa ni msukumo ktk UK,US na misaada tuipatayo kutoka kwa hawa wahuni. Urusi ni mtu wetu wa karibu sana sisi Africans kwa mjibu wa history na ndiyo maana tumekuwa kati kuhusu kura juu ya mgogoro wa Ukraine. Pamoja na ukrisito wa kizungu niliopewa lkn nasimama na PALESTINE,wanaonewa sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…