Harrier vs forester subaru

Shukrani kwa maelezo mazuri
 
Ukifuata sana ushauri wa JF unaweza jikuta unajuta, kuna kipindi niliwahi kuomba wanishauri gari ndogo ya kununua, zaidi ya 70% ya wadau walishauri ninunue CARINA TI ingawa kwa upande wangu nauona hilo gari ni mkweche wa kizamani, ingawa niliomba ushauri mwenyewe ila sikuufata kwakweli. Kwa JF gari gumu kinalovumilia njia mbovu ndio bora. Kuhusu hii thread mi mwenyewe nilishangaa hivi unawezaje kusema Subaru ni gari bora zaidi ya Harrier?
 
Acheni kulinganisha Subaru na vitu visivyoweza kushindana nayo, Subaru ni Symmetrical All Wheel Drive(AWD) inayotoa power independent kwa matairi itategemea lipi linahitaji nguvu ndo linapewa, ukiwa rough road ndo utapenda zaidi maana Forester imekua designed for rough road zaidi na kadri inavyozidi kukimbia inakua more stable inatitia flani hivi, ukitaka flexibility na comfortability barabarani basi Subaru ndo nyumbani, hizi gari ni za miendo huwezi linganisha na gari za starehe na advantage ua Subaru ni kua hakuna vifaa fake km gari nyingi za Toyota maana zinaingilia sana
 
Mhhh sijui sn magari bt Harrier is on a whole new level, level zake ni SUV, Subaru naona ni sedan, enewei mtu km mie mwonekano wa gari matters the most performance mara sijui spidi vya kazi gani Dar kwnyw foleni kila mahali
 

Gari bora kwako ni lipi, ongea kwa facts kidogo. Au kwako gari bora ni ile unayoiona sana? Kama unavyoshangaa watu kusema subaru ni bora kuliko harrier ndivyo nami navyoshangaa jinsi usivyoielewa subaru, hasa ukiongea bila facts. Watu washaeleza humu kwa nini wanasema Subaru ni bora zaidi. AWD, POWER, stability, durability. Mnaoongea kwa kejeli kuwa unafanishaje harrier na subaru mngesema kwa nini harrier bora
 
Huyo hajui na hataki kujua Subaru.

Hujaweka SAFETY. Subaru Forester ina highest safety rating from crash tests kuliko gari jingine lolote in its class kwasababu ya boxer engine kuwa chini hivyo kutobinya occupants wa gari kwenye ajali.
 
Kama una katabia ka kuonja kilevi na kuendesha gari usinunue hiyo gari, pulling yake ni ya hatari.
Sinywi na sijawahi kunywa na situmii chohote kill
Hata kuvuta sivuti

Experienced ila sio kwenye rally a sijawahi shiriki yoyote
 
Sinywi na sijawahi kunywa na situmii chohote kill
Hata kuvuta sivuti

Experienced ila sio kwenye rally a sijawahi shiriki yoyote

Basi Utaipenda. Niliwahi kuendesha Forester ya 2004 cc2500,manual turbo. Nzuri ila ni kwa wanaopenda nguvu nyingi kwenye gari. Vinginevyo Subaru ya CC 2000 bado inatosha sana na ni economical zaidi
 
Hapo umeongea kweli ndugu yangu, mimi nawajua mafundi wachache sana wa Subaru hapa dar, na huwa wanajua kutambua ugonjwa wa gari hata kabla haijaanza kukupa wenye, akisema upeleke gereji usibishe
 
Subaru kwa mauzo ndio pake ila ue na pesa ya kutosha na usiwe na gari moja
 
Kila mtu na mapenzi yake mm Brevis aka Benz ya Kijapan hunitoi hata kwa masafa kusafiri mbali Subaru itangoja sana

Ni kweli kika mtu ana mapenzi yake. Brevis ndio gari natumia mara kwa mara. Ni nzuri, comfortable na ina nguvu ila inakula mafuta zaidi na sio ngumu kama subie
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…