Harrier vs forester subaru

RO7 ZA MGOS

JF-Expert Member
Sep 27, 2016
1,952
5,552
niajee mazee gari gan hapaa naweza kununua hizo ni choice zangu nilishawahi ku drive forester mwaza la msela bonge la chuma xoo talanta niweke wap mafuta na capability n muhim kwa watalam uwanjaa huu hapa jitupeni
 
Ok but una additional details za subaru ina kitu gan cha kipekee sjawahi kuendesha harrier
 
Nina miliki Subaru Forester manual transmission tangu mwaka 2010 hadi sasa.Hizi gari ni imara sana haziharibiki hovyo hovyo ila ikiharibika jiandae spear zake ziko juu sana mfano shock up yake moja ni Tsh.250,000.Na kwa sababu ni AWD mafuta inakula zaidi ya non AWD.Hazikwami kwenye michanga,tope nk.Zinakimbia sana pia.Harrier sijawahi kuitumia.Spare za Subaru haziingiliani na Toyota!Hata Rim lazima utafute ya Subaru!
 
Subaru...ni gari za ujanani na ni potable kwa njia zote rough na kawaida...harrier aaagghh naona ipo ki mayai sana...kwa upande wangu Subaru ni gari poa na ina himili mikiki mikiki kuliko harrier kuhusu kula mafuta zote zinakula inategemea matumizi yako tuu
 
Watu wengi wanaweza wasizielewe subaru kirahisi, ila ni gari imara na ina perfomance nzuri. Inaweza isiwe nzuri sana kiuchumi lakini hata harrier si nzuri kiuchumi, inakula mafuta pengine hata zaidi. Personally ninhechukua subaru wakati wowote
 
Kwa upande wangu ningekushauri subaru kwasbabu zifuatazo:-
1) subaru iko stable sana ukilinganisha na harrier.Harrier inajitahidi kukimbia ila dakika moja uko chini
2) spare za subaru ni gharama kiasi ila ni genuine ukifunga unasahau
3) subaru ni imara kuliko harrier
4) body yake haichoki haraka kama ya harrier
.
 
Hapa sisi wenye akili zetu tunakosa cha kuchangia.utapata mawazo toka kwa watu wa aina yako.nlikuwa nmejiandaa kuja kutoa uzoefu wangu nimekuja kusoma thread yako imejaa ubashite mwingi. Ninyi ndo mnasababisha walimu patwe na hasira kwenye kufundisha.
 
Hapa sisi wenye akili zetu tunakosa cha kuchangia.utapata mawazo toka kwa watu wa aina yako.nlikuwa nmejiandaa kuja kutoa uzoefu wangu nimekuja kusoma thread yako imejaa ubashite mwingi. Ninyi ndo mnasababisha walimu patwe na hasira kwenye kufundisha.
Tupe uzoefu wako hivyohivyo hata kama kuna aliyeharibu katika kuchangia
 
  • Thanks
Reactions: kas
Kaka kuilinganisha subaru na harrier ni kuikosea heshima subaru,, subaru ni subaru tu hebu tutake radhi sisi wazee wa subaru lakini ni kwasababu umesema umeendesha subaru kidogo tu ulivyokuwa mwanza kwa hiyo bado hujaijua vizuri. Gari ina speed sana ile halafu iko stable, kingine haichagui barabara hlf haina tofauti kwenye tambarare wala mlima speed ni ile ile. Halafu ni all weather road yaani kwa kifupi ni gari yenye power sana. Mimi namiliki subaru forester ya 2004 ni gari nzuri sana halafu ni nyepesi kuchanganya kwa sababu nikiondoka kwa kasi inanichukua sekunde 8 tu mshale wa speed kutoka 0 to 100. Na kuhusu mafuta ni utumiaji wako wewe mwenyewe kwa sababu nikiamua kukimbia sana huwa kweli linanipiga mafuta lakini nikiliendesha kistaarabu wala halinipigi. Kwenye spea zake ndo kuna gharama kidogo na ni kwa sababu spea zake ni genuine ukifunga utasahau. Lakini kwa ushauri wangu subaru ni gari zuri sana na halina magonjwa yakijinga kijinga na ikitokea limepata tatizo muone fundi anayejua subaru kwani ukipeleka tu kwa fundi mradi ni fundi utajuta kitakachokupata
 
Mimi nimeendesha Harrier mpaka sasa ila hili gari halijanivutia ikija kwenye stability despite ni gari zuri ingawa Subaru Forester litakuwa zuri zaidi kwenye stability sababu ni AWD na boxer engine
Ni harrier model gani? vipi comfortability yake na fuel consumption?
 
Umewahi kuona mtu mwenye pesa zake ananunua Subaru!? Tuanzie hapo kwanza.

Wenye Subaru na Alteza wengi ni hawa hawa vijana wamepata vihela vya spea za Harrier (new model) na Rav 4 (new model) kama milion 8 hivi ndio wanaagiza Subaru.

Yani nimeshangaa kuona muanzisha uzi anafananisha gari ambazo bei zao moja ni mara karibu tano ya nyingine halafu anataka wachangiaji tumpe maoni yetu! Hatupo serious jamani
 
Ni harrier model gani? vipi comfortability yake na fuel consumption?
Mimi pia nimeendesha Harrier ya 2006 cc 2490. Kuhusu mafuta inakunywa na kuhusu comforability inategemea upo kwenye mwendo gani. Ikiwa unaendesha speed za 100km/h + utaanza kuona kama inaelea hivi barabarani na inakuwa laini hali ambayo inakupa hamasa ya kukanyaga mafuta tu. Yani inakuwa kama ndege ya ardhini.

Ingawa niliuza Harrier yangu na sasa napush Rav4 ya 2008. Hata hivyo ninapendekeza mtu kama ana uwezo nalo Harrier new model ni gari zuri sana.
 
Back
Top Bottom