Harmonize na Jide, balaa na nusu

astalavista

Senior Member
Jul 7, 2014
156
159
HARMONIZE NA JIDE, BALAA NA NUSU

Nilisikiliza kwa mara ya kwanza, nikasikiliza tena halafu nikasikiliza tena na bado naendelea kusikiliza. Napata burudani kusikiliza mashairi bora kabisa kutoka kwa chinga mmoja hivi aliyezaliwa Chitoholi kule Tandahimba, nasisimka zaidi nikiisikia sauti ya Mbibo halisi, mwanadada komando mwenye vyeo vyake kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Tanzania. Nitake nini tena kwenye mtima wangu kwa upande wa burudani, ipo raha kuwasikia.

harmonize_tz_20200315_1.jpg
Kule dada wa Kikurya toka Mara huku Konde boy chinga toka Mtwara, wameleta balaa jipya mjini 'Wife' bonge moja la wimbo niamini nachokuambia. Kama ulikuwa miongoni mwa watu wachache wasiofahamu mziki kusema eti Jide zama zimepita basi tafuta wimbo wa Wife halafu utajisahihishia mwenyewe.

Mwanadada Komando kama anavyofahamika kwa mashabiki zake ni kama amemkanya Harmonize kwamba mwana ukome, amemkomesha kwa sauti yake maridhawa na bila shaka akiwa studio alikuwa anajisema kwa kikurya 'let me show you' Mshamba mmoja wa Tandahimba. Sikiliza wewe Wife ni balaa na nusu nenda kaitafute halafu urudi hapa unibishe.

Watu wangu ambao hamjaoa sauti inatosha? Basi mwanetu Rajabu yule muuza kahawa wa zamani mitaa ya kariakoo ametuletea dude linatuhusu kabisa. Kwanza ametusanua yeye amechoka kuwa bachela, vipi yupo sawa au anasaliti kambi? Achana na hayo mambo kikubwa twende tukasikie midundo hatari, mashairi yaliyopangwa vema na sauti ya malkia wa muziki bongo Komando Jide.

Huyu Harmonize ameamua, kijana wa kimakonde amechagua kuwa somo kwa vijana wengi nchini, kila siku anatoa somo kwetu sina hakika kama vijana tumegundua kitu gani anahitaji tuchukue kwake. Ni uthubutu na kuweka nia ya dhati, Harmonize ametu'prove wrong' kwamba yapo maisha mengine baadae.

Vipi unapenda mziki mzuri? Usipoteze muda sasa fanya hima kawasikilize hawa wenye mziki wao. Harmo anamwimbia Jide, Jide naye anamjibu kwa mikogo na maringo. Hauchoshi kuusikiliza,ni balaa na nusu nishasema hapo juu.

Sikia sasa kumbe yule Komando wa Kikurya hana lolote kwa Chinga wa kilimani kule Mahuta, mwenyewe amekiri yeye ni Maji tu kwa Harmonize halafu mshikaji ni kama Chura yaani anayaoga anavyotaka. Nani ana namba ya yule Mnaijeria wa dada Judith atuambie alikwama wapi.

Balaa lipo kwa Harmo nawaambia, Chinga hata hakujali umri wala ukongwe wa Jide kwenye gemu ikasikika sauti toka kwake akimwambia wakipata watakula, wakikosa watalala. Unatamani kujua alijibiwa nini? Nenda kaisikilize nakuambia mara ya mwisho. Sema nilichogundua Jide siyo slay queen wala nini.

Eti zimewashuka sura waliojichosha na makafara, mmakonde ana mambo huyu! Inaweza isithibitishwe popote lakini huu wimbo wa Wife umerudisha tabasamu kwa mashabiki wa Simba baada ya kipigo cha Yanga, sio ajabu wala nini baada ya kusikiliza wimbo huu Antonio Nugaz ukimwita Utoporo atafurahi huku akichagiza wape salaaaaam mabachela wote.

TeAmo!!
 
Niliangalia mwanzo mwisho. Ilikuwa well prepared and presented. High profile attendance ikianzishwa na former Presidaa, Spika, mawaziri, mastaa ndani na nje ya nchi. Ukweli kijana ameanza vizuri sana. Cha kufurahisha yuko well behaved, heshima zote na ndoa kabisa. Ukilinganisha na mchungulia nyuchi Mkuu anayetamani kijana ashindwe kusonga mbele.
 
Jide mwenyewe hataki ngoma zake zipigwe..

muda mwingine tunawapa lawama nyingi Clouds ambazo nyingine sio zao
Hayo ni maelezo ya mawingu mbele ya camera waonekane wako peace hawana Shari na jide...

Nyuma ya pazia wanamuwekea conditions Kali kama akitaka kurudi kwao ..hapo ndipo anaconda anafeli kunyenyekea wachumia tumbo kama yeye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HARMONIZE NA JIDE, BALAA NA NUSU

Nilisikiliza kwa mara ya kwanza, nikasikiliza tena halafu nikasikiliza tena na bado naendelea kusikiliza. Napata burudani kusikiliza mashairi bora kabisa kutoka kwa chinga mmoja hivi aliyezaliwa Chitoholi kule Tandahimba, nasisimka zaidi nikiisikia sauti ya Mbibo halisi, mwanadada komando mwenye vyeo vyake kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Tanzania. Nitake nini tena kwenye mtima wangu kwa upande wa burudani, ipo raha kuwasikia.

Kule dada wa Kikurya toka Mara huku Konde boy chinga toka Mtwara, wameleta balaa jipya mjini 'Wife' bonge moja la wimbo niamini nachokuambia. Kama ulikuwa miongoni mwa watu wachache wasiofahamu mziki kusema eti Jide zama zimepita basi tafuta wimbo wa Wife halafu utajisahihishia mwenyewe.

Mwanadada Komando kama anavyofahamika kwa mashabiki zake ni kama amemkanya Harmonize kwamba mwana ukome, amemkomesha kwa sauti yake maridhawa na bila shaka akiwa studio alikuwa anajisema kwa kikurya 'let me show you' Mshamba mmoja wa Tandahimba. Sikiliza wewe Wife ni balaa na nusu nenda kaitafute halafu urudi hapa unibishe.

Watu wangu ambao hamjaoa sauti inatosha? Basi mwanetu Rajabu yule muuza kahawa wa zamani mitaa ya kariakoo ametuletea dude linatuhusu kabisa. Kwanza ametusanua yeye amechoka kuwa bachela, vipi yupo sawa au anasaliti kambi? Achana na hayo mambo kikubwa twende tukasikie midundo hatari, mashairi yaliyopangwa vema na sauti ya malkia wa muziki bongo Komando Jide.

Huyu Harmonize ameamua, kijana wa kimakonde amechagua kuwa somo kwa vijana wengi nchini, kila siku anatoa somo kwetu sina hakika kama vijana tumegundua kitu gani anahitaji tuchukue kwake. Ni uthubutu na kuweka nia ya dhati, Harmonize ametu'prove wrong' kwamba yapo maisha mengine baadae.

Vipi unapenda mziki mzuri? Usipoteze muda sasa fanya hima kawasikilize hawa wenye mziki wao. Harmo anamwimbia Jide, Jide naye anamjibu kwa mikogo na maringo. Hauchoshi kuusikiliza,ni balaa na nusu nishasema hapo juu.

Sikia sasa kumbe yule Komando wa Kikurya hana lolote kwa Chinga wa kilimani kule Mahuta, mwenyewe amekiri yeye ni Maji tu kwa Harmonize halafu mshikaji ni kama Chura yaani anayaoga anavyotaka. Nani ana namba ya yule Mnaijeria wa dada Judith atuambie alikwama wapi.

Balaa lipo kwa Harmo nawaambia, Chinga hata hakujali umri wala ukongwe wa Jide kwenye gemu ikasikika sauti toka kwake akimwambia wakipata watakula, wakikosa watalala. Unatamani kujua alijibiwa nini? Nenda kaisikilize nakuambia mara ya mwisho. Sema nilichogundua Jide siyo slay queen wala nini.

Eti zimewashuka sura waliojichosha na makafara, mmakonde ana mambo huyu! Inaweza isithibitishwe popote lakini huu wimbo wa Wife umerudisha tabasamu kwa mashabiki wa Simba baada ya kipigo cha Yanga, sio ajabu wala nini baada ya kusikiliza wimbo huu Antonio Nugaz ukimwita Utoporo atafurahi huku akichagiza wape salaaaaam mabachela wote.

TeAmo!!
 
HARMONIZE NA JIDE, BALAA NA NUSU

Nilisikiliza kwa mara ya kwanza, nikasikiliza tena halafu nikasikiliza tena na bado naendelea kusikiliza. Napata burudani kusikiliza mashairi bora kabisa kutoka kwa chinga mmoja hivi aliyezaliwa Chitoholi kule Tandahimba, nasisimka zaidi nikiisikia sauti ya Mbibo halisi, mwanadada komando mwenye vyeo vyake kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Tanzania. Nitake nini tena kwenye mtima wangu kwa upande wa burudani, ipo raha kuwasikia.

Kule dada wa Kikurya toka Mara huku Konde boy chinga toka Mtwara, wameleta balaa jipya mjini 'Wife' bonge moja la wimbo niamini nachokuambia. Kama ulikuwa miongoni mwa watu wachache wasiofahamu mziki kusema eti Jide zama zimepita basi tafuta wimbo wa Wife halafu utajisahihishia mwenyewe.

Mwanadada Komando kama anavyofahamika kwa mashabiki zake ni kama amemkanya Harmonize kwamba mwana ukome, amemkomesha kwa sauti yake maridhawa na bila shaka akiwa studio alikuwa anajisema kwa kikurya 'let me show you' Mshamba mmoja wa Tandahimba. Sikiliza wewe Wife ni balaa na nusu nenda kaitafute halafu urudi hapa unibishe.

Watu wangu ambao hamjaoa sauti inatosha? Basi mwanetu Rajabu yule muuza kahawa wa zamani mitaa ya kariakoo ametuletea dude linatuhusu kabisa. Kwanza ametusanua yeye amechoka kuwa bachela, vipi yupo sawa au anasaliti kambi? Achana na hayo mambo kikubwa twende tukasikie midundo hatari, mashairi yaliyopangwa vema na sauti ya malkia wa muziki bongo Komando Jide.

Huyu Harmonize ameamua, kijana wa kimakonde amechagua kuwa somo kwa vijana wengi nchini, kila siku anatoa somo kwetu sina hakika kama vijana tumegundua kitu gani anahitaji tuchukue kwake. Ni uthubutu na kuweka nia ya dhati, Harmonize ametu'prove wrong' kwamba yapo maisha mengine baadae.

Vipi unapenda mziki mzuri? Usipoteze muda sasa fanya hima kawasikilize hawa wenye mziki wao. Harmo anamwimbia Jide, Jide naye anamjibu kwa mikogo na maringo. Hauchoshi kuusikiliza,ni balaa na nusu nishasema hapo juu.

Sikia sasa kumbe yule Komando wa Kikurya hana lolote kwa Chinga wa kilimani kule Mahuta, mwenyewe amekiri yeye ni Maji tu kwa Harmonize halafu mshikaji ni kama Chura yaani anayaoga anavyotaka. Nani ana namba ya yule Mnaijeria wa dada Judith atuambie alikwama wapi.

Balaa lipo kwa Harmo nawaambia, Chinga hata hakujali umri wala ukongwe wa Jide kwenye gemu ikasikika sauti toka kwake akimwambia wakipata watakula, wakikosa watalala. Unatamani kujua alijibiwa nini? Nenda kaisikilize nakuambia mara ya mwisho. Sema nilichogundua Jide siyo slay queen wala nini.

Eti zimewashuka sura waliojichosha na makafara, mmakonde ana mambo huyu! Inaweza isithibitishwe popote lakini huu wimbo wa Wife umerudisha tabasamu kwa mashabiki wa Simba baada ya kipigo cha Yanga, sio ajabu wala nini baada ya kusikiliza wimbo huu Antonio Nugaz ukimwita Utoporo atafurahi huku akichagiza wape salaaaaam mabachela wote.

TeAmo!!
 
Mbona hujaweka hiyo audio hapa mkuu tuburudike?

Ila kama harmo hakulipi basi ntashangaa sana
 
[/QUOTE Si kwa barua hili kha, anyway Asante kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom