Harmonize kuongeza wasanii watatu August hii

anthony_art

JF-Expert Member
Jul 9, 2020
992
362
Habari wananzengo ,

Nimeona post ya Harmonize kuhusu kuwatambulisha wasanii WATATU (3) mwezi ujao (August) na kwa alivyoonyesha wawili (2) watakuwa watanzania ambapo mmoja Ni wa kiume na mwingine Ni wa kike lakini Kuna pia Kuna m_Nigeria ambaye Ni wa kiume.

Kama atafanikiwa kuwasaini wasanii hao label yake ya Kondegang(KMW) itakuwa na jumla ya wasanii watano, ambapo kwa sasaiv Ina wasanii wawili ambao Ni yeye mwenyewe harmonize na msanii wake Ibrah.

MTAZAMO WANGU:
Sijajua kwanini harmonize tangu atoke WCB na kuanzisha label yake ya Kondegang amekuwa na papara au haraka kiasi hicho, yaani anafanya Mambo mengi kwa muda mdogo.Akianzisha hiki kabla hakijafika mahali kinapotakiwa anaanzisha kingine.

Alipomsaini Ibrah niliona Ni mapema Sanaa Ila nikasema poa acha kijana ainue na wengine, lakini nikaona Tena anachanganya Mambo kwenye kumpromote kijana wake na Bado akaachia album na kijana wake akaachia Extended Playlist(EP).

Sasaivi Tena analeta wasanii WATATU je, ataweza kuwamaintain wasanii wote wakati nayeye Bado anhitaji kujitanua? Japokuwa si vibaya kuwainua wengine lakini Ni jambo linalohitaji techniques and tacts ili kuweza kumudu kuendesha label.

Ok, all in all naimani atakuwa amejipanga vilivyo kuweza kukabiliana na Hilo jambo na namuombea kwa M/Mungu.

MAONI YENU WANANZENGO.

#Kijana_Mpenda_burudani.
 
Ngoma ikivuma sana, nwishowe inapasuka Na pia mgema akisifiwa sana, tembo utia maji. So kazi kwake kusuka au kunyoa.
 
Baada ya uzinduzi wa Afro-East wakati akifanya press conference alihaidi tarehe 27 mwezi wa 6 ,atafanya launch ya album wake uwanja wa uhuru,special kwa ajili ya watu walikosa nafasi Mlimani City na akasema wasanii wote alio washirikisha ktk album yake wange kuwepo.

Lkn mpaka sasa hamna update yoyote kama wamehairisha au hawafanyi.Leo hii anakuja na lengine wakati huyo msanii wake Ibra hajasimama.Ila huwezi jua labda hela anayo ya kuichezea na huu mwaka kwa wasanii ni mgumu,show hamna wanategemea mauzo ya online.
 
Ni hataree!!! ngoja tuone maana jamaa anakurupuka saana Ana ahadi nyingi zisizo timia.Sasa ndo nimeanza kumuelewa producer bonga alichokisema kwamba jamaa alikuwa anamuahidi vi2 vingi lakini hakamilishi.
 
Kuna kikundi naona kinatamani kulia ila ndo hivyo sasa muziki uwe mpana sio wa kikundi fulani
 
Ni hataree!!! ngoja tuone maana jamaa anakurupuka saana Ana ahadi nyingi zisizo timia.Sasa ndo nimeanza kumuelewa producer bonga alichokisema kwamba jamaa alikuwa anamuahidi vi2 vingi lakini hakamilishi.
Remember na issue ile ya mgahawa sijui imeishia wapi?
 
Tatizo jamaa media zinamdanganya hana nguvu kiihivyo angejijenga kwanza na angemjenga msanii wake kuanzia kimauzo hadi kibiashara asikimbizanane nanwasafi Sio wajinga kumuweka msanii miaka minne benchi kwanza kumuandaa kisaikolojia na kuoanga technique. Sasa ibra tu hata garama hajarudisha bado tayari unaleta wengine 3 asiponagalia mwakani hatoboi na konde gang itakuwa hoiii. Music inahitaji management yenye tactic nafikiri akijifunza wasa Sio wajinga kuwa na mameneja zaidi 6. Diamond ni C.EO ila kazi zote wanafanya wengine na je msanii umemuandalia njiaa vya kutosha.
 
Inasemekana hao wasanii ni Marioo🇹🇿, Nandy🇹🇿 na Burna Boy🇳🇬
 
Tatizo jamaa media zinamdanganya hana nguvu kiihivyo angejijenga kwanza na angemjenga msanii wake kuanzia kimauzo hadi kibiashara asikimbizanane nanwasafi Sio wajinga kumuweka msanii miaka minne benchi kwanza kumuandaa kisaikolojia na kuoanga technique. Sasa ibra tu hata garama hajarudisha bado tayari unaleta wengine 3 asiponagalia mwakani hatoboi na konde gang itakuwa hoiii. Music inahitaji management yenye tactic nafikiri akijifunza wasa Sio wajinga kuwa na mameneja zaidi 6. Diamond ni C.EO ila kazi zote wanafanya wengine na je msanii umemuandalia njiaa vya kutosha.
Harmonize ajitambui
 
Habari wananzengo ,

Nimeona post ya Harmonize kuhusu kuwatambulisha wasanii WATATU (3) mwezi ujao (August) na kwa alivyoonyesha wawili (2) watakuwa watanzania ambapo mmoja Ni wa kiume na mwingine Ni wa kike lakini Kuna pia Kuna m_Nigeria ambaye Ni wa kiume.

Kama atafanikiwa kuwasaini wasanii hao label yake ya Kondegang(KMW) itakuwa na jumla ya wasanii watano, ambapo kwa sasaiv Ina wasanii wawili ambao Ni yeye mwenyewe harmonize na msanii wake Ibrah.

MTAZAMO WANGU:
Sijajua kwanini harmonize tangu atoke WCB na kuanzisha label yake ya Kondegang amekuwa na papara au haraka kiasi hicho, yaani anafanya Mambo mengi kwa muda mdogo.Akianzisha hiki kabla hakijafika mahali kinapotakiwa anaanzisha kingine.

Alipomsaini Ibrah niliona Ni mapema Sanaa Ila nikasema poa acha kijana ainue na wengine, lakini nikaona Tena anachanganya Mambo kwenye kumpromote kijana wake na Bado akaachia album na kijana wake akaachia Extended Playlist(EP).

Sasaivi Tena analeta wasanii WATATU je, ataweza kuwamaintain wasanii wote wakati nayeye Bado anhitaji kujitanua? Japokuwa si vibaya kuwainua wengine lakini Ni jambo linalohitaji techniques and tacts ili kuweza kumudu kuendesha label.

Ok, all in all naimani atakuwa amejipanga vilivyo kuweza kukabiliana na Hilo jambo na namuombea kwa M/Mungu.

MAONI YENU WANANZENGO.

#Kijana_Mpenda_burudani.
Aliyenaye hajamfikisha mbali bado
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom