Harmonize (Konde Boy) usiipe kisogo hadhira iliyokutoa jalalani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,777
699,220
Ni zamu ya Konde Boi kila kona. Si ki mashairi vina na midundo tena bali ziara za kuonesha ukwasi, kukubalika na ukaribu na mamlaka zenye nguvu.Tunda limewiva sasa kila mtu analitaka. Mkulima keshasahaulika. Nina machache kwako Konde Boi.

1. Kipaji adimu/adhimu. Hili halina ubishi kipaji kipo hasa cha utunzi wa nyimbo zinazogusa hisia.Na midundo inayohamasisha kucheza.Lakini daima mkumbuke aliyekushika mkono, aliyekulea, aliyekukuza. Aliyekutoa kusikojulikana mpaka leo upo hapo ulipo. Mheshimu sana huyu. Ana mustakabali juu yako. Usikubali kamwe kutumika ukamkejeli kumtusi ama kumsema vibaya

2. Ni haki yako kuondoka WASAFI. Kwa lugha nyingine tunasema mwana kakua. Na kama ni shule tunasema umehitimu. Nenda kwa amani, aga kwa furaha. Shukuru kwa kila jambo.Kaanze maisha mapya kwa miguu yako mwenyewe na kwa kujiamini. Lakini kamwe usinyee kambi. Usiteme bazoka kwa njugu za kuonjeshwa.

Hao wanaokusifu na kukupamba leo ndio hao hao walikudhihaki na kukutema mate huku wakikukimbia miaka mitatu tu iliyopita.

3. Punguza kuiga. Kuwa na ubunifu mpya japo wanasema learn from the best lakini angalia unaiga nini Ili isionekane kama ni copy n paste Utajimaliza. Hapa wanakusema na haya na mengine mengi.
. Aliponunua V8 jipya ukajibu mapigo
. Ameanzisha FM radio nawe unataka kufanya hivyo.
. Alipoenda Tandale na kugawa misaada ukaenda Kariakoo.

4. Ziepuke hila za wanasiasa. Wanakuona sasa kwakuwa kuna watu wamekupika na kuna hadhira ikakupokea. Wanasiasa hawana marafiki wa kudumu bali wana maslahi ya kudumu. Hadhira iliyokufikisha hapo haiko kwenye kundi la wanasiasa, ni fans wako toka imani tofauti, vyama tofauti, itikadi tofauti nknk. Usiikosee na kuipa kisogo. Ikishajigawa kwa matendo yako mbele yako iko mashakani. Wanasiasa wakutumie kwa faida huku ukibalance. Epuka ahadi za uongo

5. Waangalie watu wanaokuzunguka sasa na kukusujudia. Wanafanya hivyo kwakuwa unacho cha kuwapa na wanafaidika na wewe. Punguza ziara zisizo na tija. Chagua ya kuongea. Angalia unaongea nini na nani na wapi. Usikubali kamwe kuchonganishwa na walezi wako.

6. Wewe ni msanii sio mwanasisa. Achana na hizi ziara. Rudi kajichimbie utoe vitu vipya vikali zaidi. Muda unaopoteza utakugharimu labda tu kama hutaki kurudi kwenye gemu kwa matumaini ya ahadi ya ubunge.

7. Kuna kitu kinaitwa asili. Asili pia ni shina ama ni chanzo. Una asili na WASAFI na Mondi. Kamwe usikubali kugombanishwa naye. Nasema usikubali. Shina ni shina tuu. Wakati unasubiri kumalizana na WASAFI. Usirukeruke. Hawa wapambe kila kona wanakupoteza na kukupotosha pakubwa.

Nitaendelea panapo majaliwa.

Ndimi Jr, fan wa kazi zako.
 
Anaumia kutoa milioni 500..? Kama nakumbuka vema kuna Interview ya Diamond alisema kutoa ile nyimbo ya kwanza ya Hamonize Aiyola iligharimu milioni 100. Je vip kuhusu gharama nyingine za kumbrand..? Ili awe Hammonize? Zinaweza kuwa hazikufikia milioni 500? Kwa miaka yote mitatu?
Kama ya kuitwa Hamonize alikuwa na uwezo wa kuingiza tsh ngapi?

Lingekuwa jambo jema asizungumzie kuhusu mkataba wake na alikotoka kwenye media, sbbu kinachotokea sasa headline kwenye media zote ni tsh milion 500.
 
Kuna ushauri umempa kama kijana au yyte yule ni vema kuufanyia kazi,lkn kama kijana na star kuna maisha inabid aishi ili kulinda na kukuza brand yake,so maisha ya magar na mengne ni ustaa tu lkn pia kutengeza ushindan ni kukua pia,sasa kwann usishindane na mtu aliekuzidi.

Mwisho nimesikia interview yake leo mbona asilimia 98 jamaa alikua positively sana..imagine kwa visa vya chini anavofanyiwa nae angeamua kuongea ya moyon au kinachoendelea tena alikua ana nafas kubwa ktk kituo cha redio wapinzan,ingekuwaje. Tumpe sapoti na kama anavosisitiza kudumisha aman kwan ktk WCB ana mchango pia tena mkubwa mnooooo hata kama alishikwa mkono.
 
Napata mashaka Sana kama konde boi ataweza kusustain maisha nje ya WCBOO!!

japo kujitegemea ni jambo Zuri ila gia aliyoanza kuiweka sasa kwenye zile media zingine ni mbaya itam_backfire aanze kumkumbuka mondi

Hili saga la konde na wasafi inanifanya niukumbuke wimbo wa mondi wa "je utanipenda" hasa pale anapomzungumzia huyu dogo konde
 
Nimeisikiliza yote... Naweza kusema ni the best interview ever kwa wasaniii wetu hawa wa kibongo... Watangazaji walitaka kumtumia kuendeleza bifu lakini amewa outsmart pakubwa... Amewa frustrate sana haya yule wa kike...
Bado ana heshima kubwa kwa WASAFI na anawathamini na kuwaheshimu na kuwategemea sana... Amakinike tu na team yake na ahadi ya ubunge
Kuna ushauri umempa kama kijana au yyte yule ni vema kuufanyia kazi,lkn kama kijana na star kuna maisha inabid aishi ili kulinda na kukuza brand yake,so maisha ya magar na mengne ni ustaa tu lkn pia kutengeza ushindan ni kukua pia,sasa kwann usishindane na mtu aliekuzidi...
Mwisho nimesikia interview yake leo mbona asilimia 98 jamaa alikua positively sana..imagine kwa visa vya chini anavofanyiwa nae angeamua kuongea ya moyon au kinachoendelea tena alikua ana nafas kubwa ktk kituo cha redio wapinzan,ingekuwaje...tumpe sapoti na kama anavosisitiza kudumisha aman kwan ktk WCB ana mchango pia tena mkubwa mnooooo hata kama alishikwa mkono.
 
Back
Top Bottom