Hari tete mgodi wa dhahabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hari tete mgodi wa dhahabu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GITU, Jun 4, 2012.

 1. GITU

  GITU Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SHERIA ZAWEKWA KARI,
  WATU WANAPIGWA MPAKA KUWA VIREMA HATIMAYE KUPOTEZA UHAI.
  Ndugu zangu wanajamiiforum hari bado ni tete huku machimboni,Nyaruyeye ni miongoni mwa kijiji kinachojipatia umaarufu kwa upatikanaji wa Madini ya dhahabu kwa hari ya juu.Kijiji hiki kinapatikana Mkoa mpya wa Geita(hapo awali ilijulikana kama Wilaya ya geita) jimbo la Busanda kata ya Nyarugusu,
  mnamo mwaka jana mwezi wa tisa wazee watatu wakazi Wa nyarugusu katika shughuli zao za Uchimbaji waligundua uwepo wa dhahabu katika kijiji cha nyaruyeye umbali ni kama Kilomita 3 kutoka kijiji Cha nyarugusu ndipo taarifa zikaenea kila sehemu wachimbaji kutoka sehemu mbalimbali walifika sehemu ile na hatimaye kupata Matunda waliokuwa wakitafuta,kutokana na eneo hilo kati ya wazee wale watatu walio gundua miongoni mwao alikuwamo mwenyekiti wa Kijiji,kutokana kuwa sehemu hiyo ilikuwa inautata yaani maliasili waliamua kumtafuta mtu mmoja kwa jina Akifahamika kama Baraka yaani afanye mpango Ikibidi apate kibari kitakachowawezesha kuwa na ruhusa ya kuchimba Bira Buguza.Ndipo mashariti Magumu yalipoanza kuwawia wachimbaji hao ikabidi sehemu hiyo iendeshwe kwa taratibu sio kuchimba kwa mtu tu akijisikia,swala hilo halikuwafurahisha wachimbaji na hatimaye wakaamua kuandamana kwa sababu ya yule bwana kwani waliona anataka kuwanyanyasa,Ndipo ikabidi wakaishambulie nyumba yake kwa kuichoma moto,kwa kweli Mapolisi walijitahidi lakini hawakuweza kutuliza ghasia,ndipo walipoomba msaada wa asikari kutoka wilayani hawa wasiokuwa na huruma walianza kuwatupia mabomu ya machozi,watu hawa hawakusikia waliendelea kuwalushia mawe hali wakitaka kuwepo na hari ya uurudishwaji wa eneo hilo baada ya kutiwa mkazo, Askari hawa Wakiwa wamekodiwa kutoka Mkoani mwanza kwa gharama ya huyo bwana,
  walianza kuwapiga risasi watu wasiokuwa na hatia, Kijana mmoja akiwa katika harakati ya kukimbia alipigwa risasi ya kichwa hapohapo na kupoteza maisha karibia na Eneo la shule ya msingi nyarugusu,kijana watu wengine walipigwa rasasi za miguu na kijana mmoja alilushiwa bomu likaharibu sehemu zake za makario yaani **** lote la kushoto likamwagika.Kutokana na gasia hizo mgodi huo ukafungwa,ndipo kukawapo na mzozo kati ya eneo hilo na maliasili wao wakadai sehemu hiyo ni game sasa hairuhusiwi,ndipo wakaibuka matajiri wengine wakadai hilo ndio eneo lao kwani limevamiwa,bwana yule alieyesabisha migogoro yeye hakuwa na elimu yoyote isipokuwa Pesa tu.
  Sasa Mgodi ukafungwa kabisa, ndipo baadae mwaka huu mgodi ukafunguliwa mwezi wa nne baada ya wao kumaliza migogoro yao,
  SHIDA IKAANZA KWA WATANZANIA WASIO KUWA NA HAKI RASILIMALI ZAO.

  Kwa kweli inasikitisha ndugu zangu unaweza kutamani Mwisho wa Dunia kama Upo Basi uje Mapema Uwapumzishe watu kutoka sehemu mbalimbali nimeshudia watu wakimiminika kutoka sehemu mbalimbali wakija kutafuta madini ya dhahabu,na sheria ndio imekwisha kuwa ngumu bila kitambulisho haurusiwi kuingia Mgodini humo,kwani baada ya mgogoro kwisha walizungushia senyenge, Ndugu zangu kwa kweli sehemu hiyo kuna dhahabu lakini zinagharimu maisha ya watanzania,
  Mtu huyo amekodi askari anaowalipa, Askari hawo wamekuwa kama makaburu wanapiga watu mpaka kuwa vilema, na hata kupoteza Uhai ikitokea umepita na matope kwenye nguo utapigwa kama umbwa, kwani ukibahatika kuosha yale utapata dhahabu,
  Mgodi huu unaenda kinyume na haki za binadamu,pia nilishudia mwanafunzi mwenzangu alikwenda mgoni huko,alikosea mashariti kupita sehemu ilioandikwa kwa njia hii kwa ajili ya magari,
  kwa kweli ukiwa huku inasikitisha sana Kwa hiyo Viongozi wajaribu kuangalia watu hawa wanaopigwa mpaka kuwa vilema hatimaye kupoteza maisha yao,(gitumabula@gmail.com)
   
 2. GITU

  GITU Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu mmoja amekufa Nilijaribu kuonge na kijana anayechimba eneo hilo alishuhudia askari wakimwambia "potea hapa" baada ya kumpa kipigo baada ya siku mbili wakamuokota amekufa wapi tunakokwenda hadi sasa watu wawili wamepoteza maisha na watu wanaogopa kweli kuyaweka wazi sasa haya,kama unaweza kupata habari zaidi niandikie kwenye Email yangu nikuunganishe na mtu huyu akujuze zaidi kwani inatia uchungu, kuona ndugu, rafiki zetu wakiadhibiwa kiasi hiko.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,410
  Trophy Points: 280
  Poleni kwa yote, ila mengine mmeyataka wenyewe!. Kwa wasio ijua Nyarugusu kiukweli ni dhahabu nje nje kwa wachimbaji wadogo lakini wakazi wake ni masikini wa kutupa. Wanaishi katika lindi la umasikini uliotopea, maisha yao ni duni,hohe hahe, hawana mbele wala nyuma. Mahali hapo pako kama motoni wakati jirani na hapo ndipo ulipo mgodi wa GGM, humo ndani ni peponi!. Wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Busanda, wakazi wake waliliahidiwa kuonja pepo kama GGM kama wangechagua mabadiliko!. Mgombae wa CDM aliwaahidi kuhakikisha huo mrahaba wa GGM unawafaidia wao kwanza. Wale wale waliirudisha CCM iliyo watenda hivyo miaka nenda miaka rudi, sasa mnalalamika nini!?!.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Mkuu poleni kwa yanayowafika, nimesikitika, hii habari imenigusa kwa kweli. viongozi uchwara kuupindua ukweli usomeke uongo!!! wanapotosha haki mchana kweupe. kwa stail hii eti nape anataka tuiunge mkono ccm!
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Pasco labda sasa wamejifunza, tusiwalaumu sana! tuwahurumie na kujaribu kuwasaidia kama usaidizi upo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Imany John

  Imany John Verified User

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  usilolijua
   
 7. GITU

  GITU Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kweli,sehemu hii baadhi wamekuwa wakikipigia kura hususani watu wote wasio ona mbali,
  baada ya uchaguzi mdogo ambapo walimrudisha mbunge wa Ccm ndipo Walipoona mateso zaidi,na chakusikitisha vijana wengi tulikuwa hatuna hamasa ya upigaji kura, lakini kwa sasa swala hilo tulilivalia njuga na kuhakikisha kuwa kila kijana awe na kadi ya kupiga kura,pia na wakina mama wengi waliokuwa wamekibeba hicho chama kwa kupewa
  Chumvi
  Kanga wamekuwa wakilani vikali Jinsi gani chama hicho kinavyo wakanyaga wanyonge na Kuwabeba Matajiri pasipo kujari Utu na Thamani ya Watanzania,wachimbaji mababu bibi vizee nao wamedai wamechoka na chama hiki kwani kilichokuwa kikituangusha ni sisi vijana kuwa na ushabiki bila ya kuwa na kadi ya Mpiga kura, pia watu wamezuiwa kuingia na simu,ningekuwa na digital camera ningewapa picha kamili ya eneo hilo.
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Inabidi uwe makini pia, wasijewakateka mkuu. Cha msingi ni kujitolea na kutoa elimu kwa wasiokuwa nayo! jitahidini kuwaelimisha ndugu na jamaa ili kila mmoja wenu muweze kupiga hatua kimaendeleo. Sidhani kama jirani yako analala njaa wewe unakula hadi unabakisha utakuwa una maisha ya furaha siku zote, rahasha! ipo siku moja utagundua/utakuwa na huruma zaidi ya sasa kuona kila mmoja akifurahia kuishi.
   
 9. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wewe kama umeweza kurusha hili bango, basi ni mjanja! jitahidi kama hakuna chama makini basi jiandikisheni hadi watu 30 mfungue tawi dogo la chama makini CDM. Naimani kwa msaada wa makamanda walioko maeneo ya karibu watawapeni msaada zaidi.
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,225
  Trophy Points: 280
  kidumu chama cha mapinduzi..

  ccm oyeeee
   
Loading...