Wamtaa huu
Senior Member
- Jan 21, 2011
- 168
- 55
1.Katibu wake mkuu anakabiliwa na kesi aliyofunguliwa na Rose Kamili.
Kwamba anamuwekea pingamizi la ndoa iliyokuwa imetajwa kufanyika july 21 mwaka huu.Pamoja na mambo mengine Kamili anadai alipwe fedha za matunzo ya watoto.
Hali hii kwa katibu mkuu wa chama inamfanya kupoteza muda mwingi kudeal na kesi hiyo na chama kukabiliwa na wakati mgumu.Pia mahasimu wao wa kisiasa wanatumia mwanya huo kuwaharibia kuwa kuhusu uadilifu na hawafai kuongoza nchi.
2.Wabunge wa chadema ambao bado hawajatajwa majina wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfuasi wa CCM yaliyotokea juzi Ndago mkoani Singida.Akiongea kwa kujiamini mbunge Mwigulu Nchemba leo asubuhi bungeni amedai kuwa na ushahidi wa sms za vitisho kutoka kwa wabunge wao ambazo zinawaunganisha moja kwa moja wabunge hao wa chadema.Pia Spika Makinda alidai kufahamishwa jambo hilo na kulaani kitendo hiko na kulitaka jeshi la polisi lichukue hatua stahiki.Hapa chama kimewekwa pabaya kwakuwa makada wake na viongozi waandamizi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji.
3.Kiongozi makini wa chama na katibu mwenezi taifa John Mnyika anakabiliwa na mashtaka ya kuthibitisha maneno aliyoyatoa hivi karibuni dhidi ya Mwigulu Nchemba kuwa anahusika kwenye kashfa ya EPA.Kuna viashirio vingi kuonyesha kuwa ushahidi ama haujawasilishwa au haukidhi kujitoa kwenye sakata hilo.Kama hivyo ndivyo Mnyika atapelekwa kwenye kamati ya haki na madaraka ya bunge na anaweza apewe adhabu kali.
Hili linakipa chama wakati mgumu.Mnyika anajulikana umuhimu wake kwa chadema ndani na nje ya bunge.Kukosekana kwake bungeni na/au kutumia muda mwingi kupambana na hili suala kunainyima chadema kuufaidi ufanisi wake wa kipekee kwa 100%.
4.Hivi karibuni ililipotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa kuna makada watatu wa chadema wawili kati yao wakiwa ni viongozi na wote wakiwa ni wajumbe wa kamati kuu taifa ya chama kutishiwa maisha yao na kinachoitwa usalama wa taifa.Viongozi hao ni katibu mkuu taifa Wilbroad Slaa,John Mnyika(uenezi taifa) na Godbless Lema.Hili pia ni chungu kwa chama na linalenga kufifisha nguvu ya chadema inayoenea kwa kasi kwani viongozi wake muhimu wanatembea na hofu ya kuhofia maisha yao wakati wowote na hivyo kukipa chama wakati mgumu.