Harakati za WAMA project against Lowassa zinanikumbusha hii story...

Joined
May 20, 2013
Posts
71
Reaction score
151
Ni ukweli usiofichika sasa kwamba wale marafiki wa siku nyingi ambao hawakukutana barabarani sasa hawapikiki chungu kimoja. Mfarakano huu kila mtu anauelezea kwa tafsiri yake na kwa jinsi anavyouona. Kila kambi ya hawa marafiki wa zamani ina wafuasi wake. Mimi sijui ugomvi wao ulianzaje ingawa tetesi ni nyingi. Wapo wanaosema kuwa walikubaliana mmoja wao aanze kuongoza kipindi kimoja halafu amwachie mwenzake, lakini baada ya huyo aliyeanza kuongoza kuonja utamu wa madaraka akakataa kumwachia huyo mwenzake.

Wapo wanaosema kuwa walikubaliana mmoja aongoze vipindi vyote viwili ila amtengenezee mazingira mwenzake ya kuja kumpokea kijiti, sasa EL akawa hana subra akaanzisha harakati za kumng'oa mwenzake kipindi cha pili kwa kutumia style ile ya J.Zuma. kulazimisha kutenganisha kofia mbili ya uraisi na chama ili abaki na ya uraisi ili chama kimshugulikie. akawapeleka akina Bashe front kule dodoma wakati wa mkutano mkuu wa CCM mbinu ikabumbuluka.

Katika vijana waliojipambanua kuwa front katika kumshambulia Lowassa ni huyu bwana mdogo anaitwa Paul Makonda, Yeye baada ya kumtukana Lowassa kwenye vyombo vya habari akazawadiwa na Mkuu wa kaya ujumbe kwenye bunge la katiba, Huko bungeni pamoja na mtaani ni rafiki mkuu wa mtoto wa mkuu, riz1. Pamoja na kuendesha harakati za kumchafua Lowassa kwenye vyombo vya habari ila sasa ni ukweli usiopingika ukiwa na ushahidi wote kuwa yeye ndiye mmiliki wa akaunti ambayo haijathibitishwa yenye jina la CHABRUMA, ambayo ni maarufu sana hapa JF kwa kumchafua Lowassa na watu wote wanaomuunga mkono akiwepo mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa bwana Apson Mwang'onda.

stori yenyewe:

Mfarakano huu unanikumbusha kisa kimoja kilitokea wilaya ya Songea enzi hizo. Kulikuwa na vijana maarufu pale songea mjini waliokuwa wanaendesha maisha yao kwa kutegemea wizi akina IFUNDA, JULLY NGOZINGOZI,KACHALA, RAMSO n.k, hawa vijana inasemekana walikuwa wanajifua sana kwa mazoezi ya viungo ikiwepo na karate. Aliyekuwa ni tishio sana alikuwa ni huyu RAMSO inasemekana alikuwa na mkanda mweusi, wenyewe walikuwa wanamuita 'master'. Sasa siku moja, RAMSO NA JULY walipewa dili na mfanyakazi wa kampuni moja ya kununua tumbaku kuwa kuna hela kama mil 40 zinatarajiwa kusafirishwa kwenda kijiji kimoja kwaajili ya kununua tumbaku kwa wakulima hivyo wakae mkao wa kula. RAMSO alikuwa na bastola ila ilikuwa na risasi 2 tu, hivyo July na Ramso walienda kule kijijini porini wakaweka mawe njiani ili ile gari ikifika waiteke wachukue zile hela.

Siku ilipowadia lile gari la kampuni likaondoka na dereva, mhasibu na afisa mmoja, gari ilikuwa ni defender. wakati defender ikielekea kule kijijini, njiani walikutana na wakulima wanaowafahamu wanaelekea hukohuko hivyo wakawapa lifti. Sasa gari ilipofika kwenye yale mawe, dereva akasimama asijue kama ni mtego, wale wananchi waliopewa lifti nao wakashuka ili watoe yale mawe, gafla Ramso akatokea upande wa dereva na July akatokea upande mwingine, Ramso akapiga risasi ya kwanza hewani, wakaogopa wote wengine wakarudi kwenye gari wengine wakalala chini, hapohapo July akafungua mlango wa mbele akatoa ule mfuko wenye fedha akaanza kukimbia nao kuelekea maporini, sasa mmoja kati ya wale wananchi akataka kuanza kumkimbiza, ikabidi Ramso atake kumpiga risasi yule mwananchi, Mungu saidia ile risasi ikamkosa, sasa yule mwananchi kumbe alipitia JKT hivyo akatambua kuwa ile risasi ilikuwa ya mwisho, kwenye magazini hamna nyingine, akawaambia wengine kuwa 'hamna kitu risasi zimeisha', kwanza wananchi wengine wakawa wanasita, yeye mwenyewe akamvamia Ramso na kuanza kupigana naye, kuona hivyo wananchi wale waliobaki wakashirikiana kumpiga ramso mpaka wakamfunga kamba sasa yule mhasibu akawasihi wasimuue ili aende akamtaje July aliekimbia na fedha, wakamchukua wakampeleka polisi.

July akatajwa polisi akamatwa, alipokamatwa basi akaanza kuhonga polisi na hakimu ile kesi ilipoenda mahakamani Ramso akakataa kuwa alikuwa na July, wale wananchi walipoletwa mahakamani kumtambua July wakasema hawakumuona sura, hivyo July akakutwa hana hatia ila Ramso ndio mwenye hatia ikapangwa tarehe ya hukumu. Walikuwa wamepanga Ramso amkatae July ili atoke halafu wamuhonge hakimu ampe kifungo kidogo Ramso. Sasa July alipotoka nje akaona Ramso akitoka watatakiwa wagawane zile hela, akaamua kumuhonga hakimu hela ili amfunge Ramso miaka mingi asitoke nje tena. Sasa ramso wakati akisubiri hukumu akashangaa mbona July haji kumuona tena kule jela, akawa anapata story kwa ndugu zake jinsi July anavyotumia zile hela kwa fujo, basi Ramso akawaomba ndugu zake wajichange na akauza na pikipiki aliyokuwa nayo ili wakaongee na hakimu. Ndugu za Ramso walivyoenda kuongea na hakimu, akawaambia kuwa yeye hawezi kuchukua hela mara mbili, ameshapewa hela na July na maelekezo ya nini cha kufanya, ndugu za Ramso wakajua kuwa july ameshampa hela hakimu, hivyo ndugu yao atatoka.

Siku ya hukumu, Hakimu alimfunga Ramso miaka 45 jela, baada ya hapo july akatumbua zile hela zikaisha akaendelea na kazi yake, safari hii akaenda na SHAIBU KALUWA kuiba computer peramiho mission. wakakamatwa wakawekwa selo za polisi pale central songea. Sasa kivumbi kikawa inabidi July na Shaibu wapelekwe pale magereza kusubiri kesi yao kwa kuwa kule central hawaweki watuhumiwa muda mrefu. July akamwomba mkuu wa kituo asimpeleke kule magereza yupo Ramso atamuua. Kilichofanyika ni kusubiri mpaka Ramso ahamishwe gereza ndio july apelekwe gerezani. Sijui ni nani aliye-coordinate hiyo move lakini mwisho wa siku Ramso alihamishiwa gereza la Ukonga DSM ndio july akapelekwa pale magereza. Ile kesi ilivyoisha July na Shaibu walifungwa miaka 16 jela, sijui kama huko mbele walikuja kuonana, ila niliongea na Ramso pale Ukonga siku moja akasema alikuwa anategemea rufaa ingemtoa lakini rufaa zake zote mbili zilidunda na siku akikutana na July gerezani ndio itakuwa mwisho wa maisha yake lazima mmoja kati yao afe.

when close friends turn enemies, the relation is deadly, refer 2pac and BIG.
 
Ok,mkuu sasa tupe connextion na ishu ya EPL (edwar president lowasaa ) na hyo mkuu wa kaya
 
connection ni kwamba, JKjr, hawezi kuruhusu mazingira ya EL kuwa rais, kwa kuwa kesha mtenda vya kutosha na akipata urais, atalipiza kisasi. hivyo el asahau ukuu wa nchi hii
 
Inakuja,Inakuja...:....aaaah, imekata wadau..!!!

Nataka kumjua Ramso na July kati ya EL na MKUU wa magogoni, hivi aweza kuwa nani kati yao

Ooooh, sasa nimekumbuk kile kikao cha NEC mwaka jana...!! Naambiwa EL alifunguka mbaya sana ambapo bila UNCLE BEN mambo yangekuwa Shaghalabaghala....."Muheshimiwa Mwenyekiti, Natukanwa sana kwa mambo ambayo sikufanya sasa hebu niambie ni jambo gani ambalo mimi sikukuambia ktk mkataba huo(Richmond) hata ulipokuwa nje ya nchi nilikujilisha juu ya hilo lkn wewe ukaniambia nisubiri kwanza ni "upepo tu utapita", sasa leo nashambuliwa peke yangu kwa kukubali kwangu kulinda serikali yangu ilhali Mkiti wangu unajua kila kitu "Niambie ni kitu gani ambacho hukijui na wala sikukuambia"??......(Hapo tunaambiwa Mkiti akataka kufungua mdomo) lahaula lakwata Uncle akaingilia kati na kumkanya mkulu asijibu lolote (namlaani sana mr clean) na mambo yakaishia hivyo

Ooooh, kweli hawa watu hawakukutana mabarabarani....Sasa ndo nataka kumjua kati yao ni nani Ramso na Jully..!!! Mtoa mada nikichemsha msaada wako tafadhari hata kwa PM

BACK TANGANYIKA
 
connection ni kwamba, JKjr, hawezi kuruhusu mazingira ya EL kuwa rais, kwa kuwa kesha mtenda vya kutosha na akipata urais, atalipiza kisasi. hivyo el asahau ukuu wa nchi hii

Aiseeee nikiri hapa umenizidi uelewa...!

BACK TANGANYIKA
 
Ni ukweli usiofichika sasa kwamba wale marafiki wa siku nyingi ambao hawakukutana barabarani sasa hawapikiki chungu kimoja.

when close friends turn enemies, the relation is deadly.
Mkuu Henrich, asante kwa kisa hiki, nimeguswa sana na uwezo wako wa kusimulia, connecting the dots na ku correlate unconnected issues of the same real life scenario!, ukimaliza masomo yako hapo UDOM, you'll be very useful to this country, hongera!. Sijapenda ulivyofanya "name calling" kwa kuwataja majina halisi watu halisi na kuyalinganisha na majina fake ya humu jf, hili ni kosa, na ushukuru Mungu, uzi umepanda usiku, mode akiamka, uzi huu unaweza kufutwa kama wenyewe wakilalamika!.

Tukija kwenye issue at hand, ila kiukweli kabisa, hawa jamaa sio maadui, thay are one!, and huo uadui unaonekana. that is the plan!, yaani ndio mpango wenyewe ili waonekane ni maadui!, ili siku ya siku ikifika, hoja ya kumptisha EL iwe, yeye ndio chaguo la wengi!, yeye ndio salama ya CCM!, "its not me!", "mimi simo!".

Amini nakuambia, ukikitoa kitisho cha afya ya huyu jamaa, then 2015 ni yeye tuu!. Hvyo vikaragosi ulivyovitaja !, vinatumika tuu kumchafua zuga kama "pace makers!", ili atakapopitishwa isemekane ni kwa sababu hazuiliki!. Kikaragosi mkuu wa mavuvusela wote wa CCM, keshalijui hili!, ndani ya CC ya CCM walipoamua kuanzisha ile kampeni ya "Vua Gamba", ili kumlazimisha ajivue!, ni mkulu mwenyewe ndiye aliyawatuma kuianzisha ili kuonyesha hamuhitaji kabisa!, na mijitu ya CCM ilivyo mijinga, ikamuamini kuwa ni kweli, Mzee hamuhitaji "jamaa", vuvusela likapulizwa na kuungumishwa nchi nzima "watu wamepewa siku 90!", zilivyopita, vuvuzela mkuu akaubaini kuwa it was just a game!, siku hizi hutamsikia te na "vuvusela mkuu" akizungumza chochote against "mtu huyu!". Hivyo vikaragosi vingine ni vinajifurahisha tuu kwa kujitekenya na kucheka vyenyewe!.

Subiria utashangaa na unaweza usiyaamini macho na masikio yako, pale atakapoibuka kuwa ndiye yeye!.

Pasco.
 
Mwaka 2015 ni mwaka wa MAADUI kuwa MARAFIKI,na marafiki kuwa maadui
 
Ulikuwa wapi na hiyo story yako ya kutunga? Acheni kutumika vibaya nyie vijana wa WAMA, mnahangaika sana EL yuko kimya, anatafuta kura
 
Mimi sipati logic ta kikwete kuingilia mambo ambayo haitaji. Ni kitu gani kama sio wivu tu. Wakwere bwana.
 
mmhuh kaz kwelikweli. Kiti kimoja wanao kitaka kibao, Sita, Membe, Lowasa, Wasira, Mwigulu, Kigwangala, Mwankyembe, Pinda, Sumaye, Lipumba, Slaa,na Magufuri. Nawapambe hawaachi kuwatia joto ili wale hela zao, bora baba angu awe rais maana yeye hana chuki na mtu.
 
Nitamshangaa sana Mh. Lowassa kama hatagombea urais kwa namna yoyote iwe ni kupitia CCM ,binafsi au Upinzani.
Ndoto yake na vita anayopigwa ni kama ile ya Jummong kwenye filamu ya Kikorea.

Watu anao ,uwezo wa kuongoza anao ,uwezo wa kutawala anao,uwezo wa kutoa maamuzi magumu anao,uwezo wa kubuni mikakati anao, uwezo wa kushawishi anao,uwezo wa kusimimia mipango yake na ya serikali serikali anayo,
Marafiki wa kumuunga mkono anao na pesa za kuchukua form anazo.

Sioni sababu ya kusubiri kuungwa mkono na mtu mmoja au familia ya mtu mmoja.
 
Ni ukweli usiofichika sasa kwamba wale marafiki wa siku nyingi ambao hawakukutana barabarani sasa hawapikiki chungu kimoja. Mfarakano huu kila mtu anauelezea kwa tafsiri yake na kwa jinsi anavyouona. Kila kambi ya hawa marafiki wa zamani ina wafuasi wake. Mimi sijui ugomvi wao ulianzaje ingawa tetesi ni nyingi. Wapo wanaosema kuwa walikubaliana mmoja wao aanze kuongoza kipindi kimoja halafu amwachie mwenzake, lakini baada ya huyo aliyeanza kuongoza kuonja utamu wa madaraka akakataa kumwachia huyo mwenzake.

Wapo wanaosema kuwa walikubaliana mmoja aongoze vipindi vyote viwili ila amtengenezee mazingira mwenzake ya kuja kumpokea kijiti, sasa EL akawa hana subra akaanzisha harakati za kumng'oa mwenzake kipindi cha pili kwa kutumia style ile ya J.Zuma. kulazimisha kutenganisha kofia mbili ya uraisi na chama ili abaki na ya uraisi ili chama kimshugulikie. akawapeleka akina Bashe front kule dodoma wakati wa mkutano mkuu wa CCM mbinu ikabumbuluka.

Katika vijana waliojipambanua kuwa front katika kumshambulia Lowassa ni huyu bwana mdogo anaitwa Paul Makonda, Yeye baada ya kumtukana Lowassa kwenye vyombo vya habari akazawadiwa na Mkuu wa kaya ujumbe kwenye bunge la katiba, Huko bungeni pamoja na mtaani ni rafiki mkuu wa mtoto wa mkuu, riz1. Pamoja na kuendesha harakati za kumchafua Lowassa kwenye vyombo vya habari ila sasa ni ukweli usiopingika ukiwa na ushahidi wote kuwa yeye ndiye mmiliki wa akaunti ambayo haijathibitishwa yenye jina la CHABRUMA, ambayo ni maarufu sana hapa JF kwa kumchafua Lowassa na watu wote wanaomuunga mkono akiwepo mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa bwana Apson Mwang'onda.

stori yenyewe:

Mfarakano huu unanikumbusha kisa kimoja kilitokea wilaya ya Songea enzi hizo. Kulikuwa na vijana maarufu pale songea mjini waliokuwa wanaendesha maisha yao kwa kutegemea wizi akina IFUNDA, JULLY NGOZINGOZI,KACHALA, RAMSO n.k, hawa vijana inasemekana walikuwa wanajifua sana kwa mazoezi ya viungo ikiwepo na karate. Aliyekuwa ni tishio sana alikuwa ni huyu RAMSO inasemekana alikuwa na mkanda mweusi, wenyewe walikuwa wanamuita 'master'. Sasa siku moja, RAMSO NA JULY walipewa dili na mfanyakazi wa kampuni moja ya kununua tumbaku kuwa kuna hela kama mil 40 zinatarajiwa kusafirishwa kwenda kijiji kimoja kwaajili ya kununua tumbaku kwa wakulima hivyo wakae mkao wa kula. RAMSO alikuwa na bastola ila ilikuwa na risasi 2 tu, hivyo July na Ramso walienda kule kijijini porini wakaweka mawe njiani ili ile gari ikifika waiteke wachukue zile hela.

Siku ilipowadia lile gari la kampuni likaondoka na dereva, mhasibu na afisa mmoja, gari ilikuwa ni defender. wakati defender ikielekea kule kijijini, njiani walikutana na wakulima wanaowafahamu wanaelekea hukohuko hivyo wakawapa lifti. Sasa gari ilipofika kwenye yale mawe, dereva akasimama asijue kama ni mtego, wale wananchi waliopewa lifti nao wakashuka ili watoe yale mawe, gafla Ramso akatokea upande wa dereva na July akatokea upande mwingine, Ramso akapiga risasi ya kwanza hewani, wakaogopa wote wengine wakarudi kwenye gari wengine wakalala chini, hapohapo July akafungua mlango wa mbele akatoa ule mfuko wenye fedha akaanza kukimbia nao kuelekea maporini, sasa mmoja kati ya wale wananchi akataka kuanza kumkimbiza, ikabidi Ramso atake kumpiga risasi yule mwananchi, Mungu saidia ile risasi ikamkosa, sasa yule mwananchi kumbe alipitia JKT hivyo akatambua kuwa ile risasi ilikuwa ya mwisho, kwenye magazini hamna nyingine, akawaambia wengine kuwa 'hamna kitu risasi zimeisha', kwanza wananchi wengine wakawa wanasita, yeye mwenyewe akamvamia Ramso na kuanza kupigana naye, kuona hivyo wananchi wale waliobaki wakashirikiana kumpiga ramso mpaka wakamfunga kamba sasa yule mhasibu akawasihi wasimuue ili aende akamtaje July aliekimbia na fedha, wakamchukua wakampeleka polisi.

July akatajwa polisi akamatwa, alipokamatwa basi akaanza kuhonga polisi na hakimu ile kesi ilipoenda mahakamani Ramso akakataa kuwa alikuwa na July, wale wananchi walipoletwa mahakamani kumtambua July wakasema hawakumuona sura, hivyo July akakutwa hana hatia ila Ramso ndio mwenye hatia ikapangwa tarehe ya hukumu. Walikuwa wamepanga Ramso amkatae July ili atoke halafu wamuhonge hakimu ampe kifungo kidogo Ramso. Sasa July alipotoka nje akaona Ramso akitoka watatakiwa wagawane zile hela, akaamua kumuhonga hakimu hela ili amfunge Ramso miaka mingi asitoke nje tena. Sasa ramso wakati akisubiri hukumu akashangaa mbona July haji kumuona tena kule jela, akawa anapata story kwa ndugu zake jinsi July anavyotumia zile hela kwa fujo, basi Ramso akawaomba ndugu zake wajichange na akauza na pikipiki aliyokuwa nayo ili wakaongee na hakimu. Ndugu za Ramso walivyoenda kuongea na hakimu, akawaambia kuwa yeye hawezi kuchukua hela mara mbili, ameshapewa hela na July na maelekezo ya nini cha kufanya, ndugu za Ramso wakajua kuwa july ameshampa hela hakimu, hivyo ndugu yao atatoka.

Siku ya hukumu, Hakimu alimfunga Ramso miaka 45 jela, baada ya hapo july akatumbua zile hela zikaisha akaendelea na kazi yake, safari hii akaenda na SHAIBU KALUWA kuiba computer peramiho mission. wakakamatwa wakawekwa selo za polisi pale central songea. Sasa kivumbi kikawa inabidi July na Shaibu wapelekwe pale magereza kusubiri kesi yao kwa kuwa kule central hawaweki watuhumiwa muda mrefu. July akamwomba mkuu wa kituo asimpeleke kule magereza yupo Ramso atamuua. Kilichofanyika ni kusubiri mpaka Ramso ahamishwe gereza ndio july apelekwe gerezani. Sijui ni nani aliye-coordinate hiyo move lakini mwisho wa siku Ramso alihamishiwa gereza la Ukonga DSM ndio july akapelekwa pale magereza. Ile kesi ilivyoisha July na Shaibu walifungwa miaka 16 jela, sijui kama huko mbele walikuja kuonana, ila niliongea na Ramso pale Ukonga siku moja akasema alikuwa anategemea rufaa ingemtoa lakini rufaa zake zote mbili zilidunda na siku akikutana na July gerezani ndio itakuwa mwisho wa maisha yake lazima mmoja kati yao afe.

when close friends turn enemies, the relation is deadly, refer 2pac and BIG.

Mkuu umenikumbusha mbali sana,,nimekunywa sana soda za Julli wakati nipo mfaranyaki shule ya msingi,,jamaa alikuwa jirani yetu!!pia inasemekana baba yake alikuwa mchawi sana,,
 
Back
Top Bottom