Harakati za UKAWA ,Ahadi ya katiba mpya na Ujio wa Lowassa

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
UKAWA-Umoja Wa Katiba ya Wananchi.

Huu ni mwanvuli wa kisiasa na kijamii ingawa kiutendaji uko kisiasa zaidi na sasa naweza kusema umeshakuwa kisanii zaidi unless nipate ufafanuzi kutoka kwa pro-Ukawa wa sasa.

Tujikumbushe mchakato wa kuipigia kura rasimu ya katiba inayopendekezwa ambayo iliandaliwa upya chini ya anayetajwa kuwa mtuhumiwa wa skendo mbalimbali za ufisadi.

Hapa ndipo tulipoiona nguvu ya kina Tundu lissu na Jussa na hatimaye kukaibuka kikundi hiki ambacho sasa nakivalisha jina rasmi la kikundi cha dunderheads waliokosa fursa.kikundi cha UKAWA kilichogeuka kiwa Ikiwa.

Baada ya kubishana kwa hoja kikundi hiki kilijidai kutoka nje ya mjengo ili tu wasishiriki kile walichokiita najisi yaani kupitisha katiba ya mafisadi.

kabla jogoo halijawika mara ya nne na hata jina wanalolitumia halijasajiliwa unashangaa wakimpokea kwa mbwembwe na bashasha mtu waliyemtwika tuhuma zote mbaya!!na mmoja wa rafiki zake ndio alikuwa mtaalamu(chemical Ally) wa kuchakachua katiba ya jaji warioba.


Swali ninalojiuliza ni moja tu...hivi hiyu aliyepewa kupeperusha bendera ya UKAWA alikuwa na msimamo gani kuhusu katiba pendekezwa???

Katika kura ya kupitisha katiba ya Sitta na Chenge alipigia wapi??

Iweje aaminike kwa kikao cha wiki mbili tena gizani kwamba atasimamia uwepo wa katiba mpya??


Napenda kuwaona waandishi wakongwe na wataalamu wa vyuo vikuu wakiuliza maswali muhimu kama haya na sio kubaki kutuambia jamaa ana watu au ni Tembo!


Cc: nguruvi
 
Last edited by a moderator:
Profesa naamini ulinisoma na kuniekewa mno na umefanya maamuzi sahihi.

Haina mbaya kuanza moja 2015 washaitia najisi.
 
Mtanzania usifanye makosa tena mwaka huu. Usiruhusu GENGE LA KATIBA PENDEKEZWA liingie Ikulu, hiyo katiba ya Sitta na Chenge haifai haifai haifai, mtajuta.

Chagua Lowassa, Chagua Katiba ya Wananchi.
 
lowasa?... katiba ya wananchi? (??)

Lengo la UKAWA ni kutetea rasimu ya pili ya Warioba, iwe ndio Katiba ya Wananchi. Mkiwachagua hao wengine ni dhahiri mtakua mmeruhusu ile KATIBA PENDEKEZWA iwe rasmi sasa.
 
Wananchi inabidi wapewe elimu ya kutosha, kwamba hii ni VITA DHIDI YA KATIBA YAO (LOWASSA) NA ILE KATIBA INAYOSUBIRI KUPITISHWA KIBABE, KATIBA PENDEKEZWA (MAGUFULI).

Huu ndio wakati wao wa kuifurusha hiyo katiba kandamizi (katiba pendekezwa).
 
Ninadhani hufahamu hata unachokiandika na kama unafahamu, utakuwa unapotosha.

Lowassa na Katiba ya Wananchi wapi na wapi?

Vipaumbele vya Lowassa amesema viko vitatu.
1)Elimu
2)Elimu
3)Elimu
 
Nyie majuha someni ilani ya cdm uchaguzi huu kipaumbele cha katiba kimepewa priority sio blah blah
 
Back
Top Bottom