kiria babu
Member
- Sep 13, 2017
- 12
- 8
Ndugu zangu wana Forum wenzangu,
Nimekua nikifuatilia mijadala hapa kumuhusu Mh. Lissu hapa jukwaani, Inisikitisha sana tena sana mijadala ya vijana wetu. wengi wamediriki kuhoji uzalendo wake na kumwita msaliti wa Taifa.
Kinachosikitisha wenye hoja za kusema Lissu ni msaliti hawajawahi kuwa na ushahidi wa usaliti wake. Wakati tunaitisha press conference na kusema tulivofuatilia mawasiliano ya kina Mwanyika na kugundua walikua wakiwasiliana wa wawekezaji, simu za Lissu zimekaa polisi zaidi ya wiki mbili lakini hazijawahi kukutwa na ushahidi wa kumtia hatiani, nyumba yake imesachiwa mara nyingi hatujawahi kumkuta na ushahidi wa aina yoyote, amefuatiliwa kila anapoenda lakini sijawahi kusikia hata siku moja kakutana na mtu ambaye analiibia Taifa.
Lissu hivi sasa ana miaka 49, ina maana kaanza kupigania lasilimali za nchi hii na kupambambana na dola, mabepari akiwa kijana ambaye hajafika hata miaka 30. watu tunamwita msaliti kweli. mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, ipo siku tutamkumbuka.
Lissu kpambana sana huko, migodini kutetea wanyonge, tukianzia kule nyamongo, resolute nzega, buzwagi, ufisadi wa kgoda, kiwira, rada, EPA, iptl, n.k hutaikosa sauti ya Lissu .
1. Je, Wajua Tundu Lissu Aliwatoa Gerezani BURE Wananchi 466 Wa Tarime Waliofungwa Kwa Kupinga Mwekezaji Asiwanyanganye Ardhi Yao?
2. Je, Wajua Tundu Lissu Alishawai Kupigwa Marufuku Asikanyange Nyamongo Kwasababu Ya Harakati Zake Za Kuwatetea Wananchi Dhidi Ya Wawekezaji?
3. Je, Wajua Tundu Lissu Alipambana Na Kaka Yake Alute Lissu Mahakamani Kwenye Kesi Ya Kupinga Ubunge Wa Lema, Alute Akiitetea CCM Na TL CHADEMA?
4. Je, Wajua Tundu Lissu Akiwa JKT Itende Alidhaniwa Kuwa "Usalama Wa Taifa" Kutokana Na Tabia Yake Ya KUHOJI Bila Woga?
5. Je, Wajua Tundu Lissu Alipambana Na Serikali Ya Mkapa ISIUZE Rufiji Delta Kwa Mwekezaji Nolan, Hadi Bank Ya EIB Ikagoma Kutoa Mkopo Kwa Nolan?
6. Je, Wajua Mwaka 2004 Freeman Mbowe Alimuomba Tundu Lissu Ajiunge CHADEMA Baada Ya Kumtetea Chacha Wangwe Kwenye Kesi 10 Za Jinai?
7. Je, Wajua Tundu Lissu Alianza Kushtakiwa Kwa "Uchochezi" Mwaka 2001 Na Mpaka Leo Hajawai Kukutwa Na Hatia?
8. Je, Wajua Kwenye Kampeni 2010 Kikwete Aliwai Kusema Ni Heri Dr.Slaa Awe Rais Kuliko Tundu Lissu Awe Mbunge?
9. Je, Wajua 70% Ya Kesi Anazozisimamia Tundu Lissu Halipwi Chochote Na Watu Anaowatetea, Yeye Hufurahi Akiona Mtu Haonewi Wala Kunyanyaswa?
10. Je, Wajua Tundu Lissu Hutumia Mshahara Wake Wa Mbunge Kusafiri Maeneo Mbalimbali Nchini Kuwatetea Walalahoi BURE Mahakamani?
Sent using Jamii Forums mobile app