Harakati za Ben Saanane kupambana na Rais Magufuli, ni njia sahihi ya kuwaridhisha wafadhili wake?

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Mwanzoni mwa mwaka huu, niliweka taarifa kwenye mitandao ya kijamii hususan hapa Jamiiforums juu ya Mkuu wa Sera na Utafiti CHADEMA, Ben Saanane kununuliwa vitendea kazi kama simu, kompyuta mpakato, ipad, tablets na zana nyingine. Nilieleza kuwa aliyemnunulia vitu hivyo ni Edward Lowasa. Nilitoa sababu za Lowasa kufanya hivyo ni kutaka Mkuu huyo wa Sera na Utafiti afanye kazi ya kumsafisha Lowasa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia amshambulie Rais Magufuli ili tunapoingia 2020, asiaminike tena. Nilieleza kuwa Ben na Lowasa wamekubaliana kuwa malipo ya kazi hiyo ni milioni 4 kwa mwezi.

Kwenye uzi ule, nilieleza bayana kuwa Ben Saanane amepangiwa ofisi ya kufanyia kazi hiyo katika sehemu ambapo sikubainisha kwenye mtandao kutokana na sababu za kimkakati.

Hata hivyo, baada ya uzi ule kuwekwa, Ben Saanane alikosa uvumilivu. Aliishia kuporomosha lugha zilizokosa staha kwa lengo la kushinikiza mods waufute. Alifanikiwa. Uzi ule ukaenda na maji. Leo mdogo wangu Ben namuomba awe mvumilivu ili tujadili kwa staha.

Miezi 5 imepita sasa tangu Ben Saanane anunuliwe. Matunda ya uwekezaji ule yameanza kuonekana. Ben Saanane na genge lake wameanza mashambulizi dhidi ya Rais kwa hoja ambazo kimsingi hazina mashiko.

Ben Saanane na genge lake wameshindwa kabisa kuona udhaifu wa Rais Magufuli kiutendaji na badala yake wanaegemea kwenye mipasho na mapambio. Wanafanya siasa za kuvizia. Niliwahi kuanzisha mada humu kwamba, ikitokea Rais akawa bubu, je CHADEMA watakuwa na ajenda zipi?

Tathmini yangu ya muda mfupi imebaini kwamba, hoja zinazojengwa na Ben Saanane na genge lake zinategemea nini Rais anaongea. Kwa maana utendaji wa Rais uliotukuka unasababisha Ben Saanane na Genge lake wakose hoja za kumkosoa. Hata kama wanapojaribu kukosoa utendaji, wanakosoa kwa hoja dhaifu. Mathalan, ziliponunuliwa ndege mpya mbili aina ya Bombadier Q400, walijenga hoja za kitoto eti ndege hizo hazina mwendo. Mara wanasema ni mapangaboi. Mara wanasema eti water salute haikufanyika kisawasawa. Almradi wanawaonesha wafadhili wao kuwa wametimiza wajibu wao. Utoto.

Uwezo wa vijana wa CHADEMA katika kujenga hoja ni mdogo. Kuna wakati Lusinde aliwahi kuwaambia kuwa akili zao zimeshikiliwa na Mbowe na ndio maana wanawaza kimbowembowe tu.

Hata hivyo, najaribu kuwaza, je kazi anayofanya Ben Saanane na genge lake inatosheleza matakwa ya wafadhili wake? Je watafanikiwa kushusha morali ya Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi? Je watakwamisha juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli katika kutekeleza ilani ya CCM? Thubutu! Rais ameapa kuwa hakuna atakayekwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM. Ben Saanane na Genge lake wataishia kujadili water salute, kuomba Salary Slip ya Rais na kujipongeza kutokana na kauli ya Rais kuwa anatamani malaika afungie mitandao ya kijamii kwa mwaka mmoja ili itakapofunguliwa wakute Tanzania imepaa.

Nimhakikishie Rais wangu kuwa, hawa wapiga kelele mitandaoni hawatafanikiwa kukwamisha harakati zako za kuwaletea maendeleo wananchi. Waache wapige kelele. Wewe piga kazi. Mwisho wa siku kelele zao zitageuka kuwa kicheko kwako. Watanzania tuna imani kubwa kwako. Kazi unayofanya inapokelewa kwa mikono miwili na Watanzania. Utafiti wa Twaweza unabainisha kuwa 96% ya Watanzania wanakulibali. Endelea kupiga kazi ili ifikapo 2020, wapinzani waone aibu kumsimamisha mgombea Urais kupambana na wewe.
 
naona mkulu amekiri kwamba kikosi kazi cha ccm mitandaoni kimegalagazwa chali na cha ukawa....mpaka anatamani kuifuta mitandao,ikifutwa mitandao lizaboni na kundi lake watarudi kijijini mpigamiti wakachome mkaa.

poleni sana akina lizaboni,ajira zenu hatihati,hoja za ukawa zimefika jumba jeupe
 
kinakushangaza nini wakati JK alisema ccm ina kundi la vijana 46 mitandaoni,watu 46,mnapigwa na mtu mmoja,ben saanane
Hehehe vioja hivyo
Mmeishia wapi!!
Kila kukicha matamko yakijingajinga mbona hamjafanya lolote na huyo mropokaji,
Hilo kundi la mitandaoni analijua Lowassa lilivyo mchachavya 2015
Hana hamu
 
Hawa wacha wapige kelele wajipatie hela za bwerere, maana hela za bure bure zimekuwa adimu sana awamu hii. Ila hakuna kitu wata affect. Hii serikali ni mpango wa Mungu sio mpango kando
 
Hawa wacha wapige kelele wajipatie hela za bwerere, maana hela za bure bure zimekuwa adimu sana awamu hii. Ila hakuna kitu wata affect. Hii serikali ni mpango wa Mungu sio mpango kando
Mbaya zaidi ni kwamba, maendeleo yanakuja kwa kasi kuliko speed yao ya kukwamisha. Wanaisoma namba
 
Ile kazi ya Luhwavi na Lukuvi uliyotuelezaga imeisha?
Malizaneni huko kwenu kwanza,halafu ndio muanze kumuwaza Saanane.
Saanane na Malisa G wanawamudu sio tu UVCCM wote,bali CCM yote kabisa.
 
akisemwa Lowassa sawa,akisemwa mkuu kelele kaaaaaaaaaaaaah


Sent from Bombadier Q400 using JamiiForums aeroplane app
 
Ile kazi ya Luhwavi na Lukuvi uliyotuelezaga imeisha?
Malizaneni huko kwenu kwanza,halafu ndio muanze kumuwaza Saanane.
Saanane na Malisa G wanawamudu sio tu UVCCM wote,bali CCM yote kabisa.
Mbele ya Magu kila mtu anatia adabu. Subiri mwisho wake
 
Hivi wale wataalam wao wakuchakachua matokeo walishatoka kifungoni...maana jamaa wanachowaza ni ulongo na uzandiki.....
 
Mkuu, tofauti ya vijana wa CCM na hao mavuvuzela wa CHADEMA ni kwamba, sisi tunajenga hoja, wao wanaattack personalities. Wao hawajasoma, sisi tumeenda shule na ndio maana tunafit kila tunapowekwa
mlioeneza propaganda za uongo dhidi ya lowasa ni nyie,hasa wewe,hata juzi tu ulikuwa unamshambulia lukuvi,najua ameshakutia adabu tayari
 
Si lazima kile unachokiona sawa kwako kiwe sawa kwa mwingine......
 
Back
Top Bottom