Happy New Year 2017

Jun 6, 2016
20
45
Bwana Yesu kristo asifiwe Sana wapendwa katika Bwana.
Ninafuraha kubwa kumshukuru Mungu kwa yote natumaini Mungu mwema ametufikisha leo Trh. 31 tukiwa na pumzi. Wapo wengi tulianza nao lakini wameishia Katikati hawakuweza kumaliza mwaka.
Tukumbuke haikuwa rahisi ila ni rehema na Neema za Mungu kwetu ametushindia kwa ushindi wa ajabu hatuna cha kumlipa zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote.

Haijalishi mwaka 2016 umepitia mangapi magumu na mazito lakini umevuka Salama jua tambua kuwa si nguvu zako ila ni rehema zake Mungu.

Hivyo basi tuungane kwa pamoja siku ya leo kutafakari matendo makuu ya Mungu aliyo tenda mwaka 2016 na pia kumkabidhi mwaka 2017 anze pamoja nasi.
Immanuel Mungu pamoja nasi awa nawe Kwanzia sasa na Hata milele Amen.
Mungu awabariki sana na awape umaliziaji mwema wa masaa Haya machache yaliyo baki na tupokee mwaka Salama.
Katika jina la Yesu kristo Amen.
HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA. View attachment 452424
1483173454385.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom