Happy islamic new year/weka salamu zako hapa

Status
Not open for further replies.

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
May 10, 2012
5,416
4,872
WEKA SALAMU ZAKO ZA KHERI HAPAK:amen:
1391734_433600690077588_106061265_n.jpg
 
Nina furaha kubwaaa kuwa mtu wa kwanza kutoa salaam zangu za mwaka mpya, Happy Islamic New Year to all tanzanian na dunia.
 
Furahia kwa kuomba na kuswali ili Allah s.b.w atuwezeshe kuufikia na mwingine.inshaalah!
ASalaam 3aleykum W W... Shukran Umm.. Naengezea tu, Tuhesabu yaliyopita na turekebishe katika mwaka huu!! Allah atukubalie yetu machache na atusamehe maovu yetu. AMIN
in-ShaAllah Kila mwaka wote mupate Neema za Moula-al-Rahim ....Amin
 
هممم نحن سوف نفعل ذلك من دون أدنى شك
Al-hamdulillah panapo Uhai tutarekebishana na kuUsiana Nasaha njema. Baraka za Mwnyeezi Mungu kwa jamii yote.Amin
in-ShaAllah.. 1435 hejria mwaka wenye Salama na Amani.AMIN
 
kila la heri waislamu wenzangu katika mwaka huu mpya!Allah atujaalie wepesi Inshaallah katika kila lililo na heri nasi
 
Kawaida wanaUchumi/Wafanyabiashara,nk... huwa wanalinganisha mapato yao na hasara zao na matumizi yao katika mwaka (miezi 12) halafu hutoa repoti. Ndugu zangu Waislamu nasi tujiulize na tuweke mezani ya matendo mema tuliyofanikisha kwa mawaka ulopita, na kama kunamapungufu au kasoro tukamilishe mwaka huu. Inshallah uwe MWAKA wa majukumuu ya kutenda Salehatti, kheri, mshikamano na uwe MWAKA wa kukatazana Mabaya na maovu. AMIN
" Na mshikamane pamoja katika kamba Mwenyenzi Mungu, Wala msifarikiane (msitengane) kati yenu ".......Inamaa AlMuuminina Ikhwaa.... Sadaka Allau al-adhim.
Daima Hadhii njema na kwa jamii.
 
Allah atujaze hekima na busara ktk kuzikabili changamoto mbalimbali zihusuzo jamii ya kislamu na watanzania kwa ujumla.
 
Waalaykum Salaam Dada zangu na Kaka zangu katika Uislam,

Tumuombe Allah atujaalie hekma, busara na uvumilivu katika kukabiliana na vitimbi vya ulimwengu na walimwengu.
Na pia atutuzame kwa jicho la rehma kila wakati.
Na atufanye wepesi kwenye kuyaendea mema na wazito kwenye kuyaendea maovu.
Allahuma Aamin.

Kwenu ndugu zetu msiokuwa Waislamu, amani kwenu.
 
Mwenyezi Mungu atupe afya na uzima ili tuendelee kumtumikia mola wetu katika kuyatenda yaliomema na kuacha maovu.
Mwenyezi Mungu awape nafuu waislamu wote duniani kwote wanaoteseka na madhila mbalimbali kutoka kwa makafiri na wanafiki miongoni mwa waislamu. Mwenyezi Mungu awape nafuu waislamu wa Pakistani waliokatika mikono ya dhalimu Amerika, awape faraja waislamu wanaoteseka na dhulma za mayahudi kule Israel, Mwenyezi Mungu awape faraja waislamu waKashmir wanaochomwa moto na baniani kisa kumuamini Mungu mmoja tu, mwenyezi Mungu awape nafuu na faraja waislamu wanaoteseka kwa dhulma za makafiri kule Iraq, Libya, parestina. Mwenyezi Mungu awape nafuu waislamu kwote duniani na hapa kwetu Tanzania.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom