Happy Christmas and Happy New Year | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Happy Christmas and Happy New Year

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Dec 28, 2009.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  ''Sasa,uko tayari kufanya mtihani ili tuweze kufahamu kiwango cha vipaji vyako? Tunataka tukuchukue katika matembezi katika astral,na katika dunia chini ya astral,tunataka tukupitishe kama ghost katika Potala yetu.

  Nilimtazama kwa mshangao. Nitembee?Walidhani ningeweza kutembea vipi?Niliweza kuchechemea katika corridor,lakini miguu yangu ilikuwa haijapona kuniwezesha kutemembea na imani ya aina yoyote.
  Nilisita,nikafikiria kwa muda,halafu nikavuta pindo la joho langu. Halafu nikajibu,''Waheshimiwa Wakuu! Mimi niko sana katika uweza wenu,lakini ni lazima niseme kwamba siwezi kutembea sana kwa sababu ya ajali zangu;lakini,kama mtawa mzuri,najiweka ili niwatumikie na kutegemea kwamba Kiongozi wangu,Lama Mingyar Dondup ataafiki uamuzi wangu'' Hakuna aliyecheka,au hata kutabasamu,kwa ajili ya haya maneno ambayo yalikuwa ni ya kujigamba,kwa vile nilikuwa kijana na sina uzoefu,na nilikuwa tu najitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu,na mtu anaweza vipi kujitahidi zaidi ya uwezo wake. ''Lobsang,tunataka ulale chali,ni lazima ulale chali kwa sababu miguu yako haiwezi kuruhusu kukaa katika nafasi ya kawaida. Kwa hiyo lazima ulale chali'' Yule Lama mzee kwa uangalifu alichukua mto wa kukalia na kuuweka chini ya kichwa changu,halafu akaiweka mikono yangu na vidole vimeingiliana,ili mikono yangu iwe kati ya mfupa wa mbavu na kitovu. Halafu wakajipanga upya;wakaiweka crystal upande mmoja,wakaiweka kwa heshima sehemu ambayo nilikuwa sijaiona bado, chini ya Sanamu Takatifu. Walikaa kunizunguka na kichwa changu kilikuwa katikati kabisa ya mduara. Mmoja wa Lama aliondoka kutoka kwenye kundi halafu akarudi na vijiti vya udi na chelezo ndogo. Karibu nijiaibishe kwa kupiga chafya moshi wa udi ulpipopita katika uayangu na kuifanya iwashe.

  Ajabu,macho yangu yalianza kuwa mazito. Nilihisi mwili unaanza kuwa mchovu,lakini lama walikuwa hawanitazami mimi,walikuwa wanatazama sehemu juu yangu,juu kabisa. Niliyalazimisha macho yangu kufunguka,na niliweza kuona chini ya videvu vyao,niliweza kuona ndani ya pua zao,vichwa vyao vilikuwa vimegeuzwa kiasi kwamba sikuweza kuyaona macho yao. Hapana,walikuwa hawanitazami mimi,walikuwa wanatazama -Wapi?

  Udi uakendelea kuwaka na kufanya sauti ya kuchemka ambayo nilikuwa sijaisikia kwanza. Ghafla nikajishikilia na mikono yangu kwa nguvu zaidi kwa sababu ilikuwa inaelekea jengo lote lilikuwa linatingishika. Nilikuwa nimesikia kuhusu matetemeko ya ardhi na nilidhani kwamba sisi hapa katika Potala tulikuwa tumekumbwa na tetemeko la ardhi. Niliingia woga na kwa juhudi kubwa niliweza kuwa mtulivu,na kufikiria kwamba itakuwa ni aibu kwa Kiongozi wangu kama nikikurupuka na kutoka kwenye hekalu wakati wale lama wamekaa shwari.

  Kutikisika kukaendelea ,na kwa muda mfupi karibu niugue. Kwa muda nikahisi kwamba nilikuwa nakwenda juu,niliona kwamba moja ya boriti katika paa ilikuwa nchi chache kutoka kwenye mkono wangu. Nikanyoosha mkono kujikinga,na nilistuka kuona kwamba mkono wangu ulipenyeza katika boriti bila hata kuzitimua vumbi zilizokuwepo juu yake.

  Baada ya kustushwa na hilo tukio,nilizama chini upesi na kutua kwa miguu yangu kando ya Sanamu Takatifu. Upesi nikanyoosha mkono kujiegemeza,kwa kufahamu kwamba miguu yangu haiwezi kunibeba vyema. Lakini tena,mkono wangu ukapenyeza katika ile Sanamu Takatifu,na miguu yangu ilikuwa imara na yenye nguvu,nilikuwa sina maumivu,sina usumbufu. Nikageuka upesi-kundi la lama lilikuwepo pale bado. Lakini,hapana! Mmoja alikuwa hayupo. Alikuwepo,niliona,amesimama kando yangu na mkono wake ulikuwa umekaribia kugusa kiiko changu. Alionekana anaang'ara,alionekana kuwa mkubwa kidogo kuliko wengine,na nilipoitazama ile Sanamu Takatifu niliona kwamba mimi, pia,nilikuwa mkubwa kuliko hali yangu ya kawaida. Tena,fundo kubwa la woga likuwa lipo ndani mwangu na tumbo langu lilisokota kwa woga. Lakini yule lama alinigusa katika kiiko,na kunipa moyo,''Ni sawa,Lobsang;hakuna kitu cha wewe kuhofu.'' Aliongoza njia na mkono wake kwenye kiiko changu cha kulia. Kwa uangalifu tukawazunguka wale lama ambao walikuwa wamekaa katika mduara. Nilitazama,na-nikatazama katikati ya mduara,lakini mwili wangu haukuwepo pale,kulikuwa hakuna kitu pale. Ili kuhakikisha nilinyoosha mkono wangu[surreptitiously,kwa siri ili asijue nia yangu] na kumgusa yule lama pembeni mwangu,na yeye alikuwa imara pia. Aliona nilivyofanya na kuckeka na kucheka. ''Lobsang!Lobsang! Sasa uko katika hali nyingine kabisa na mwili wako. Wale tu wenye uwezo mkubwa wa kiroho,uwezo wa kuzaliwa nao,wanaweza kufanya kitu kama hiki. Lakiini,njoo pamoja na mimi''


  Tulitembea na kwenda pembeni mwa hekalu,na ukuta ukaja karibu na karibu. Nikajichomoa kutokana na mshiko wake na kujaribu kugueuka upande,na kusema,''Hapana,Tutajiumiza tusiposimama. Huu ukuta haupitiki!'' Lama akanishikilia kwa nguvu zaidi,na kuamrisha,''Njoo!Ukiwa na uzoefu zaidi utajuwa hii ni rahisi kiasi gani!''Akaenda nyuma yangu na akauweka mkono wake mgongoni mwangu na kunisukuma. Ukuta ukaniijia,ukuta wa jiwe la majivu. Akasukuma,na nikajisikia vizuri kiasi ambavyo sijasikia maisha yanguyote,ilikuwa kama mwili wangu wote unatekenywa. Ilikuwa kama vile mamilioni -mabilioni - ya mapovu yalikuwa yanajigonga kwangu,hayanizuii,yananitekenya tu,yananifanya niwashwe mwasho mzuri. Nilikuwa nakwenda mbele bila taabu yoyote,nilivyotazama,nilihisi kama vile naenda katika dhoruba ya vumbi,lakini vumbi ilikuwa haidhuru macho yangu hata kidogo,na nikanyoosha mikono yangu kutaka kuishika hiyo vumbi. Lakini ilinipenyeza au mimi niliipenyeza,sijui ipi ni sahihi. Yule lama nyuma yangu alicheka na kunisukuma kwa nguvu zaidi,na nikapenyeza katika ukuta na kutokea upande wa pili. Mzee mmoja alikuwa anakuja katika corridor ameshilkiia karabai katika kila mkono,na ameshika kitu alichokibana kati ya kiiko chake cha kushoto na mwili wake. Nilijaribu kujizuia kumgusa,lakini nilikuwa nimechelewa. Nilitayarisha kuomba msamaha;lakini yeye alitembea na kunipenyeza,au mimi nilitembea kumpenyeza,na hakuna yeyote kati yetu aliyejua tumegusana,hakuna aliyejua kwamba tumetembea na kumpenyeza binadamu mwingine.


  Huku yule lama ananiongoza,tuliendelea kupita katika jengo,bila kuingila shughuli za faragha za watu waliokuwa peke yao katika vyumba,badala yake tukatembelea ghala na-kama kwa mzaha wa yule lama aliyekuwa ananifahamu sana-tukatembelea jiko!

  Yule mzee lama mpishi alikuwa pale amepumzika ameliegemea kasha kubwa la ngozi limejaa barley. Alikuwa anajikuna na kutoa uchafu kutoka kwenye meno na kipande cha jani kutoka seheme fulani;kila baada ya muda aligeuka na kutema pembeni halafu kurudia tena kujikuna kwake na kusafisha meno. Hatimaye,tulivyosimama tunamtazama,aligeuka,na kutoa sauti kubwa,na kusema,''Ai! Ai!;Muda tena wa kutayarisha chakula,nadhani. Oh! Maisha gani haya;tsampa,tsampa,na tsampa zaidi,watu wote hawa wenye njaa kuwajaza.''


  Tukazidi kutembea katika jengo. Miguu yangu haikunisumbua hata kidogo,ilivyokuwa,kwa kweli,sikuifikiria kabisa miguu yangu,kwa sababu kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kufanya hivyo-haikunisumbua. Tulikuwa waangalifu,waangalifu,tusimwingile mtu katika mambo yake ya faragha. Tuliligeuka katikka njia za ukumbi kwa kadiri tulivyoweza ili tusiingilie sehemu anayoishi mtu binafsi. Tulikwenda chini kabisa katika ghala. Nje alikuwepo rafiki yangu Mheshimiwa Paka,amejilaza,huku akitingishika kidogo. Masharubu yake yalikuwa yanacheza cheza na masikio yake yalikuwa yamegandana kwenye kichwa chake. Tulikuwa tunasogea kimya,tulidhani,lakini ghafla akaamka na kuwa macho kabisa na akaruka katika miguu yake na kutoa meno. Lakini baadaye macho yake yakageuka na akatazama katika ngazi ya astral[ambavyo paka wote wanaweza]na akanza kufurahi aliponiona mimi. Nilijaribu kumgusa lakini mkono wangu ukampenyeza,jambo la kushangaza sana,kwa vile mara nyingi niliwahi kumgusa,na hakuna hata mara moja mkono wangu ulipenyeza. Alionekana kufurahi kwa kiasi kile kile ambacho mimi nilistushwa,lakini akanigonga mimi,lakini mkono wake ukanipitia mimi ambalo ilimshangza,halafu akaliondoa jambo lote katika akili yake,akajilaza,na akarudi kulala tena

  Kwa muda mrefu tulitembea katika hizo kuta,tukipanda katika ghorofa,hatimaye yule lama akasema''Chini tena,twende chini,kwa sababu tumetembea kiasi cha kutosha sasa hivi,'' Akauchukua mkono wangu,na tukazama chini kupenyeza sakafu,na tukatokea katika dari ya chini,halafu kupita sakafu nyingine mpaka tukafika katika hekalu lilipokuwa. Kwa mara nyingine tena tukausogelea ukuta,lakini safari hii sikusita,nilitemeba na kupita,na kufurahia hisia ya yale mapovu na kutekenywa. Mule ndani wale lama walikuwa bado wamekaa katika mduara wao,na lama wangu-yule aliyekuwa anaushikilia mkono wangu-aliniambia nilale sehemu niliyokuwepo kwanza. Nilifanya hivyo,na usingizi uakaniijia mara moja
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  .... hadithi njoo utamu kolea!!
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  aaaaaaaghhh summary please
   
Loading...