Happy birthday!

Happy birthday!

mcndomba maprosoo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2013
Posts
225
Reaction score
94
Tunaomba mwenyezi Mungu aweze kukulinda na kukufanikisha katika maisha yako yote, “ukiendelea vema katika hekima, na kimo, ukimpendeza Mungu na wanadamu”,kama alivyokuwa mtoto Yesu (Lk 2:52). Ili Mungu mwenyewe aweze kuwapiga na kuwadhuru adui watakao inuka mbele zako na kuiamuru baraka ije juu yako (Kumb 28:7-8).

Basi Mungu mwenyezi, “akubarikie na kukulinda; akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; akuinulie uso wake, na kukupa amani” (Hes 6:24-26).

Hata hivyo katika wakati wote tumefarijika sana na huduma yako kwani, wakati mwingine umekuwa kama mwl & mshauri ukiungana na Mfalme Daudi pale aliposema, “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama” (zab 32:8).

Wakati mwingine umekuwa kama Mchungaji ukiungana na nabii Yeremia kwamba, “Nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakao walisha kwa maarifa na fahamu” (Yer 3:15).

Kuna wakati pia umekuwa kama mwana falsafa aliyekuwepo kabla ya Kristo lakini anayeishi leo ukifananishwa na Socrates aliyeamini kuwa, “ a teacher should not besiege students with a barrage of words but instead help people to discover and articulate their own hidden knowledge” (Socrates: 469-399 B.C.E)

"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yako yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo", (3Yoh 1:2)
Happy birthday..! & Stay blessed:;
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom