Nakushukuru Mungu kwa kuniongezea mwaka mwingine maishani mwangu, najua sikustahili kabisa ila kwa neema yako tu, kipekee nakushukuru kwa kuniwezesha kutimiza malengo yangu yote niliyojipangia kwa mwaka huu mpaka kufikia tarehe ya leo, naomba nijalie mwaka mwingine wa baraka na kufunguliwa, najua ushapanga ila naomba kwako nikiamini u mwingi wa rehema, wala si kama nitakavyo mimi ila mapenzi yako yatimizwe. Amin.