Amani kwenu wadau
Juzi kati ilikua ni kumbu kumbu ya siku ya kuzaliwa mamsapu,sasa kulingana hali ya maisha ni ngumu ,na yeye kulipokucha aliniambia baba timdwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa nataka unifanyie kijisherehe nifurahi na shoga zangu ,imekua mimi nakwenda kwa wenzangu kila mara lakini kwangu hakuna,
Ok mimi sikubisha kiume nikaenda kwenye mizunguuko yangu nikanunua keki na vitu vingine vitafunwa nikanunua kreti kama mbili za soda nikarudi navyo nyumbani,nikakuta familia yote wameunganika nikatuma mwanangu ashushe vile vitu avilete ndani,mamsapu akauliza vitu hivi ni vya hiyo sherehe.. nikamjibu ndio,ukumbi wapi ..aah nikamwambia ukumbi, mbona nyumba yetu inatosha tu,..akauliza na hao shosti zangu..mimi nikajibu shosti zako si hawa wanao wanatosha mpaka ubebe watu wakati mambo sio freshi,
Baada ya hapo bibie akaingia ndani kanuna kalala hataki mazungumzo,na hata tendo la ndoa pia nisimguse yaani tafrani na inashangaza utamaduni huo alikua hana miaka nenda,hili la kunyimwa haki kisa tu birhtday pananitatiza
Sasa jamani naona giza nisaidieni mawazo kidogo tu!