Happy Birthday Baba Askofu Mwamakula

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
141,361
Reaction score
283,424


Leo hii ni siku ambayo tunakumbuka Kuzaliwa kwa Mpigania Haki muhimu wa Tanzania Askofu Emmaus Mwamakula , ambaye wapenda haki wengi wanamuita Desmond Tutu , huku wengine wakimuita Malcom X .

Mwamakula ni Miongoni mwa Viongozi wachache sana wa dini wa kiafrica walioamua kusimama na wananchi katika kupigania haki , hakuwahi kuogopa mikwara ya Watawala wala hakuwahi kuogopa kukamatwa , hakujali hata alipodhalilishwa na Lazaro Mambosasa , bali yeye alisimama na wananchi na kiukweli bado yuko na wananchi wakati huu tukielekea kwenye kupata Katiba mpya.

Si rahisi kuelezea umuhimu wa Askofu huyu kwa nchi hii , Lakini kwa ufupi naomba kumtakia Baba Askofu huyu Maisha marefu , Amina .
 
Bandikule ni aina ya ulanzi

USSR
 
Huyu mwehu nae ni Kiongozi wa Dini? Hivi WALOKOLE hamnaga akili kiasi hiki?
 
Happy birthday Askofu wangu Mungu akuzidishie siha njema na umri mrefu, ili ushuhudie Tanzania mpya itakayotoa HAKI kwa watu wake. Tanzania isiyoongozwa na wezi wa mali za umma.

Tanzania yenye Katiba bora na mpya,Tanzania yenye tume HURU ya Uchaguzi, Tanzania ambayo itaongozwa kwa Kura moja mtu mmoja,

Tanzania itakayokuwa na Taasisi imara zinazojiendesha kwa kufuata katiba na sheria na sio matakwa ya wanasiasa.
 
Amen
 
Acheni kumfananisha Malkolm X na vitu vya ajabu
 

Ila we jamaa mnafiki sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…