Happiness starts within you

Happiness starts within you

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,688
Habari za saa hizi marafiki,

Leo tuongelee kuhusu jinsi ya kujipenda na kuwa na furaha bila kutegemea watu wengine.

Ukiwa unajitegemea kifikra ndio mwanzo wa kujitambua na kutambua mahitaji na matarjio yako kutoka kwa watu wengine.Nikisema kujitambua namaanisha kujua nini kinachokufanya uwe nafuraha,kinachokukera na kukubughudhi,majonzi yako,malengo yako,mahitaji yako na matarajio yako.

Jaribu kutoka kwenye lile eneo ambalo upo comfortable na kumiliki fikra zako,kutimiza ndoto zako na kupigana kufikia malengo yako.

Usikubali kuburzwa kifikra na mtu mwengine usifanye kitu kwasababu fulani amefanya,fanya kitu kwasababu wewe umetaka kufanya hivo,wewe ndio muamuzi wa furaha yako,si kosa kuwa mbinafsi kwa minajili ya furaha yako."Timiza ndoto zako na simamia zile zinazokufanya wewe kuwa wewe"

Ishi kwa kujifunza vitu vipya kuhusu wewe na jifunze vilevile kutoka kwa wengine,furahia maisha na jenga uelewa wa kuwa unataka kuwa mtu wa aina gani na ujipende.Furaha ni jambo kubwa na fikra zako ndio zinazoamua na kutawala hilo.

Tatizo linalowakabili wengi ni kwamba tunafikiria sana yanayojiri sasa na si ya malengo yetu ya baadae.Ni vyema kufurahia maisha ya sasa na vilevile kujijenga kifikra kwa baadae.Mabadiliko yanaanza na wewe.Pigania kwaajili ya vitu vinavyokupa ubora vinavyokupa inspiration ya kuwa mtu unayetaraji kuwa.

Hakuna aliyekamilika lakini kuna mstari mwembamba kati ya kuukubali ukweli na kuishi maisha ya kufikirika yanayotupa furaha ya muda mfupi.Usiishi kwa majuto bali kupitia kwenye makosa yako na somo ulolipata kupitia hapo.

Kitu kimoja nimejifunza ni kwamba ni kawaida kuvutiwa na watu wanaofanana na wewe.Kama wewe umevurugwa,utavutiwa na walovurugwa,kama ni mtu bora utavutiwa na watu bora.Jipe nafasi ya improvement na utaona mabadiliko.Jenga ukaribu na watu ambao wanajitambua kifikra,watakuinspire wewe kuwa mtu bora.

Jipende na utambue thamani yako."Happiness starts within you"

Wasalaam gorgeousmimi
 
True dat..maneno yako ni darasa tosha..watu uwa wanatoa elimu kama hizi kwa malipo..we sijui mashetani yako hayapendi pesa lol...nyc words sisy..kip it up
 
Aya ya mwisho nimeielewa zaidi, niliwahi kusoma mahali 'you can tell your future by looking at the 5 people you hang-out the most with', naweza kuoanisha.

On another note, wish you could show me the blue-print they made you with, coz i gotta make me one like you. Stay blessed.
 
True dat..maneno yako ni darasa tosha..watu uwa wanatoa elimu kama hizi kwa malipo..we sijui mashetani yako hayapendi pesa lol...nyc words sisy..kip it up

hahahaa hapo kwenye red .....hivi hauamini kama kuna wanawake hawana utumwa wa pesa....? kama ukiwa mpenda pesa unakuwa mtumwa...unafanyishwa vitu ambavyo hata mnyama hawezi fanya ila sababu unapenda pesa unavumilia tu....sasa ukishajitambua katika hili....mashetani ya pesa hayawezi kukupanda kamwe......
 
my sisy huu ndo ukweli mara nyingi ndege wanaofanana huruka pamoja

ukiona mpole yuko na waruwaru na wanaelewana bas huyo mpole anapenda mambo hzo sema alikua hajapata wa kumjanjarusha

siku zote mwenye akili na mwenye akili mwenzie
zero brain na zero brain mwenzie

automatically unajikuta nature inaselekt.

so usemavyo ni sahihi na hakuna kitu kibaya km nidhamu ya woga
au upretender kujifanya saint ili ufurahishe watu while wewe ni mcharuko.com
 
hahahaa hapo kwenye red .....hivi hauamini kama kuna wanawake hawana utumwa wa pesa....? kama ukiwa mpenda pesa unakuwa mtumwa...unafanyishwa vitu ambavyo hata mnyama hawezi fanya ila sababu unapenda pesa unavumilia tu....sasa ukishajitambua katika hili....mashetani ya pesa hayawezi kukupanda kamwe......
wapo..japo wachache..huyu namtania tu..najua hana itikadi hizo..niliwahi kumshawishi tutengeneze kitabu tupige pesa akagoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom