Hapo sasa!!

Mwanangu Saudari hii kitu imenifurahisha. Sijui ni kwa sababu ya uzee au ukale lakini nimependa jinsi walivyovaa hawa wanamuziki. Je ni bendi gani na ya wapi? Lait wangemechisha hata viatu vyake!
 
Jamani swaga hizo...mwanaume mzima unamechi pink na yellow, damn
 
Saafi sana...hapa ni kitu inaitwa DISKO LA YESU....yaani raha tupu...
 
Tupe maujanja ya Colour coding wengine to 'shallow' kwenye maswala haya

Huna GF wewe au mke....mambo ya color coding au color blocking yanataka ufundi kwenye formal suit kama hii, kwanza hizi rangi hapo juu sijui nyekundu sijui ni fuschia for me haiendi na suit hasa hiyo ya njano too flashy, kama wewe mweusi please avoid labda iwe mustard yellow. Kwanza jua rangi yako na rangi zipi zinaendana nazo usifate mkumbo wa fashion au kwasababu John kavaa, maumbile yenu, rangi zenu kama ni tofauti itawapa muonekano tofauti.

kama ni theme, jaribu kuifanya hiyo rangi isitawale mavazi, I call diluting color, umeona huyo wa mwanzo alivyoivaa, kama wangevaa wote kama huyo wa mwanzo ingekuwa tofauti, ile njano haikuonekana sana. Kwangu mie naona ni bora kuliko wengine.

Kama ni casual wear, rangi nyingi unaweza kuzichanganya zikapendeza, lakini ogopa rangi za kituko, orange, flash pink, flashy yellow, usiache ikawa dominating color. Umenifahamu CHUAKACHARA ?

Kama wewe ni mwanamuziki au muimba kwaya endelea tu.....you're on right track:glasses-nerdy:
 

Nashukuru sana kwa shule. Inaelekea wewe ni mtaalamu wa rangi na mavazi-mitindo. Anyway, mimi kidogo yamenipita kando. GF sina ila nina mke huwa sifuatilii sana nguo nguo nguo na rangi zake. Ila ninachujua ni kuwa rangi isiwe conspicuous mwilini say ukuiwa kanisani kila mmoja ana note your presence kama say unakwenda kutoa sadaka/kupokea!!!! Nashukuru sana, ingawa colour concepts have to be taught ostensibly- by seeing. Huwezi kumwelezea kipofu ambaye amepata muujiza wa kuona leo tangu azaliwe (akitoka kwa Mzee wa upako!!!) akai-perceive ilivyo. Nitakutafuta unionyeshe hizo rangi. Usiogope nimeoa na watoto watatu-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…