Hapa Waziri wa Sheria sijakuelewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa Waziri wa Sheria sijakuelewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Averos, May 30, 2011.

 1. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Katika hali ya kushangaza Waziri wa Sheria Mh: Kombani amesema kuwa ili tume ya kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba iweze kufanya kazi vizuri inatakiwa isiundwe na wata wenye mitazamo tofauti ya kisiasa wala wasiwe na ilani (manifestos) tofauti.

  Wanatakiwa wawe na Muono mmoja tu wa mambo, hayo aliyazungumza akiwa katika kongamano la katiba huko Ruaha.

  Hoja katika hili, je tukisema tuwaachie watu wa fikra moja kufanya hiyo kazi mwisho wa siku itakuwaje? Hivi ni kweli kuwa watu wenye muono tofauti wa mambo hawawezi kufanya jambo moja likawa kwa masilahi ya watanzania?

  Hivi ni kweli ndani ya CCM au CHADEMA au CUF wote wana mawazo sawa na wanauwezo sawa wa kufikiri mambo?

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Bila peoples power sidhani kama CC watakubali kuwe na katiba mpya wala haikuwa ajenda yao ktk ilani yao.

  Na hawatakubali eti kuwe na tume huru ya uchaguzi, rais apunguziwe madaraka, nk nk wao wanawaza tu kushinda.

  Uchaguzi hata vikao vyao vyote wanajadili kushinda uchaguzi na sii kumletea maendeleo mtanzania.
  Wenzetu nchi nyingine wana pigania kuongoza ili kuletta maendeleo na wakishindwa kuleta maendeleo wanaachia, madaraka hilo kwa bongo hakuna.

  Tunisia na Misri wamefungua njia, Yemen na Siria wamekubali kuyatoa maisha yao
  sadaka wamechoka kuonewa, wamechoka kunyonywa.

  Kwa tanzania bado somo hili halijawaingia watawala wetu wanadhani watatawala milele.
   
Loading...