Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,940
Neno hili ni maarufu sana kwa wakristo na waislamu. Inasemekana watu waovu watateswa kwa moto milele na milele. wasichojua wengi ni kuwa jehannam ni sehemu halisi huko Jerusalem.
neno jehannam limetokana na neno la kigiriki Gehena ambalo nalo ni kutoka kihebrania gehinnom. ambalo inamaanisha bonde la wana wa hinnom (Gai Ben-hinnom). hili ni bonde lililopatikana nje ya ya mji wa Jerusalem.
zamani waisraeli waliomuasi Mungu walikuwa wakichoma watoto wao moto kwenye hilo bonde kama ibada kwa mungu Moleki. mfalme Yosia aliikomesha. 2 wafalme 23:10.
10 Mfalme Yosia pia alipatia najisi mahali pa kuabudia miungu ya uongo palipoitwa Tofethi katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu yeyote asimchome mwanawe au bintiye kuwa tambiko kwa Moleki.
inasemekana alilinajisi kwa kupageuza kuwa sehemu ya kuchoma moto takataka za jiji la Jerusalem na kutupa/kuchoma moto wahalifu. hapo ndiyo watu wakapata wazo kuwa watu waovu watachomwa moto milele Jehannam. Yeremia 7:32-33
32 Basi angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo halitaitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu bali litaitwa, Bonde la Machinjo; maana watazika watu katika Tofethi, hata hapatakuwapo mahali pa kuzika tena.
33 Na mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi; wala hapana mtu atakayewafukuza.
siku hizi jehannam ni mahali pazuri pakupendeza na hakuna moto wa kuwatesa watu milele.