Hapa kweli kuna mapenzi/ndoa?!

Huu ujumbe umenigusa sana, nashukuru mno dada angu kwa kushare nami juu ya hili, ubarikiwe sana!
 
Mkuu kabla ya wakwe kuambiwa, ulimuelewesha kuwa italazimu kureview tarehe ya harusi?
Au kwa lugha nyingine ni wakati gani yeye alijua hayo maamuzi ya kureview tarehe?
 
Mkuu kabla ya wakwe kuambiwa, ulimuelewesha kuwa italazimu kureview tarehe ya harusi?
Au kwa lugha nyingine ni wakati gani yeye alijua hayo maamuzi ya kureview tarehe?
Kabla ya wakwe kupewa taarifa, nilimtaarifu huyu mwenzangu na kumueleza sababu, ofcourse ilikuwa ni lazima mimi nimweleze yeye kama mpenzi wangu, taarifa kwenda kwa wakwe halikuwa ni jukumu langu, hilo lilibaki kuwa ni jukumu la mshenga!
Nilipomjuza tu, response yake ikawa "kwanini sasa mlitaja tarehe ya harusi huku mkijua mtakuja kuibadili............"
Kwenye uzi wangu wa msingi, nililigusia hili!
 
Duuuh ngoja tuitazame kwa upande mwingine! Labda anakupa pressure kutest how much you need her, unajua mapenzi ya muda mrefu kama yenu mnakuwa mmeshakutana na changamoto nyingi saaana, ups and downs, wakati mwingine mpaka upendo kupoa(au kuhisi umepoa) kwa sisi wadada mara kadhaa huwa tunadhani sasa huyu mtu kwa vile kashanizoea saanaa ananichukulia poa, au kanichoka ndio maana hanipi priority fulani , mimi nikushauri kabla ukate tamaa for good( kumbuka umesema ni bint aliyetimiza vigezo vyako) kwa mara ya mwisho mkalishe chini mwache ajieleze vizuri sababu zake don’t pressure her during this, wewe wamfahamu vyema majibu yake kama yatakuridhisha you must try to work on it together
Mithali 13:12
Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua.
Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.

 
Mkuu pole kwa hizo changamoto, mtu mwenye majibu sahihi ya swali lako atabakia kuwa wewe mwenyewe.
Umedumu kwenye mahusiano zaidi ya miaka mitano, kuna kitu kiliwawezesha kukaa kwa muda wote huu.
Pia kumbuka kuwa kwa wadada, kuna muda ambao pressure ya kuwa ndani ya ndoa inakua kubwa zaidi. Kwa maelezo yako ni wazi kuwa huyo atakua kati ya 25-29. Na saa nyingine pressure inaweza kumfanya mtu afanye au aseme kitu ambacho sio sahihi kwa wakati.
Angali ni rahisi kwa familia yako kuelewa sababu yako ila ujue kwa familia ya mwenzio sio rahisi kihivyo kukuelewa hata kama wamesema wameelewa. Na ukumbuke huyo binti anaishi na ndugu zake na sio ndugu zako hivyo katika siku kuna uwezekano mawazo anayopokea kuhusiana na uamuzi huo mengi yakawa hasi.
Mawasiliano ni kitu muhimu kama utashindwa kuingia kichwani mwake na kumfanya aelewe mawazo yako. Ujue kabisa yeye sio mtu sahihi kwako na wewe sio mtu sahihi kwake
 
Ukimjali msichana kwa kila kitu alafu ukampa uhuru ukawa haumbani bani, anaamua kila anachojisikia yeye akiamini huwezi pinga maamuzi yake na huku ilihali wewe unaona jambo unalofanya lina manufaa kwa wote wawili badae, pigania penzi lako huenda shetani kamuingia hivo wewe usimuache nenda kwao siku ukiwa free waelezee wazee wake ukweli mpaka mwez wa6 mwaka2020 utaona uelekeo sahihi wa huyo mwenza wako then utanipa mrejesho.
NOTE:Mwanaume hazeeki hadi anaingia kaburini...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii imenipa comfort sana, shukrani mno!
 
Hii imenipa comfort sana, shukrani mno!
Yeah, sisi wanawake huwa tunafanya maamuzi kulingana na hisia zaidi, so makosa yetu mengi yanatokana na kutawaliwa zaidi na hisia( hisia zinatuchukua tunasahau kabisa vitu logic) na nyie wanaume ni mko kilogic zaidi kuliko kubebwa tu na hisia. So huwa tunakosea wakati wa kutoa ushauri tunasahau kabisa utofauti wetu wa kufikiri, kureason mambo na kuyafanyia maamuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…