Hapa kweli kuna kesi???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa kweli kuna kesi????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Jan 7, 2011.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kesi ya Mpesya dhidi ya `Sugu` kusikilizwa Januari 19


  Wanasheria naomba mtusaidie, maana kwa hoja hizo tatu na eti ndiyo kuu kuna kesi hapa????


  [​IMG]
  Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM, Benson Mpesya, dhidi ya Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ Januari 19 mwaka huu.

  Katika kesi hiyo, Mpesya analamikia mambo makuu matatu ambayo anaona yalimfanya ashindwe na Mbilinyi katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka jana.

  Katika uchaguzi huo, Mpesya ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo alibwagwa na mgombea wa Chadema, Mbilinyi, ambaye alipata kura 46,411 huku mgombea huyo wa CCM akipata a kura 24,236, hatua iliyomfanya aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo, Dk.Samweli Lazaro, kumtangaza Mbilinyi kuwa ndiye mshindi.

  Mpesya katika kesi yake hiyo ambayo hata hivyo bado haijapangiwa jaji wa kuisikiliza,

  1. anadai kuwa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Monica Saile, ambaye wakati wa uchaguzi alikuwa msimamizi wa uchaguzi, alikuwa na maslahi na Chadema kutokana na kuwa miongoni mwa wanachama wa chama hicho cha upinzani waliopendekezwa kugombea ubunge wa viti maalum.


  2. Madai mengine aliyoyatoa Mpesya katika kesi hiyo ni kwamba, wakati wa mchakato wa kampeni, Mbilinyi, alikuwa akitoa maelezo ya uongo kwamba yeye (Mpesya) amejenga shule ya sekondari mkoani Dodoma, hali iliyowafanya wananchi wamuelewe vibaya na hivyo wakashindwa kumchagua.

  3. Sababu ya tatu iliyotolewa na Mpesya ni kwamba Mbunge wa Chadema, wakati wa kampeni alikuwa akieleza maneno ya uongo kuwa yeye (Mpesya) amejenga vilabu vya kuuzia pombe za kienyeji hali iliyomchafulia sifa kwa wapiga kura ambao walimuona kuwa si mpenda maendeleo kwani fedha alizozitumia kujenga vilabu hivyo angeziwekeza katika kujenga hospitali na shule.

  Mpesya katika kesi hiyo anatetewa na wakili wa kampuni ya Mkumbe and Company Advocate.
   
 2. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ground ya kwanza ina weight kidogo but the rest are Crap
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Great bwana sugu usiogope sana mamboo ya kawaida huo ni mkwara tu.
   
 4. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kesi ndogo sana hiyo...
  Bwana Mdogo Sambwee Shitambala hata usingizini anaimaliza hiyo kesi, na itatupiliwa mbali...
  Hivi msimamizi wa uchaguzi anateuliwa na CHADEMA?...So whats that got to do with Mr Two?
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hata hiyo ya kwanza naona bado iko weak kwa sababu atatakiwa kuithibitishia mahakama ni namna gani huyo afisa utumishi aliinfluence ushindi, je ni kwa kuiba kura, kukampeni, kuhujumu kura za Mpesya? Na kama hii argument itaonekana kuhold water basi kesi nyingi sana zitaibuliwa kutoka wabunge wa CCM kwaniwakurugenzi wa wilaya ambao ni wasimamizi wa uchaguzi ni wanaCCm and it can be proved.
   
 6. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hata mimi nashangaa...au walimwachia sugu ateue?

  Ukichoka kufikiri bwana, hata maiti inakuwa na nafuu, maana imepumzika imetulia
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hana cha kupoteza anatekeleza agizo la Katibu Mkuu wa CCM kuwa wana CCM wote walioshindwa Ubunge/Udiwano wafungue kesi na CCM italipa gharama za kesi, possibly from DOWANS ICC proceedings
   
 8. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kisiasa kesi ipo,zinaweza kuwa weak arguments ukiziangalia but si za kudharauliwa kwenye nchi amabyo rushwa,mabavu ni moja ya njia za ushindi,hata waliongalia ile ya Liyumba walisema hana Kesi tena akiwa na mwanasheria anayeheshimika kama Magafu.......hakuna haja ya dharau kwenye suala kama hili.........na kwenye hiyo ya kwanza kweli kuna conflict of interest ya huyo msimamizi wa uchaguzi....ila ni kesi inayoshindika.
   
 9. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Mbilinyi, ambaye alipata kura 46,411 huku mgombea huyo wa CCM akipata a kura 24,236

  mtu umeachwa kwa mbali hivi lkn bado tu unang'ang'ania
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni haki yake kikatiba. Mwache ajaribu kwa majaji hawa ambao siku hizi nao wamejaa u-ccm kwa kuwa tu aliyewachagua ni m-ccm labda anaweza kusikilizwa. Lakini kwangu sijaona lolote la maana kwenye malalamiko yake.
   
 11. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Sisi wa huku Mbeya tunajua kuwa Mpesya amesaidia sana ujenzi wa vilabu vya pombe. Huu ni ukweli!
   
 12. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Hata wakitengua wakarudia uchaguzi CCM haiwezi kushinda
   
 13. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ama kweli mfa maji haishi kutapatapa. Huyu kaishiwa akili
   
Loading...