Hapa kikwete katupiga bao!

IsayaMwita huyo muungwana anafanya usanii tu na ni watu kama wewe mnaozugika na tabasamu lake mnafikiri ndio maendeleo!! Huyu muungwana akiwa majukwaani analaani RUSHWA lakini kwa hisia na vitendo vyake anatetea wala rushwa ama sivyo Lowassa, Rostam, Karamagi na Msabaha mpaka sasa wangekuwa lupango. Angalia kwenye chaguzi za CCm, yeye ni mwenyekiti; wagombea wanapeleka ushahidi wa waziri wake anatoa hongo kwenye uchaguzi wa uwT, badala ya kumuadabisha yeye anayetoa hongo tena waziri wa utawala bora ndio kwanza anakwenda kumpigia debe eti msomi; huko ndio kuipiga vita rushwa kweli!! Aaangalieni wasiopenda rushwa wakina Kagame wanavyofanya
 
Last edited:

Bulesi;

Naomba uelewe kuwa hiyo ni jazba iliyoko ndani ya fuadi yako, kwa hali halisi ni watanzania wangapiwaishio vijijini wanaoelewa kuwa Muungwana hapa anacheza kamchezo kachafu?

Bulesi; naomba uelewe tukiendelea kushadadia na kuendelea kupiga kelele 2010 sisi itakula kwetu, ni bora tukaelekeza hisia zetu 2010 na jinsi gani ya kuweza kukipiku CCM, usisahau hapa wenzako hawalali wanaendelea kujisafisha vilivyo.

Bulesi;tuwe makini .
 
Nakubaliana na nawe IsayaMwita, kuwa makini ni lazima kama tunataka kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi ; inatubidi tuwe na mkakati wa kuwaelimisha wenzetu hasa wale waishio vijijini ambao ndio wanateseka sana na matokeo ya ufisadi ya CCM. Unfortunately, CCm ndio inawalenga hao hao inaowatesa, kwa kuwahonga khanga na fulana wakati wa uchaguzi na kuifanya kama hazina yao ya kupata kura za kutawala nchi!! Operasheni kama hii ya SANGARA isiwe nguvu ya soda bali ipambe moto kwa wanachama wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA na CUF katika sehemu ambazo wanajua wanawafuasi wengi huko ndio waanze kujiimalisha kabla ya kwenda kwenye sehemu mpya. Ni muhimu kukaa na kustrategize badala ya kukurupuka na ni vizuri pia kama matayarisho yakaanza sasa badala ya kungoja karibu na uchaguzi!! Chadema na Cuf wasitegemee ruzuku bali wawategemee wanachama wao kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha mobilisation campaign zao.
 
ukilinganisha na uchumi wa mataifa makubwa (mfano marekani)ulivyo mbaya,naona tusianze kumlaumu Jk just give him five more years! we will get there.
 
Nakubaliana na nawe IsayaMwita, kuwa makini ni lazima kama tunataka kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi ; inatubidi tuwe na mkakati wa kuwaelimisha wenzetu hasa wale waishio vijijini ambao ndio wanateseka sana na matokeo ya ufisadi ya CCM. Unfortunately, CCm ndio inawalenga hao hao inaowatesa, kwa kuwahonga khanga na fulana wakati wa uchaguzi na kuifanya kama hazina yao ya kupata kura za kutawala nchi!! Operasheni kama hii ya SANGARA isiwe nguvu ya soda bali ipambe moto kwa wanachama wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA na CUF katika sehemu ambazo wanajua wanawafuasi wengi huko ndio waanze kujiimalisha kabla ya kwenda kwenye sehemu mpya. Ni muhimu kukaa na kustrategize badala ya kukurupuka na ni vizuri pia kama matayarisho yakaanza sasa badala ya kungoja karibu na uchaguzi!! Chadema na Cuf wasitegemee ruzuku bali wawategemee wanachama wao kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha mobilisation campaign zao.

Wananchi wa vijijini huwezi kuwaelimisha ikiwa kuelimisha kwenyewe ni kuponda mtu mmoja mmoja ,wananchi wataelimika ikiwa utaiponda serikali nzima ya CCM na sio kuchagua fisadi mmoja mmoja ,ambao CCM na Serikali yao wameanza kumuweka kando mmoja mmoja ,tunasema tunachohitaji ni kuiondoa CCM madarakani na si kumuondoa Lowasa au Chenge ,CCM nzima iondolewe katika uongozi wa Inchi hii na kuwekwa sio benchi bali nje kabisa ya uwanja.

Hivyo serikali ipondwe mbele ya macho ya wananchi mchana kweupe ,maana ukipima gharama za maendeleo wanayojisifia CCM na gharama ya Fedha zilizoibiwa utaona zilizoibiwa ni nyingi sana kuliko hiyo miradi inayojisifia serikali hii huku ni kuwadanganya wananchi ,maendeleo yanayotakiwa kusikika ni kuhakikisha serikali ya CCM inaondolewa madarakani kwa njia ya upigaji kura na fedha walizoiba wanachama wao kupitia vyeo mbalimbali vya serikali zinahakikishwa zinarudishwa ,hapo ndio mwananchi wa kijijini atakuelewa lakini kwenda huko na kusema Mkapa ni mwizi atakwambia na wewe mwizi vile vile.
 
Back
Top Bottom