Hapa kikwete katupiga bao!

Dark City kama huelewi tofauti ya success na failures sana itakuwa jambo lingine hlo.

Pia Msanii aliahidi kupitia na kurekebisha mikataba ya sekta ya madini. Kwa kweli mpaka leo mimi sijaelewa kabisa deliverables muhimu katika hili?

Suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar alilojifanya kuongea kwa hisia kali sana, mpaka leo ni kitendawili.

Suala la nyumba za serikali walizoziuza wakati wa Mkapa aliloahidi kulipitia mpaka leo anasuasua tu.

Hoja:

Kama ameshindwa kuyafanya yote hayo na mengineyo kipindi cha kwanza cha miaka mitaka (hadi mwakani) ikiwa ingekuwa ni vyema kwa ajili ya kugombea kipindi cha pili, sidhani kama kipindi cha atakuwa na changamoto yoyote muhimu kwani anajua hataweza kugombea kwa mujibu wa kikatiba.

Kumbukeni hata Chinga Mkapa alifanya madudu sana kipindi chake cha pili.

Kazi kwetu.

La muhimu ni wa Tanzania ni kuchagua wabunge wengi wa upinzani ili kuweza kulipa bunge guvu ya kuidhibiti serikali.

Nsololi;

Ndugu yangu jina lako ni jema sama kule kwetu jina lako lina maana kuwa mtoto aliyezaliwa pekee,
Ila nataka nikuamshe usingizini, najua wewe haujui mchezo mchafu wa CCM, wao ccm kwa sasa hawalali wanatafakari 2010 ila kwa sisi wapinzani hatujipangi tunaishia kupiga kelele huku tukuwapa mwanya ccm kujikosoa.
 
Jambo lililo dhahiri ambalo JK, watangulizi wake, TANU na CCM ni kushindwa kudeliver a very basic right kwa kila mtu nayo ni maji safi na salama. Hata pale yanpopatikana kiasi basi ngonjera za kuchemsha maji haziishi!
 
Nyambara nimekusoma,

ILa nyambara 2010 tutan'goa Muuungwana?
 
ndugu isaya mwita, mi nadhani unakashughuli kanakokupatia vijisenti na imekuwa ni kama pazia ambalo uwezi kuona maendeleo ya wenzio, maendeleo ya nchi ayapimwi kwa kipato cha mmoja mmoja.
1. tuliambiwa kutakuwa na ajira 100000, naona wewe upo miongoni mwa hizo
2. kuna mabilioni ya kikwete, labda wewe ndio umetokea humo
ukiona kwenye nchi mpaka chumvi inapanda bei basi hiyo ni balaa
jaribu kuwa muungwana basi watanzania wenzako wanakuomba umwage mafanikio aliyoyafanya huko Mpiganaji
 
Unless kiswahili kimebadili maana ya mafanikio, lakini mafanikio ni hali chanya kuelekea lengo fulani, kama vile la maendelea, sasa kama uanendelea kuelekea nyuma hayo ni matatizo sio mafanikio tena

Mkuu Kaizer, kuna mafanikio negative pia. Kuna mafanikio ya kubomoa, kuna mafanikio ya wizi, kuna mafanikio ya kudhalilisha, kuna mafanikio ya kuharibu vile vile na mafanikio mengine mengi yasiyofaa. Kinachofanya mafanikio hayo kuwa chanya au hasi ni nia ya jithada zinazotumika kuyafanikisha.
 
Recta,

Nadhani umeniewa vizuri kuliko nivyotamani kuelewekaa! Mafanikio yanategemea na mtu anavyoamua kueleza. Hivi mtu akisema hivi (kama awanavyosema wenye chama chao), "tumefanikiwa kuviua vyama vyote vya upinzani na kuwanunua wanachama wao, ambao sasa tumewapa vyeo kwenye chama chetu" atakuwa amekosea? Lakini ukifikiria kwa mapana na ukiwa na mtazamo wa kuipenda nchi, utaweza kusema hayo ni mafanikio?? Ipo mifano mingi ya namna hiyo. Kwa maana hiyo, tunatakiwa kuwa na vigezo vya kutumia kujipima ili tuweze kusema kama tumefanikiwa au la! Vinginevyo mtu anaweza kuja na mambo ya ajabu ajabu na kujaribu kutuaminisha kuwa hayo ndiyo mafanikio yake au ya serikali.
 
Maane hebu ni evidence gani utahitaji kuona kama jamaa anaweza hata kumsariti hata rafiki yake mpenzi(Rowasa)

Isaya Baba jina lako linatoka katika kitabu chema na ndani ya kitabu hicho kuna mistari inasema: Kuna wenye macho hawataona na wenye masikio hawatasikia sidhani kama wewe ni mmoja wa hao, kwani LOWASA hakusalitiwa bali KAJISALITI. nae hayupo pekee.
 
serikali ya chama tawala siku zozote inasimamia vyema ilani ya uchaguzi isipokuwa watu binafsi kwa ubinfsi wao wanafanya makosa wanakosa maadili wasiona vyema wanajumuisha chama na mtu binafs .

hata jambazi anaweza kuwa na kadi ya ccm lakini ccm si jambazi!!!! tuelewe hili.

Rais anafanya vyema kabisa kwa hili tumpongeze sana ingawa binadamu hajakamilika,nasi tumuumge mkono kwa nguvu zote zetu kwa kila jambi aliloanzisha linaloitakia mema nchi yetu ya Tanzania.
 
ndugu isaya mwita, mi nadhani unakashughuli kanakokupatia vijisenti na imekuwa ni kama pazia ambalo uwezi kuona maendeleo ya wenzio, maendeleo ya nchi ayapimwi kwa kipato cha mmoja mmoja.
1. tuliambiwa kutakuwa na ajira 100000, naona wewe upo miongoni mwa hizo
2. kuna mabilioni ya kikwete, labda wewe ndio umetokea humo
ukiona kwenye nchi mpaka chumvi inapanda bei basi hiyo ni balaa
jaribu kuwa muungwana basi watanzania wenzako wanakuomba umwage mafanikio aliyoyafanya huko Mpiganaji

Kituko;

Mara kwa mara nimekuwa nawashauri wana jamiiforums kuwa kwa hizi kelele zetu hapa jamvini hazitatusaidia kabisa, mwaka 2008 july niliwahamasisha akina mwanakijiji, Jmush1 kuwa tuwe na mkakati na wala si kelele, ndipo Mwanakijiji akaja na kijarida cha chehche, Cheche kijarida kinachopendwa na watu wengi kinafanya vizuri kule mtaani,

Haikutosha hapo nikaona nirudi kule nyumbani nikapige kelele ili niwaamshe ndugu zangu waelewe ubaya wa CCM na kweli ule uchaguzi wa Tarime tukashinda bila hofu japo nilipigwa vya kutosha.

Haijalishi leo tena nasema wewe Kituko; na wenzako mmelielimisha Taifa hili kwa kiasi gani? ama ni hizi kelele hapa jamvini kisha mnarudi kwa mama zenu kunyonya?

Kituko; tukiwa na matanzania 10 kama wewe hakika taifa hili litaendelea kuzama.

Wito wangu wana Jamii forums tunatokaje 2010?

Kule Mara najua CCM hawatakuja kabisaaa!!!!!!!!,

Mnakumbuka sherehe za CCM 2009 zilifanyikia wapi?

Eti kuimarisha chama.......... wapi Mkoani Mara????????
 
Last edited:

Mkuu I Mwita, mbona sherehe za CCM 2009 (miaka 32) zilikuwa Shinyanga? Au kuna nyingine unaongelea?
 
Mkuu I Mwita, mbona sherehe za CCM 2009 (miaka 32) zilikuwa Shinyanga? Au kuna nyingine unaongelea?

Dark City;

walichinja nini huko shy?

Mkuu wangu kama sikosei pale serengeti kulikuwa kunaadhimishwa nini?

Dark City;mimi kama mimi najua mabadiliko yanakuja japo wewe Dark City; haujafanya chochote katika mkoa wako na watu wako, nakushauri toka huko mjini rudi kule kwenu kijijini kawaelimishe ndugu zako kawaambie jinsi CCM WALIVYOTUFANYA MIAKA 48 hii.
Dark City; acha kung'ang'ania mjini
 
Hongera jafar kwa uchambuzi wako, umetulia. Hii ndio hali halisi hasa mfuko wa mbolea kupanda kutoka 15,000 hadi 125,000 na wanadai wanaboresha kilimo..., huu ni mchezo wa kuigiza ninavodhani mimi
 
Kwa jinsi Muungwana anavyo wajibika kwa sasa si ndiyo anazidi kukiruka kiunzi 2010? hatujui tutamrushia madongo yapi, kwani yeye kama yeye hakika anaendelelea kuisafisha ile njia,

Tuangalie tusije tukakosa mshiko, !!!!!

Nadhani zile hoja za kufichua ufisadi tungeanza sasa si mwaka jana, hawa jamaa wanaendelea kujisafisha

Sijaelewa kwamba wanapowapeleka akina Mramba baada ya uchaguzi watawafutia kesi zao ama?

Nimeipenda ile style yao.

Ama nina makengeza?

The man is trying to play out cards. However its too late!
 
The man is trying to play out cards. However its too late!

Calnde;

Hizo ndizo fikra zako na hisia zako, wakati wenzako tunazichanga na kuelekeza akili zetu miaka 5 ijayo wewe umeshikilia ganda la muwa, lina utamu hilo????

Fikiri sana my young bro/ hapa tupo kutikisa akili za watu na kuzifanya ujinga uondoke vichwani mwao, wewe unaona kama ...., ok.

Calnde; ujue kuwa kama tutakosa mtizamo sisi tutalaaniwa na kizazi kijacho , fumbua macho ndugu yangu.
 
i
sayamwita;375997]
Dark City;

walichinja nini huko shy?

Kwa CCM nadhani walichinja kila kitu isipokuwa binadamu:cool:

Mkuu wangu kama sikosei pale serengeti kulikuwa kunaadhimishwa nini?
Sijapata kusikia habari ya sherehe za Serengeti. Labda makada wa Chama Chao humu ndani watatupa data.

Dark City;mimi kama mimi najua mabadiliko yanakuja japo wewe Dark City; haujafanya chochote katika mkoa wako na watu wako, nakushauri toka huko mjini rudi kule kwenu kijijini kawaelimishe ndugu zako kawaambie jinsi CCM WALIVYOTUFANYA MIAKA 48 hii.
Dark City; acha kung'ang'ania mjini
Mkuu naona unataka idendity yangu kwa nguvu au? Soma profile yangu kwanza ujue niko wapi halafu ndo upigie mistari miwili (conclusion) kwamba niko mjini.
Watu wameshaelimika mkuu, ila bado yale maji ya bendera waliyonyeshwa ndo yanawapa hang-over. Hata hivyo hakuna mwalimu wa nguvu kama shida. Kwa kibano wanachopata naamini hiyo nyamulunda (anaesthesia) itaisha sasa hivi, labda kama WaTz wamelaaniwa.
 
mnamtafuta mshindi wa 2010 kwa ticket ya CCM, Chadema, TLP au CUF? Nijuavyo mimi kila chama kitapitisha na kitamsimamisha mgombea wake, baada ya hapo wananchi wapima sifa kila mgombea. CCM hawajesama kuwa JK ndiyo mgombea wao, vyama vingine pia wavijasema mgombea atakuwa yupi hapa tupambanisha nani na nani?
Uchumi
Yapo matatizo ya kidunia mbayo hata JK asingeweza fanya miujiza ya kuibadili TZ haraka hivyo, USA yenyewe pamoja na kuwa na uchumi wenye nguvu kwa hali yao ya sasa wanasema hawawezi jichomoa over night sembuse TZ? Hata hivyo kisiasa inakubarika na mtu anaweza itumia kuisambaratisha CCM au kumuangusha mtu hata kama mtu huyo siyo factor. Hilo ndio tatizo la siasa ama wanasiasa......kutungushia maneno ili wapate kura.....
 
care4all,

care4all sipati shida kuelezea itikadi yako, nadhani si wakati muafaka kurumbana ila naomba usome nyakati, tambua yote yanayofanyika ndani ya serikali yetu kwa sasa ni kivuli cha 2010, najua unaufahamu mwamvuli kazi yake kubwa ni kukukimba usilowe na mvua au jua, sasa tunapaona serikali hii inaanza kutudanganya ili tuamini hakika tunapata mashaka makubwa mno.

care4all najua wewe ni mzalendo wa kweli ila tu uzalendo wako haujielezi vema, wakati sisi tunafikiri nini kifanyike ili tupate upinzani wa kweli wewe unalete hadithi za rejea hebu kweli tutafika?
 
baadhi ya mafaniko ya Jk

1. kajenga chuo kikuu Dodoma
2. makusanyo ya kodi yameongezeka kutoka bilioni 195 wakati wa Mkapa hadi bilioni 400
kila mwezi ambayo ni mara mbili
3. kapunguza ujambazi.
4. kapeleka watuhumiwa wa EPA mahakamani
5. Kamwachisha kazi Waziri Mkuu Lowassa
6. Amenunua Panton jipya Kigamboni linabeba magari 60 na abiria 2000
7. Ameokoa shirika la ndege ATCL kwa kuwapa mtaji mpya
8. Amerudisha nyumba za serikari 120
9. amesimamisha ununuzi wa magari ya serikali ( mashangingi) na pesa hizo ziende katika ununuzi wa matrekta.
 
Ongeza na hii,
"ameoa au anataka kuoa mke mwingine kabla ya 2010"!!:rolleyes:
 
Back
Top Bottom