Hapa inakuage wadau na hii mitandao ya simu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa inakuage wadau na hii mitandao ya simu!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkare, Dec 23, 2010.

 1. M

  Mkare JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani kuna vitu vya ajabu huwa vinatokea. Sasa sijui ni kwa tigo pekee au na mitandao mingine. A friend of mine ingekuwa sio kutumia busara ilibakia kidogo tu ndoa iote mbawa. Alimpigia mkewe aliyekuwa mkoani Dodoma mida kama saa nne usiku. Ile simu ikapokelewa na mwanaume. Akamwambia namuomba mwenye simu, jamaa akasema simu ni yake ana maana gani kumwambia anamuomba mwenye simu? Jamaa akakata. Kidogo akapiga tena, simu ikawa haipatikani, akapiga kama mara tatu hivi ikaita. Akapokea mkewe aliyeamka kutoka usingizini.
  Jamaa kwa ghadhabu akamwambia uko wapi, wife akajibu nilikuwa nimelala. Wee, jamaa si ndio kupanic na kuanza kubwabwaja, huyo mwanaume nani, malaya mkubwa wewe... hee! wife hana hili wala lile, akajua tu jamaa labda ni wivu tu kawaida... si ndio akamwambia jamaa, wee vipi hebu nitolee wazimu wako hapa na wivu wako... Akazidi kumchanganya jamaa.... Kwa hiyo ndio mmepanga hivyo na huyo bwana wako... bla bla kibao. Mh! Wife akaona hii sasa kali. Si ndio kuuliza kwani vipi wewe... Jamaa ndo kuelezea.... Wife hana hata moja....
  Lakini m/mme roho haikumpa kabisa.... Asubuhi kabla hata ya kwenda job akatia timu afisi za tigo makao makuu akawaelezea wamuambie inakuaje hiyo, Wakamwambia kuwa huwa inatokea... Kumthibitishia, wakamwonyesha namba iliyopokea simu alipopiga kwamba ni mbaba yupo Manyoni-Singida.Na haikuwa ya tigo iliingia kwenye mtandao mwengine!!! Hebu niambieni hii situation kama huna subira si umeshaacha mke???
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiyo issue ilisha nitokea sana kama mara mbili au tatu hivi but nikachukulia ize tu. ila inakera sana kwa kweli!
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  inatokea sana tena sana mwingiliano huo mitambo hyo inakuwa imezidiwa ina amua kuchakachua
   
 4. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni Uzembe tu wa telephone operator wetu hao wa TIGO na machine zao feki. Kama ni mitambo kuzidiwa basi isingeunganisha, ingeonyesha kuwa namba haipatikani. Wazembe saana TIGO, Bora Airtel, Voda au Sasatel:teeth::teeth::teeth:
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kwa voda hutokea mara nyingi ila hukatika muda mfupi baada ya mpigiwa kupokea simu!kama una papara waweza ua mtu
   
Loading...