Hamisi Kigwangalla: Nimeambiwa nafuatiliwa, ila naamini niko salama

Kigwa anatuchanganya tu, kwenye taarifa yake ya mwanzo hakutaja jina la yeyote, hapa tena anadai watu wake wanafuatiliwa na wasiojulikana, huyu mbona anatuzungusha tu...

Ni kama vile alijitungia story ambayo anaiendeleza kijanja bila kutaja jina la yeyote, sasa hao TAKUKURU na wengine wamfuatilie kwa kosa gani ikiwa hajamtaja yeyote mpaka sasa? wala hajalalamikiwa na yeyote mpaka sasa?!

Usanii wa siasa. Anataka ku trend tu.

Sent from my SM-G900H using
You nailed.Anataka ku trend lakini amechagua ku trend kishamba.Hamna uzito wowote kwa alichosema ni kama kupiga ngumi hewa.
 
Uyo Faller anaongeaga Sana akishatolewa kwenye uwaziri, akirudishwa tu ana myuti Kama hayupo.

Uyo Ni mnafiki, namuonaga Ni limbukeni flani,afu mshamba flani mwenye wivu.

Sijajua uyo jamaa Ni kabila gani
 
Ng'ombe wa kufugwa wana taabu sana, usipompa majani kwa muda fulani...hizo kelele ni balaa lake!

Btw, tuko kipindi cha giza totoro na watu wako usingizini wanakoroma, acha tu apige kelele yamkini wezi wakaogopa kwa kuhisi watu wako macho.
Panyaroad au
 
"Kujaribu kuninyamazisha haitosaidia kitu maana kama unahisi mimi najua kitu, ambacho sijakisema, jua na wengine wanajua." meaning kuniondoa/kuninyamazisha mie hakupunguzi/hakufuti madhara yanayoweza tokea. Ni siri iliyo wazi ye katangulia tu kusema 😂....Tunaelekea wapi nchi hii?
Kazi kweli kweli !! Hiii 🙄
 
Huyu anatafuta teuzi kwa kila hali. Haamini kuwa kawekwa benchi. Anapiga kelele ili aambiwe ‘njoo bwana tule wote, acha kelele’.
 
Nimeambiwa kuwa nafuatiliwa - sijui kwa lengo gani, lakini naamini niko salama. Mnaoniuliza msiwe na shaka. Kama nikiitwa TAKUKURU, Tume ya maadili, polisi n.k. siyo mambo ya ajabu, huko ni mahala salama. Watu wangu wa karibu wamekuwa wakipewa vitisho na watu ambao hawawezi kuwataja kuwa nafuatiliwa.

Nimekuwa nikishangaa na kushtuka, maana sina uadui na mtu, na sikutaja mtu. Kujaribu kuninyamazisha haitosaidia kitu maana kama unahisi mimi najua kitu, ambacho sijakisema, jua na wengine wanajua!

Kama umeficha vizuri, hakuna litakalokupata, maana TAKUKURU ama sekretariet ya maadili watataka ushahidi usio na shaka kabla ya kukupeleka kortini. Na siku zote ushahidi hautopatikana, na hivyo kama Jamhuri hatutokupata! Kama wewe ni kiongozi, jiulize tu ukishaiba mali nyingi sana ya umma unasikia raha gani? Utapeleka wapi? Utatumia zote hizo? Utazikwa nazo?

Halafu jiulize, mwenye kosa ni anayetoboa mtumbwi ama anayepiga yowe na kumsonteshea mtoboaji ili wasafiri wote tushtuke? Tumdhibiti?

Kushtuka shtuka namna hii inaonesha watu wanajishuku. Kunifuatilia na kutafuta kunitisha tisha mtanifanya nichambue hadharani taarifa za CAG, za TAKUKURU na michango ya wabunge bungeni nk. Humo kuna viashiria vingi sana vya rushwa na ubadhirifu, je kama Taifa mifumo yetu ya uwajibikaji imefanya kazi ipasavyo?

Nilipozungumza juu ya uwepo wa haja ya kuimarisha mifumo ya uwajibikaji na usimamizi wa mali ya umma, sikuwa na nia ya kumtaja mtu yeyote. Nilipenda kutoa maoni yangu tu juu ya haja ya kuimarisha mifumo/taasisi za uwajibikaji kama Taifa; aidha mifumo/taasisi za kifedha, na mifumo/taasisi za kisiasa. Kama hujaitazama ile interview, nenda kaitazame.

View attachment 2876430
Hadi mtajane 😆😆
 
Back
Top Bottom