Hamis Kiiza 'Diego' aipasha Simba SC!

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
5,119
5,683
Mshambuliaji aliyetupiwa virago na klabu ya Simba, Hamisi Kiiza amesema timu hiyo ya Simba haiwezi kupata mafanikio hata kama itawasajili wachezaji wote wanaofanya vizuri Tanzania, na kumrudisha Mbwana Samatta, kwani tatizo kubwa lililopo Simba ni baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakianzisha na kuendekeza na chuki na wachezaji hasa wanaposema ukweli na kudai haki zao stahiki,”alisema Kiiza.

Nyota huyo raia wa Uganda, amekwenda mbali zaidi akisema timu ya Simba haitakuwa na mafanikio hadi baadhi ya viongozi wanaoendekeza chuki, fitna na migogoro isiyokuwa na tija kwa timu waondoke madarakani.

Kiiza alisema Simba ilikuwa na nafasi kubwa ya kubeba ubingwa msimu uliopita, lakini fitna za baadhi ya viongozi hao ndiyo ziliwaumiza sana wachezaji na kuwatoa kabisa kwenye ramani ingawa walikuwa na nafasi kubwa ya kufanya vizuri tangu wakiwa na kocha Dylan Kerr na Jackson Mayanja

Kiiza aliye enguliwa kwenye kikosi cha msimu ujao wa Ligi Kuu na uongozi wa timu hiyo, licha ya kushika nafasi ya pili kwa ufungaji bora kwa kufunga mabao 19, kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita alisema tatizo kubwa la Simba ni uongozi na siyo wachezaji wala makocha ambao wamekuwa wakibadilishwa kila msimu,

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, alisema ameshindwa kumalizia mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki Simba kwa sababu ya tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili ndani ya timu hiyo, kubwa ikiwa ni kuambiwa anaigawa timu na kwamba ana mapenzi na Yanga, alisema kama angekuwa anaihujumu timu hiyo asingefunga mabao 19 ambayo ndiyo yaliipa ushindi timu hiyo, hadi kuna wakati ikawa inaongoza ligi na kuziacha mbali Yanga na Azam.

Source: Gazeti la HabariLeo!
 
Hili ndio tatizo linalo sumbua timu yetu. Sina imani na Simba kama itaweza kuchukua Ubingwa mwaka huu.

Hata wageni wameliona hili. Ni bora MO. Apewe
 
Anaye lalamikiwa kila mara yupo na anajulikana, najua habari hii imekwisha mfikia, sasa ingekuwa vema akatumia busara kuwapisha wanachama wengine wa Simba wenye uwezo kama yeye au hata kumpita yeye kuiandaa timu kwa ajili ya msimu ujao!
 
Hahaaa, hiii siyo rahisi, viongozi wa kiafrika wanatolewa bakora na mitutu ya AK-47!
 
Sidhani kama ni ajabu kumuacha mfungaji wa pili penye ligi kama waliweza kumuacha tambwe nadhani ni muendelezo wa majirani zangu ila kila siku nasema hizi timu zetu kuwekwa mfukoni na mtu mmoja ni khatari sana. Ulaya Inawezekana sababu kuna sheria na kanuni zinafuatwa ila kibongo bongo hakuna namna.
 
Anaye lalamikiwa kila mara yupo na anajulikana, najua habari hii imekwisha mfikia, sasa ingekuwa vema akatumia busara kuwapisha wanachama wengine wa Simba wenye uwezo kama yeye au hata kumpita yeye kuiandaa timu kwa ajili ya msimu ujao!
Hafadhali hujamtaja jina, utaambiwa jina hilo lilitumika wakati ule wa vita vya ukombozi wa wenzetu, sasa uhuru upo ni kama ndugu hayati Mandela alituambia.

Siyo rahisi kumtoa jamaa anatisha, yeye anataka usaidizi tu afanye yake hataki cheo kikubwa.
 
Huyu Kiiza nae atulize kipago.. Asidhani kama tumesahau haya

1. Ile tabia yake ya kuchochea vitendo vya utovu wa nidhamu ndani ya timu. Mfano kitendo chake cha kupinga kufungiwa kwa nahodha wake, Hassan Isihaka.. Sasa Leo wote OUT.

2. Tabia yake ya kuchelewa kujiunga na kambi ya Simba akitokea Uganda alipokuwa akitumikia timu yake ya taifa.. Na hii nadhani ni kujiona amekua Mkubwa zaidi ya timu.

Kiiza kila la heri uendako.. Simba tutaendelea kua imara zaidi.

Simba S.C [Nguvu Moja]
 
Mbona Okwi alikuwa na tabia ya kuchelewa na kuishi kifalme simba na hamkumfukuza?
 
Back
Top Bottom