Uchaguzi 2020 Hamasa ya wananchi kuunga mkono upinzani

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,572
9,809
Mwaka huu wa uchaguzi tunashuhudia kampeni za uchaguzi zikiendelea kushika kasi huku upande wa upinzani ukiwa na hoja imara zenye kukosoa sera za kimazoea za chama tawala. Nasema ni sera za kimazoea kwa kuwa CCM haina hoja mpya zaidi ya ile ile ya kuzungumzia kutimiza wajibu wa kawaida kwa serikali yoyote ile yenye kutoza kodi wananchi wake.

Chama tawala kinajitahidi kumpambanua na kumnadi mgombea wake wa uraisi kama ni mtu maalum ambaye amejitolea kwa dhati kuleta maendeleo ya vitu hapa nchini. Wanajaribu kujenga ghiriba kama hiki ni kitu cha kipekee kuwahi kutokea, na pia ambacho hakuna mtawala yeyote aliyemtangulia ama wa nchi nyingine aliyewahi kufanya maajabu kama yake.

Naam! Kama ni ujinga wa hali ya juu ambao utawasukuma wapiga kura kukataa kughiribiwa ni hoja kama hii. Hapo ndipo hujikuta wakilazimika kufanya uamuzi sahihi wa kuwapuuzia na hata kuwakataa, na kwa hakika "this is the crux of the matter". Hoja hiyo isiyo kuwa na mashiko yoyote yale ndiyo hasa sababu inayowafanya wananchi kuwashtukia na kuishi nao kinafiki.

Katika kipindi toka awamu hii ya tano ilipoingia madarakani, imekosa kabisa njia sahihi na yenye tija katika kupangillia "scale of preference" zake ili kuweza kuendesha miradi mikubwa iliyokwisha kuianzisha. Badala ya kupangillia kuanza na mradi mmoja mkubwa na pale unakamilika kwa asilimia kubwa ndipo tena waje na mradi mwingine mkubwa, wao kwa pupa wakaamua kuanza miradi mikubwa zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja ili tu wapate sifa za kutaka kufunika awamu zilizotangulia hasa awamu ya nne.

Miradi mikubwa hii huitaji fedha nyingi sana ktk kuijenga. Hapa ndipo serikali imejikuta ikiingia ktk mtego wa kukwepa kutekeleza majukumu yake muhimu ya kufanikisha maendeleo ya watu. Serikali hii imejikuta ikilazimika kujikita zaidi ktk maendeleo yake ili kukwepa aibu inayoweza kutokea mbele ya safari kwa miradi hii kutokamilika.

Kwa uamuzi huo imejikuta ikiyaathiri makundi mengi ya kisekta kimapato hasa sekta binafsi. Badala ya serikali kutumia fedha zake za matumizi ndani ya nchi ili kuongeza mzunguko wa fedha, imejikuta imekuwa ni mnunuzi wa vitu kutoka nje ili kutaka kumalizia miradi hiyo mikubws, na hivyo basi matokeo yake ni kuwa na mzunguko mdogo sana wa fedha ndani ya nchi hali iliyoleta ukata wa fedha kwa wananchi.

Kuwa na ukata mkubwa wa fedha kwa miaka mitano mfululizo, huku serikali ikionekana kuwa imevaa miwani ya mbao ndiyo hasa inapozaliwa hamasa ya wananchi ya kuunga mkono vyama vya upinzani, ikiwa kama njia mbadala ya kutaka kuhakikishiwa hali bora ya maisha yao ya kila siku. Ni ukweli kabisa pale vipato vinapopungua kwa wazazi ama walezi "multiplying effect" hutokea kwa wategemezi wao wote, kwa sababu kile wanachokipata hujikuta wakilazimika kukitumia tu kwa mambo yao muhimu tu tena yenye ulazima wa hali ya juu.

Ni jambo llililokuwa bayana kuwa makundi mengi ya kisekta yamepigika kweli kweli ndani ya awamu hii ya tano. Vipato ktk familia navyo vimepungua mno huku watawala wakibeza kuwa eti hapo awali walikuwa ni vipato vya ziada kwa kuwa walikuwa wapiga dili. Na eti kwa kuwa sasa dili hizo zimedhibitiwa barabara hii ndiyo sababu inayopelekea ukata wa fedha utamalaki ktk jamii.

Watawala wanasahau jambo moja muhimu kuwa pale kipato cha mtu mmoja mmoja kinapopungua, wanaoathirika zaidi ni wale walio tegemezi moja kwa moja kwake. Mtu akikosa kipato cha uhakika, mathalani kwa mwanaume basi nyuma yake pengine yupo mke, watoto, wazazi, ndugu wa mume, ndugu wa mke na wengine anao waajiri na wote hao wanaathirika endapo watakuwa ni tegemezi kwa kipato chake moja kwa moja.

Ni dhahiri kuwa nyuma ya mtu mmoja aliyekumbwa na ukata kuna uwezekano wa uwepo wa wastani wa kati ya watu 3-10 wenye kuathirika pia kiukata. Hawa wote ndiyo tuna washuhudia hii leo wakimuunga mkono Tundu Lissu kila pale aendapo. Wanaoonekana zaidi ni vijana, lakini ukweli ni kuwa kuna kundi lingine lisiloonekana ambalo ni lenye hamasa kubwa na lipo nyuma ya vyama vya upinzani.

Mpaka sasa kuna hakikisho la zaidi ya 68% ya kura zote zinazotegemewa kupigwa siku ya tarehe 28-10-2020 kutoka kwa wapigakura hawa. Katika jicho lisilokuwa na idadisi ama shahuku ya kutambua, anaonekana mtu mmoja mwenye kuathirika, mathalani mtumishi wa umma, bali kuna mlolongo wa watu nyuma yake pia wanakuwa na hasira juu ya watawala.
 
Wimbo ni uleule madaraja, barabara, flyover n.k, huwezi kusikia anazumgumzia bei ya mazao, mifugo, maisha ya kawaida ya wananchi, uhuru wa watu, mishahara kwa watumishi wala ajira za kudumu.
Kubwa kuliko yote kila mara wamekuwa wakisisitiza kuilinda amani na wanadiliki kuwaambia wapiga kura kuwa wakichagua wapinzani wataleta vita.

Katika hotuba zao huwezi kuwasikia hata siku moja wakisisitiza kutenda haki. Neno haki kwao umekuwa ni msamiati mgumu sana kuutamka.

Halafu wanaamini wapiga kura ni wajinga, hawajielewi ndio maana ya kauli yao kuwa wakichagua wapinzani wataleta vita kauli hii imekuwa ikitumika miaka yote kama njia sahihi ya kuwashawishi wapiga kura.

Bahati mbaya wanashindwa kujua kwamba kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano elimu ya uraia imeenea kwa kasi sana mpaka huko vijijini na kiwango cha uelewa kwa watanzania kimeongezeka sana. Hivi inawezekanaje mtu uliyempigia kura ndio akuletee vita?

Yaani propaganda zingine ni choko sana.
 
Ukweli huu unaleta uchungu!

Wapiga kura ,wengi ni vijana,
Wasiokuwa na kazi(ajira),wengi ni vijana.
Wanaohudhuria na kufuatilia mikutano hii,wengi ni vijana.
Wanaomuelewa mtia nia ya nafasi ya urais,wengi ni vijana.
Wanaofahamu kuwa wakiamua wanaweza,wengi ni vijana.

Ushauri:Wenye Mamlaka wasipuuze ,hisia na maamuzi ya wapiga kura kwa kutumia nguvu na hila kudhulumu maamuzi ya wananchi.
Tukumbuke,watawala huwa wanajisahau,na kujikuta wakitumia vyombo vya dola vibaya!!!
 
Mwaka huu wa uchaguzi tunashuhudia kampeni za uchaguzi zikiendelea kushika kasi huku upande wa upinzani ukiwa na hoja imara zenye kukosoa sera za kimazoea za chama tawala. Nasema ni sera za kimazoea kwa kuwa CCM haina hoja mpya zaidi ya ile ile ya kuzungumzia kutimiza wajibu wa kawaida kwa serikali yoyote ile yenye kutoza kodi wananchi wake.

Chama tawala kinajitahidi kumpambanua na kumnadi mgombea wake wa uraisi kama ni mtu maalum ambaye amejitolea kwa dhati kuleta maendeleo ya vitu hapa nchini. Wanajaribu kujenga ghiriba kama hiki ni kitu cha kipekee kuwahi kutokea, na pia ambacho hakuna mtawala yeyote aliyemtangulia ama wa nchi nyingine aliyewahi kufanya maajabu kama yake.

Naam! Kama ni ujinga wa hali ya juu ambao utawasukuma wapiga kura kukataa kughiribiwa ni hoja kama hii. Hapo ndipo hujikuta wakilazimika kufanya uamuzi sahihi wa kuwapuuzia na hata kuwakataa, na kwa hakika "this is the crux of the matter". Hoja hiyo isiyo kuwa na mashiko yoyote yale ndiyo hasa sababu inayowafanya wananchi kuwashtukia na kuishi nao kinafiki.

Katika kipindi toka awamu hii ya tano ilipoingia madarakani, imekosa kabisa njia sahihi na yenye tija katika kupangillia "scale of preference" zake ili kuweza kuendesha miradi mikubwa iliyokwisha kuianzisha. Badala ya kupangillia kuanza na mradi mmoja mkubwa na pale unakamilika kwa asilimia kubwa ndipo tena waje na mradi mwingine mkubwa, wao kwa pupa wakaamua kuanza miradi mikubwa zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja ili tu wapate sifa za kutaka kufunika awamu zilizotangulia hasa awamu ya nne.

Miradi mikubwa hii huitaji fedha nyingi sana ktk kuijenga. Hapa ndipo serikali imejikuta ikiingia ktk mtego wa kukwepa kutekeleza majukumu yake muhimu ya kufanikisha maendeleo ya watu. Serikali hii imejikuta ikilazimika kujikita zaidi ktk maendeleo yake ili kukwepa aibu inayoweza kutokea mbele ya safari kwa miradi hii kutokamilika.

Kwa uamuzi huo imejikuta ikiyaathiri makundi mengi ya kisekta kimapato hasa sekta binafsi. Badala ya serikali kutumia fedha zake za matumizi ndani ya nchi ili kuongeza mzunguko wa fedha, imejikuta imekuwa ni mnunuzi wa vitu kutoka nje ili kutaka kumalizia miradi hiyo mikubws, na hivyo basi matokeo yake ni kuwa na mzunguko mdogo sana wa fedha ndani ya nchi hali iliyoleta ukata wa fedha kwa wananchi.

Kuwa na ukata mkubwa wa fedha kwa miaka mitano mfululizo, huku serikali ikionekana kuwa imevaa miwani ya mbao ndiyo hasa inapozaliwa hamasa ya wananchi ya kuunga mkono vyama vya upinzani, ikiwa kama njia mbadala ya kutaka kuhakikishiwa hali bora ya maisha yao ya kila siku. Ni ukweli kabisa pale vipato vinapopungua kwa wazazi ama walezi "multiplying effect" hutokea kwa wategemezi wao wote, kwa sababu kile wanachokipata hujikuta wakilazimika kukitumia tu kwa mambo yao muhimu tu tena yenye ulazima wa hali ya juu.

Ni jambo llililokuwa bayana kuwa makundi mengi ya kisekta yamepigika kweli kweli ndani ya awamu hii ya tano. Vipato ktk familia navyo vimepungua mno huku watawala wakibeza kuwa eti hapo awali walikuwa ni vipato vya ziada kwa kuwa walikuwa wapiga dili. Na eti kwa kuwa sasa dili hizo zimedhibitiwa barabara hii ndiyo sababu inayopelekea ukata wa fedha utamalaki ktk jamii.

Watawala wanasahau jambo moja muhimu kuwa pale kipato cha mtu mmoja mmoja kinapopungua, wanaoathirika zaidi ni wale walio tegemezi moja kwa moja kwake. Mtu akikosa kipato cha uhakika, mathalani kwa mwanaume basi nyuma yake pengine yupo mke, watoto, wazazi, ndugu wa mume, ndugu wa mke na wengine anao waajiri na wote hao wanaathirika endapo watakuwa ni tegemezi kwa kipato chake moja kwa moja.

Ni dhahiri kuwa nyuma ya mtu mmoja aliyekumbwa na ukata kuna uwezekano wa uwepo wa wastani wa kati ya watu 3-10 wenye kuathirika pia kiukata. Hawa wote ndiyo tuna washuhudia hii leo wakimuunga mkono Tundu Lissu kila pale aendapo. Wanaoonekana zaidi ni vijana, lakini ukweli ni kuwa kuna kundi lingine lisiloonekana ambalo ni lenye hamasa kubwa na lipo nyuma ya vyama vya upinzani.

Mpaka sasa kuna hakikisho la zaidi ya 68% ya kura zote zinazotegemewa kupigwa siku ya tarehe 28-10-2020 kutoka kwa wapigakura hawa. Katika jicho lisilokuwa na idadisi ama shahuku ya kutambua, anaonekana mtu mmoja mwenye kuathirika, mathalani mtumishi wa umma, bali kuna mlolongo wa watu nyuma yake pia wanakuwa na hasira juu ya watawala.
#Ni yeye#
 
Kubwa kuliko yote kila mara wamekuwa wakisisitiza kuilinda amani na wanadiliki kuwaambia wapiga kura kuwa wakichagua wapinzani wataleta vita.

Katika hotuba zao huwezi kuwasikia hata siku moja wakisisitiza kutenda haki. Neno haki kwao umekuwa ni msamiati mgumu sana kuutamka.

Halafu wanaamini wapiga kura ni wajinga, hawajielewi ndio maana ya kauli yao kuwa wakichagua wapinzani wataleta vita kauli hii imekuwa ikitumika miaka yote kama njia sahihi ya kuwashawishi wapiga kura.

Bahati mbaya wanashindwa kujua kwamba kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano elimu ya uraia imeenea kwa kasi sana mpaka huko vijijini na kiwango cha uelewa kwa watanzania kimeongezeka sana. Hivi inawezekanaje mtu uliyempigia kura ndio akuletee vita?

Yaani propaganda zingine ni choko sana.
Neno HAKI ndani ya CCM ni sawa na tendo la ndoa.
 
Naunga mkono, nimezaliwa na kukulia mjini, almost maisha yangu ya utafutaji 70% ni huku polini naweza sema ni mwisho wa hii dunia, idadi kubwa ya msimamo wa sisi wapolipoli ni kuunga mkono vyama pinzani husani ni CDM.
 
Baada ya Fiesta ya sisiem hapa Mbeya, Pale kabwe zilisikika kauli za vijana wakisema..

Kila kampeni wanatuambia habari za madaraja na barabara, hivi hizo barabara haziishagi tu kujengwa kwani zinaenda mbinguni...?

Mwingine akasikika akisema "Mzee anatupigia magoti sisi kwani tumemkosea nini huyu mzee..? Si mwaka 2015 alipiga Push ups, iweje kampeni hizi anapiga magoti..?

Kubwa kuliko yote kila mara wamekuwa wakisisitiza kuilinda amani na wanadiliki kuwaambia wapiga kura kuwa wakichagua wapinzani wataleta vita.

Katika hotuba zao huwezi kuwasikia hata siku moja wakisisitiza kutenda haki. Neno haki kwao umekuwa ni msamiati mgumu sana kuutamka.

Halafu wanaamini wapiga kura ni wajinga, hawajielewi ndio maana ya kauli yao kuwa wakichagua wapinzani wataleta vita kauli hii imekuwa ikitumika miaka yote kama njia sahihi ya kuwashawishi wapiga kura.

Bahati mbaya wanashindwa kujua kwamba kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano elimu ya uraia imeenea kwa kasi sana mpaka huko vijijini na kiwango cha uelewa kwa watanzania kimeongezeka sana. Hivi inawezekanaje mtu uliyempigia kura ndio akuletee vita?

Yaani propaganda zingine ni choko sana.
Propaganda za toka mwaka alfu tisamia kenda na tano wangali wanazitumia!!!
Hawajui kizazi kimeshabadilika
 
Ndio maana karata iliyobaki ni VITISHO vya mwenyekiti pekee. Kwamba msipochagua chama chetu SILETI MAJI, utafikiri kodi wanalipa watu wa Chato pekee.
 
Back
Top Bottom