Hamasa ya utalii: vijana wa mitandaoni watambuliwe

McFerson

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
2,120
2,167
Salaam wana jamvi

Nimejaribu kutembelea mitandao mbali mbali, Instagram Facebook/meta Twitter,n.k nimegundua Kuna harakati za kizalendo huko mitandaoni zinaendelea, vijana ni mabalozi wa sekta hii ya utalii inayoipatia nchi fedha nyingi za kigeni. Wengi wamefungua account za kuhamasisha utalii kwa nchi yetu kitaifa na kimataifa wahamasike ili watalii waongezeke nchini.

Ni wakati sasa kwa wizara ya utalii na mali asili kuwatambua na ikiwezekana kuwakutanisha na kuwapa semina nini wapost na nini wasipost na mengine mengi yatakayoonekana ni mema kuwajuza.

Asanteni
 
Hiyo wizara wakutane na watu ili wawafundishe nini cha kupost na kipi cha kuacha, kwani hao wizara wao wanapost nini kikubwa? Au wao ni kutunga sheria tu?
 
Tatizo ni wote kutumia Lugha ya Kiswahili pekee yake.

Vijana tujiongeze kuposti Instagram Facebook / meta Twitter kwa lugha za kigeni kama za ki Polish, Russian, Arabic, Hindu, Mandarin, Ukrainian, German, Spanish, English n.k ili habari hizo za vivutio zisambae kote ulimwengu.

Tuache woote kungangania Kiswahili tu katika majukwaa / platforms habari TV, Habari YouTube, Habari Online, Habari Michezo, Habari Utalii, Habari Elimu ya Juu, Habari miundo-mbinu, Habari Utamaduni, Habari Vyuo Vikuu, Habari Vyuo Elimu ya Ufundi, Habari Mahakama n.k
 
Huyu hapa anawakilisha vizuri kuitangaza Tanzania kwa lugha ya kigeni

Kitonga Mountain Tanzania 2022 full Experience !! Not For The Faint Hearted !!



Source : malango travel
 
Mdau huyu ktk clip angejiongeza zaidi maana clip kama hii ngumu kuonekana duniani ingawa ni nzuri kimazingira ya uoto wa kijani


MTO WA MBU



Source : traveller
 
Back
Top Bottom