Mm nakupa history ya kiswahili kipande kidogo tu utaelewa chanzo cha hawa wayahudi kuhamishwa Palestina
' jina liliendelea kutumiwa kwa umbo la Kiarabu "Filastin" na kutazamwa kama sehemu ya Shamu au Syria
Tangu eneo lilitawaliwa na Milki ya Osmani. Kwa muda mrefu maeneo ya Palestina yalikuwa sehemu ya kusini ya jimbo la, Damesk(Damaskas) katika( karne ya 19) jimbo la pekee la Yerusalemu liliundwa.'' Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Uingereza ulitawala eneo hili kama eneo la kukabidhiwa la Shirikisho la Mataifa, na eneo hili lilikuwa pamoja na sehemu kubwa upande wa mashariki wa mto Yordani. Waingereza waligawa eneo katika sehemu mbili upande wa magharibi (Palestina yenyewe) na upande wa mashariki wa mto Yordani uliokuwa baadaye milki ya Yordani.
Kwenye sehemu ya magharibi iliyokuwa Palestina yenyewe kulikuwa na uhamiaji wa Wayahudi kutoka nchi za Ulaya ulioweka msingi kwa mapambano kati ya Israeli na Palestina ya baadaye.
Mwaka 1947 Umoja wa Mataifa uliamua kugawa Palestina katika sehemu tatu zilizopangwa kama Dola la Kiyahudi, Dola la Kiarabu na Yerusalemu kama mji wa kimataifa. Lakini Wayahudi walitangaza uhuru wa Dola la Israeli. Wenyeji Waarabu walipinga azimio hili na vita ilitokea. Baada ya mkataba wa kusalimisha amri Israeli mpya ilikuwa na sehemu ya Palestina kubwa kuliko awali. Asilimia kubwa ya wakazi Waarabu wa sehemu zilizokuwa chini ya Israeli mpya walikimbia au walifukuzwa nje. Ukanda wa Gaza ulishikwa na Misri na Ukingo wa Magharibi wa Yordani ulitawaliwa na milki ya Yordani''